I was once in a position like yours! Ilikuwaje na nilifanya nini...endelea then amua mwenyewe mkuu
Noel 2014
Tulitokea kumpenda msichana mmoja mimi na rafiki yangu na tuliambizana wote tukiwa na washikaji wengine. Tulijadiliana na kutoka kwenye majadiliano, jamaa akasema mbele ya washkaji wengine kuwa ameamua kunipa go ahead nifanye yangu kumpata msichana. huyo msichana alikuwa ni rafiki wa dadaake huyo jamaa alienipa go ahead.
Nilifanya yangu na kweli binti akakubali nikawa nae. Baada ya muda nikaanza kuona mambo ambayo hayaeleweki baina ya binti na mshkaji wangu na nilipofanya uchunguzi wangu, nikagundua wanakulana (nilipata ushahidi kwa kuona pichu ya binti kwenye begi la jamaa akiwa ameificha chini kabisa ya begi - ni moja ya uchunguzi wangu).
Nini nilikifanya?
- Baada ya kukusanya ushahidi wa kutosha, nilichokifanya ni kuanza kumdelete binti taratibu taratibu. Nilipunguza mawasiliano nae mwisho nikayakata kabisa. Nilikuja kuonana nae tena mahala pengine akataka kunizoea, nikampotezea.
- Mshikaji nae sikumwambia kitu na nikamuachia binti kimya kimya na mpaka leo bado tunawasiliana na mshikaji ila kwa kiasi kikubwa nimepunguza kumshirkisha mambo yangu
My take:
Fanya uchunguzi na jizolee data na ushahidi wa kutosha. Ukithibitisha wanakulana, achana na binti kimya kimya (huna haja ya kuongea nae) na mshkaji punguza kumsirikisha mambo yako ya ndani kwani aatakuwa ameprove kuwa si mshkaji wa kuaminika kwako