harusi inatakiwa iwe nzuri ya kuridisha lakini isiwe na israf na ufujaji wa pesa wala kujionyesha.
nafikiri tutakapoanza kufanya harusi kwa uwezo wetu tu bila ya kuchangishana basi tutafanya harusi z kiasi
Mzee ume-summarize kila kitu. I see the future ...
nashukuru mungu na namuomba aendelee kunisaidia niwe nakaidi kuchanga.
Tuko pamoja. Mwanzo mgumu lakini wataelewa tu ...
dawa ni kugoma kuchangia! Kwani hawataoana?? Watu wanapendana huko halafu kero na usumbufu kwa wengine!
Yaani mtu unafuatwa na michango ya harusi..utadhani una deni la mtu!
Watu bwana! We acha tu!
Hahaha utamaduni hujengwa na watu wenyewe. Ukikubali kuchangia ujue unasaidia kuuendeleza utamaduni. Usimlaumu yeyote bali we mwenyewe.
ukianza kuhesabu utaona ni nying sana ila ni mambo ya kijamii zaidi huwezi kukwepa. ila inabidi system ya harusi nzima ibadilishwe maarusi wawe wanapewa kiasi kikubwa tofauti na ile zawadi ya kamati
Jisemee mwenyewe. Sema "siwezi kukwepa". Wenzako wengine wanaweza.
Kuchanga inategema na unavyojisikia. Sioni haya wala aibu kuchanga elf 15, 20, 30 kadiri na nipatacho na ninavyojisikia na ukaribu wangu na mhusika. Na kama sina au sijisikii sikupi tu na nakuangalia usoni nakwambia - sina kwa sasa. Sitakuwa mtumwa kamwe wa kuchanga michango ya harusi za kifahari bila sababu, unajikuta una kadi kumi kwa mwezi, mkeo tano, mkitoa elfu 50 nlika kadi ni Tshs laki 6. Shauri zenu na sifa zenu. Jamaa zangu nawaambiaga, ukitaka harusi ya kifahari, kaza buti tafuta hela, ila sitatembeza mikadi kila mahali.
Nimependa msimamo wako. Ila we hukuwachangisha?
🙂 Maana nilicho notice kingine ni kwamba watu hawapendi kuchangishwa (na inawaauma kweli kuzitoa) lakini kwenye zamu yao wanakuwa experts wa kukusanya michango. I don't know what happened to "do unto others what you would like to be done unto you".
Si vibaya kumsaidia ndugu au rafiki kukamilisha vizuri shughuli kama hiyo ambayo ni muhimu sana kwake. Lakini katika mtindo huu wa kisasa, mtanisamehe bure tu.
Kosa la kwanza wanalofanya ni kuniambia ni-pledge. Huu ni mtindo mmbaya sana huu. Yaani ni kama kamfumo flani ka kutumia peer presure kumlazimisha mtu kutoa zaidi ya uwezo wake. Mimi nimeacha ku-pledge kabisa. Nnatoa kama nnajisikia kuto kwa kiasi nnachoweza na kutaka kutoa wakati ninatoa. Nilimuonea huruma rafiki yangu mmoja aliponiweka kwenye laud-speaker wakiwa kwenye kikao na washkaji wengine akidhani kwamba hiyo ingesaidia.
Mwingine alishangaa nilipo-pledge 500; imefika zamu yangu nnawaomba kwa utaratibu wani-excuse maana sintoweza ku-pledge kabla ya kuangalia budget yangu wao hawanielewi (maana hata shughuli yenyewe hatukuambiwa ni ya nini mpaka tunafika pale). Basi nikawaambia 500. Wakacheka wakidhani nnatania; iliwachukua muda kidogo kutambua kwamba sitanii. Nikatimiza ahadi, lakini sikuja hata kuambiwa harusi inafanyika lini.
Naungana mkono kabisa na Gaijin. Watu waanze kutayarisha harusi zao wenyewe kadiri ya uwezo wao. Mtu akiamua atumie 25M yake yote kwenye harusi yake, that is fine with me. Lakini hiyo 25M inapotoka kwa wengine, tena baadhi yao inabidi wachague kati ya kutoa mchango au kupeleka mtoto shule, inaanza kuwa mbaya kabisa.
Juzi juzi hapa ndugu mmoja aliye katika harakati za kuchangisha aliniomba nimpe namba ya ndugu mwingine ili akakusanye na huko. Hapo ilikuwa haijapita hata wiki mbili tumetoka kumkopesha huyu ndugu wa pili pesa za ada za watoto waliorudishwa nyumbani. Hivi nilikosea nilivyomnyima? Yaani hata hatutaki kujua watu wanaishije au wanatoa wapi hizo pesa, tunataka michango tu. Ndio maana ndoa nyingine zinakufa so prematurely, unakuta mmekusanya mpaka pesa za dawa za wagonjwa halafu mnategemea hiyo ndoa idumu kweli?
Unajua hata kama unachangisha watu, kumbuka hawa ni binadamu na wana mahitaji yao binafsi. Na hujui hizo pesa wamezitoa wapi, au wamefanya nini kuzipata. Usipite kama vile wana visima vya hela majumbani kwao, na kwamba wana wajibu wa kukupa wewe, au walikuwa wanakusubiria wewe upendane na mtu ndio zitumike.
At least usije kwangu kuchangisha. Nitaarifu tu kwamba unao/unaolewa, kama inakupendeza mimi kujua.