Folks, this is what happens when the basic qualification for leadership in the country is being good at corruption and deceit. Kwani tulidhani ni nini kitafuata? Walitoa hela kwa kuwa kwao ile ni biashara tu! Unatoa mtaji, halafu unatafuta faida! Simple as that.
Mathalan, hata uteuzi wa wajumbe karibu wote ulibebwa na rushwa, hata kama siyo za moja kwa moja. Najua wengi hawatanielewa. Lakini ilie tu kuwa waliteuliwa na Rais, amabye he turns out to mwenyekiti wa CCM, amabye kipindi anakampeni tulishuhudia jinsi alivyoshiriki kampeni kwa kejeli na matusi, rushwa na wizi, bila kusahau kubebana katika uteuzi ndani ya chama! Unategemea kizaliwe nini hapo? Uzalendo? Kweli? Katika utaratibu huo kilichotengenezwa ni kusanyiko la wanasiasa-mafisi, wenye uchu na uroho wa kila senti inayopatikana karibu.
Lakini bado nawshangaa na wle wenzetu walio bungeni! Ilikuwaje wakakubaliana na upuuzi huu tangu mwanzo? Kwa wanaojua, kulikuwa na kasoro tangu kuundwa kwa sheria ya katiba. Sheria ilionyesha wazi kukwama kwa mchakato wa katiba mapema. Kivipi? Pale iliposema wazi kuwa:
1. Wajumbe wa bunge Maalum la Katiba watakuwa:
i. Wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya muungano-wa kuchaguliwa na kuteuliwa!.....ambapo hata mjinga anajua kuwa katika hali ya kawaida hakuna uwiano wa idadai katika bunge hilo. Kwamba wale mafisi ni wengi kuliko wengine! Lakini hata hao wengine wakakubali!!!!!
ii. Ili kuleta uwiano wa uwakilishi katika Bunge Maalum la Katiba kutakuwa na nyongeza ya wajumbe 201 kutoka makundi maalum........wajumbe hao watateuliwa na rais baada ya kuchaguliwa na vikundi vyao na majina 3 kuwasilishwa kwa Rais..... Kwamba wote hawakuona kuwa Rais anayetajwa ndiye mwenyekiti wa Chama cha Mafisadi-CCM, chama ambacho kimekumbatia mafisadi kwa muda mrefu na kwa nguvu zote. Kwamba hata yeye Rais ana kashfa yake ambayo haisemwi tu kwa kumwogopa! Kwamba hata hao wenzetu waliona Rais huyo anafaa na anatosha kufanya kazi hiyo ya uteuzi? Kwamba ana sifa za kutosha kututeulia wawakilishi waadilifu wakati yeye mwenyewe hajwahi kuwa muadilifu! Au tulitegemeaje? Kwamba ukimtuma fisi akalete marafiki zake ataweza kabisa kuwa na uwezo wa kuleta kuku eti tu kwa kuwa ni waadilifu! Kwa hali ya kawaida hata mtoto angeweza kujua kuwa ukimpa kazi hiyo fisi ataleta fisi wenzake! Ajabu ni kuwa hawa wenzetu hawakuona hilo, hata baada ya mimi kuwaandikia baadhi yo mapema tu-wakati wa kuandika sheria hiyo!.....kuna wakati nakosa imani na wanasiasa kabisa!
Lakini nimalizie kwa haya ya mwisho. Kwamba Serikali ilishatoa tamko kuwa Katiba hapana! Waziri Kombani na Mr Mwanasheria mkuu wakasema haihitajiki, mara ghafla rais anasema itaandikwa. Mara kama ndoto CCM imeshika kibendera cha katiba kama siyo wao waliosema haihitajiki- hakuna aliyeamka wala kustuka! Mpaka ikapitishwa sheria mbovu haaaa-salama kabisaaaaa! mara uteuzi ukawa una maluweluwe haaaa! baridiiii kabisa. Leo matusi na kejeli yameanza ndiyo tunakurupuka kuwa hatuko sawa! Leo mafisi yanapitisha vifungu kwa ubinafsi na ubabe ndiyo tunajuwa wametuzidi idadi! huu ni upunguwani!
Kana kwamba haitoshi, imekuja hii ya mwisho, kwamba hata rais anaona katiba imeshindikana lakini hataki kuchukua maamuzi magumu. Wao waendelee kule Ddodma kufuja hela na mchakato utaendelea baada ya uchaguzi!!!! Nadahni tukubalianae tu kuwa:
Kwa kuwa CCM iliona hakuna haja ya katiba, na kwa kuwa iliamau kwa makusudi kuamua kuuharibu mchakato huo ni wazi kuwa lengo halikuwa katiba bali ulaji kama kawaida! na ndiyo maana hata baada ya kuona katiba haitaweza kupatikana, bado tumeendelea kujiweka bungeni na kulipana posho huku tukijua kuwa katiba haitapatikana!
Kinachonishangaza tu ni kuwa hawa wanafanya haya kwa kuwa sisi wananchi tuekubali wayafanye. Ni kwa nini tumewapa mamlaka hayo? What are we gonna do about it?