HOUSE GIRL - MWIZI & MCHAWI ; True story! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOUSE GIRL - MWIZI & MCHAWI ; True story!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lokissa, Sep 10, 2012.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  ilikuwa tarehe 21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa
  kike (mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana
  na atakuja nae home jioni akifunga saluni.

  Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.

  Mdogo wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake
  akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa
  anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama
  mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano
  ya ndugu yeyote ila baba yake anishi mwanza but hanjui mama yake. Basi
  mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni
  na nifanye nae mahojiano ya kina.

  Jana majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula
  ikabidi nianze kumhoji yule binti.

  Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na nia yake ni kufanya kazi za
  ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia then angerudi tena
  kuendelea na kazi yake.

  Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.

  Baada ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu
  ni lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na
  alikubali.

  Nikaenda kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho
  asubuhi (yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na
  kuandikishana.

  Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema
  asubuhi after mlango na geti kufunguliwa.

  Majirani wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda
  kutupa taka coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na
  chumbani kwa kina dada ikaonekana everything is OK.

  Basi nikawmambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then
  mimi nikaondoka zangu kuelekea job.


  Here comes the story part II.

  Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu
  anitaarifu yaliyojiri:


  Akaniambia yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani
  karibia na barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata.

  Walimpiga kidogo na kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa
  aliziiba ktk wallet ya mdogo wangu.


  Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi saluni kwake
  kimanga ili akamhoji zaidi.

  Yule binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea morogoro but anaishi na
  bibi ake mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.

  Akasema kuwa bib ake ni mchawi na huwa anamtumaga kwa nyumba za watu kwa
  mbinu ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo
  kimazingara.

  Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine
  wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.

  Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni.

  Akasema kuwa jana alipoingia getini bibi ake alikuja kimazingara but
  ghafla macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi
  ake akaondoka.

  Ilipofika muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta
  mdogo wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu
  akakimbia kurudi sebuleni.

  Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona
  yule binti hana amani.

  Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka
  akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala.

  Yule binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na
  kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto
  ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu.

  Akasema tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi
  tumeweza kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi ake alimjia
  kimazingara na akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri.

  Alionesha CHALI alizochanjwa na bibi ake kama kinga na alipokuwa
  anapigwa hakusikia maumivu yoyote.

  Alielezea mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea ktk simu
  kwani nae alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyoukuwa yanatokea.
  Walimuachia akaondoka zake.


  I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.

  Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to
  your relatives and beloved.


  NAWASHIRIKISHA KISA HIKI CHA KWELI
  ila hakijanitokea mimi ni rafiki yangu
  .
  SIKU NJEMA   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Mhhhh . . . . . . . . . . . . !!
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Poleni sana Ila muelewe kuwa Mungu amewaangazia mema, neema na ulinzi wake. Mumtumaini
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  UCHAWI UPO LAKINI HAUTA MDHURU MTU YOYTE KAMA MUNGU HAJATAKA.

  [SIZE=+1]SURA AL-BAQARAH: Verses 102-103[/SIZE]

  And they followed [instead] what the devils had recited during the reign of Solomon. It was not Solomon who disbelieved, but the devils disbelieved, teaching people magic and that which was revealed to the two angels at Babylon, Harut and Marut. But the two angels do not teach anyone unless they say, "We are a trial, so do not disbelieve [by practicing magic]." And [yet] they learn from them that by which they cause separation between a man and his wife. But they do not harm anyone through it except by permission of Allah . And the people learn what harms them and does not benefit them. But the Children of Israel certainly knew that whoever purchased the magic would not have in the Hereafter any share. And wretched is that for which they sold themselves, if they only knew
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Daaa, ni kisa cha kusisimua sana. Kwa hali ilivyosasa ni vzr sana kuwa makini na watu tusiowajua na hasa hawa mahousegel na wale wanaokuja na gia ya kuwa ni wageni na hawana mwenyeji maeneo ya karibu. Ni kweli wapo baadhi ambao ni waaminifu na unakuta ni watu wenye shida ki-ukweli lakini kwa kuwa dunia imebadilika, ni vyema sana kujiuliza mara mbili mbili unapotakiwa kumsaidia mtu wa aina hii.

  Ktk hili najisikia kuongelea suala la mahousegel na maisha yao majumbani. Kwa kweli tunatakiwa tujue namna ya kuishi na hawa ndg maana hao ndiyo tunaowakabidhi watoto wetu, nyumba zetu, mali zetu, waume zetu (kwa wadada) nk. Wao ndo wapishi wetu wa kila siku na wana uwezo wa kutulisha na kututendea jambo lolote baya saa yeyote. Ni vyema unapochagua housegel uwe makini mno ukizingatia ndiyo anakuwa kama msaidizi mkuu wa nyumba.

  Tumesikia matukio mengi mabaya wanayoyatenda mahousegel kwa akina mama wasioishi nao vzr ikiwepo kumfungia mtoto ndani ya friza, kuna mwingine alimuweka mtoto kwenye sufuria la maji ya moto juu ya jiko na kuliwasha, wengine wanadumbukiza watoto visimani nk nk. Ni vyema kwa wenye familia kuwa makini kwenye uchaguzi wa hawa watu na kuishi na kwa hekima na upendo pia.
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Fazaa hebu tuwekee na maandiko ya kiswahili wengi tuelewe
  nimeipenda verse yako
  cha msingi ni kuwa na imani na uchaji mda wote
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wasichana wa kazi siku hizi sio wa kuokoteza kabisa......inabidi kuwa makini nao sana manake wengi wana nguvu za giza sana......nshakutana na kisa kama hiki lilimtokea rafiki ila yeye hakuibiwa na msichana alikuwa anatokea moshi.....alitoa siri nyingi sana ila yeye alikuwa anafundishwa uchawi na mama yake! Ukihadithiwa unaweza kuzani ni uongo ila kiukweli hivi vitu vipo sana siku hizi!

  Ongezeni kusali sana manake dunia ni kama imegubikwa na giza nene!
   
 8. awp

  awp JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  sura al-baqarah ni sura ya ngapi? nithibitishe
   
 9. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hadithi huwa jioni bana saa hizi bado tupo mihangaikoni
   
 10. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,134
  Trophy Points: 280
  pole yake mkuu, aombesana Mungu aendelee kumlinda....
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Allah ni mwema kwa wote
  ni bahati kuwa katika nyumba wapo watu wanasali bila hivo ingekuwa hadithi nyingine
   
 12. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Hii story nimeisoma wiki iliyopita ililetwa na mtu kama ilivyo........i smell ni Shigongo copy!
   
 13. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu amesaidia duh! haya mambo yamekuwa yakijitokeza sana hapa Dar cha msingi inabidi tuwe waangalifu. sometimes huruma inatuponza.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  we pata msg mkuu na wape wengine habari ambao hawajaisoma
   
 15. Blue G

  Blue G JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 4,887
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Pole sana kwa huyo yaliyemkuta but asante sana kwa kutualert.Hii ndo maana sahihi ya ujamaa.
   
 16. Blue G

  Blue G JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 4,887
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Not hadithi bro haya mambo yapo na ni vizuri kuwa makini.okay???????
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Vile hayajakukuta ni haki yako kufikiri kuwa hii ni hadithi!

  Ila kiukweli yapo !
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  omba Mungu kisa hiki kisikupate tumekiweka ili kuokoa nyumba zetu.
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Shigongo's apprentice ??
   
 20. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160

  Mie niliforwadiwa kwenye email kama last two weeks hivi......copy and paste inahusika sana hapa
   
Loading...