Ngoja niwasaidie kidogo tu;
Jasusi ni mtu anayeajiliwa na Serikali ya nchi yake au taasisi ili kupata taarifa za siri toka kwa mataifa mengine ya nchi nyingine, shirika au makampuni yaliyo ndani na nje ya nchi.
Tafsiri nyingine ni kwamba jasusi ni mtu anayetumia mda wake kutazamana na kuchunguza watu wengine...katika dunia ya leo Jasusi anatakiwa kuwa zaidi ya maelezo ya hapo juu na ni laziima watu wa aina hii wawe wa kisasa zaidi ili kuendana na hali haslisi ya mazingira na mabadiliko ya teknolojia.
Jasusi wa kisasa ni lazima aishi kati ya maadui, ajifananishe nao, aongee lugha yao, awe na urafiki na lakini zaidi ya yote ajifunze na kutambua mbinu za adui zote na namna ya kukabiliana nazo....
Jasusi lazima ayajue mazingiwa ya eneo analoishi kwa ufasaha na jasiri mwenye utayari wakati wowote. ni lazima jasusi afundishwe mbinu na mafunzo ya awali ya kijeshi hasa yanayohusisha matumizi ya silaha aina mbali mbali, namna ya kujilinda lakini pia lazima afundishwe mbunu za kugoma kuhojiwa hasa pale anapotiwa mikononi mwa adui
Mazingira ya kazi ya kijasusi ndugu zangi wanaJF ni mazingira yaliyozungukwa na hatari, upweke na ''kivuli'', na hivyo Jasusi ni lazima awe amejifunza mbinu zote za kazi hii (tradecraft)
Sifa za Jasusi:
1. Sifa ya kwanza ya Jasusi ni lazima awe na uwezo kuchunguza (observation).. Haijalishi mazingira ya mahali alipo na anafanya nini, akili ya Jasusi ni lazima we ina rekodi maeneo, matukio, na watu waliopo huku kiwango cha kumbukumbu kichwani kiwe kikubwa na cha hali ya juu...Lazima ajifunze na akumbuke vitu vya aina nyingi kwa wakati mmoja na vyote viwe vya usahihi...
Mfano akiingia ndani ya nyumba chini ya dakika moja na nusu lazima awe amshajua nyumba hiyo ina vyumba vingapi milango mingapi madirisha... Kama kuna gari limeegeshwa lazima ajue plate namba zake nk...na nilazima vitu hivyo vikae kichwani kwa mda mrefu hata mwezi mmoja..
Vijana wengi hawana kumbukumbu nzuri, na hili ni tatizo kubwa. Mtu hata kukumbuka namba za simu hata kumi kwa wakati mmoja ni ngumu...Wengi wa watu niliokutana nao wengi wanaangukua katika kundi la 7+_ 2. .
2. Sifa ya pili ya Jasusi ni lazima atumie mantiki(logic)katika kuelewa vitu nakufikiri..na sifa hii ni muhimu sana .lazima ajue kwa nini hiki kiko hivi na hik kiko hivo na pia ajue namna ya kukifanya tofauti na kilivyo kuwa awali si katika muonekano tu bali pia katika ufahamu pia.
3. Jasusi ni lazima ajue kubadili tabia kulingana na mazingira na eneo alilopo na pia tukio husika. lazima ajue watu wanaomzunguka wanataka nini na ni watu wa aina gani...Hii itamsaida kujua aenende vipi katika mazingira hayo. Jasusi lazima ajue kucheza ana hisia za watu.. Hii ni sifa muhimu sana tena sana...
4. Jasusi ni lazima asikilize na Awe na Uwezo wa kusikiliza milango yote 7 ya fahamu (Wengi mnajua milango mitano), na achambue kwa uharaka nini cha kufanya kama yu katika hatari...Ndugu wanaJF katika ubongo wa mwanadamu kuna maelekezo mengi sana yanayomuonya binadamu juu ya hatari yoyoe. Jasusi ni lazima ajifunze maelekezo hayo na achukue hatua stahiki pindi anapokuwa katika hatari....
Mfano jasusi akiwa anatembea mitaani akifanya kazi yake kisha akakutana na mtu aliyemuona mtaa mwingine saa moja lililopita, Jasusi ni lazima ajiulize, ''Hii ni kawaida au nafatiliwa''?
5. Jasusi hatakiwi kuwa mkurupukaji, anatakiwa achukue stahiki na kokotozi kwa hatari iliyoko mbele yake au upande wa pili kwa kurekebisha plan zake kulingana na mahali alipo.. Lazima atafakari hatua za kuchukua na ni lazima hatua hizo ziendane na taarifa muhimu kulingana na eneo husika...Kama jasusi ni mkurupukaji, ni lazima hatafikia malengo ya kazi yake..
Sasa ili mtu aingie huku kuna mambo mengi lazima yaangaliwe...uwezo wake kichwani, unapenda nini, unaTaka nini katika maisha yako, ukoje...Kuna watu hawajui na hawajifahamu kabisa hata akisimama na kuanza kutembea ni mguu gani unaanza kutangulia, lazima tabia yako ijulikane...
Na kuna njia nyingi za kutambua tabia za mtu ikiwa ni pamoja na namna anavyotembea, namna anavyopanga au mpangilio wa vitu ndani ya nyumba yake au chumbani kwake (unaweza kuingia chumbani kwa mtu na kuangalia mtu muonekano wa chumba kilivyo na hapohapo ukajua mtu huyo akiwa njiani anafanana vipi bila hata kukutana nae), mwandiko wa mtu nayo ni njia ya kujua tabia ya mtu, namna anavyolala (Kifudifudi, kulala chali, kulala kwa ubavu huku umejikunja na mkono mmoja kuweka kichwani kama mto wa kulalia huku mkono mwingine umeubana katikati ya miguu), paji la uso hasa mtu akiwa anaongea n.k...So kuna njia nyingi za kujua ni mtu gani anafaa...
So sio kazi rahisi tu ya kuamka asubuhi ukapiga mswaki na wakati umetoka kuoga huku umejifunga taulo unapaka mafuta kisha unasema naenda kujiunga na kazi ya Ujasusi...Kwanza ukionekana unaitaka na ukabainika, lazima uwekwe kwenye rejected file au hata uenguliwe katika hatua za mwanzo kabisa...Ukionana na wakakuona ''wenyewe'' na ukaonekana unafaa basi watakuchukua tu...
Muda umeniishia.. hadi wakati mwingine ndugu zangu..