House girl/ house boy inalipa kweli?

fourtypercent

Member
Jun 4, 2011
53
20
Jamani wanandugu, kitu hiki kimekuwa kikinipa shida sana mimi, unakuta mtu ndugu yake au rafiki yake labda amemaliza la saba au form 4 ya 'Mulugo', katika kutaka kumsaidia anamtafutia kazi hii, je unapomtafutia kazi hii unaamini atatoka kweli? maana kwa uzefu wangu watu hawa wamekuwa wanaambulia matatizo mbalimbali hasa ukikuta mabosi wao hawajatulia, na mara zote wakichoka hizo kazi zao huwa wanakosa mwelekeo.

MY TAKE
Tujaribuni kuwapa ushauri au msaada ambao at least utamtengenezea future yake nzuri, mfano kumshauri aanzishe kibiashara hata cha mtaji mdogo(na ikiwezekana umuwezeshe), au aanzishe kilimo cha bustani au cha aina yoyote ili mradi awe na malengo maalum, mi nahisi utakuwa umemsaidia zaidi kuliko hizo kazi. NAWASILISHA
 
fourtypercent unachosema ni kweli, kumtafutia mtoto kazi ya u-house boy/girl inaweza kuwa si jambo zuri endapo watoto hao wataangukia kwenye mikono ya akina baba/mama wapenda dogodogo au akina baba/mama wasiojali utu na heshima ya watoto wa wenzao. Wapo baadhi ya watu walionufaika na kazi hizo kwa kusomeshwa na kutafutiwa maisha na mabosi wao.

Ila pia wapo walioambuliwa kubakwa, kunyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa na baadhi ya mabosi wao. Kikubwa nafikiri si aina ya kazi, bali kuwe na mabadiliko ya kitabia kwa wazazi wanaoajiri ma-house girl/boy na kulinda heshima na utu wao. Ni vyema kuwatreat watoto/ndugu hawa kama watoto/ndg zetu wa karibu. Tuache ukatili maana hata sisi tusingepata elimu na vijikazi vya hapa na pale, huenda tungeangukia huko hususan kwa nyakati hizi ambapo ajira imekuwa ni tatizo ...

Nafikiria pia kipuuzi, tusingekuwa na mahouse girl/boy, hali za familia zetu kwa sisi tunaoishi mijini ingekuwaje? Naomba nisinukuliwe hapa wala kueleweka vinginevyo, ni fikra tu .....
 
waofaidika kusomeshwa ni wachache mno ukilinganisha na kundi kundi kubwa la wanaohangaika na maisha baada ya kuachana na kazi hiyo, mfano mzuri kuna dada nimekutana naye kwenye basi(tulikaa siti moja) katika mazungumzo ya hapa na pale ndani ya basi mwisho wa safari tukabadilishana mawasiliano. katika kuwasiliana analalamika sana maisha magumu kiasi kwamba anashindwa kuyamudu, katika kumdodosa aliniambia siku tunakutana kwenye basi alikuwa anatoka huko alikuwa anafanya kazi za ndani sasa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake kaamua kurudi kijijini.

na aliyemfanyia mpango kuo ni ndugu wake wa karibu na huyo ndugu yake anakauwezo fulani, kwa muda wote huo angemsaidia kwa njia nyingine angekuwa amefika wapi maana kafanya hiyo kazi more than 8 years!
 
Inabidi huyo anaesaidiwa aweze kusimama imara na kutumia akili na maarifa kufanikisha mambo. Nadhani ukimpeleka ndugu au rafiki aende kufanya kazi za ndani unachunguza muajiri wake angalau kabla ya kumpeleka, si ndio? Kazi ni kazi. Kama kweli anafikiria kujikwamua na umasikini inabidi ajitahidi kubuni njia itakayomwezesha kuacha kazi za ndani. Anaweza akaanzisha biashara ili asiwe tegemezi kwa ndugu zake, na asiwe anasubiri kupewa kamshahara kila mwisho wa mwezi.

Ndio, kuna matatizo mbalimbali ambayo yanajulikana kwenye mambo ya kazi za ndani, lakini si lazima atakumbana na hayo matatizo sehemu zote atakazofanya kazi. Kazi ni kazi; ogopa ndugu yoyote anaechagua kazi. Atakuwa mzigo kwako na kamwe hatajua thamani ya pesa kama hawezi kufanya kazi kwa bidii. Msidekeze watu wazima. Huyo dada nae miaka 8 yote hayo alikuwa anategemea kupandishwa cheo au??
 
Hiyo ni kazi kama kazi zingine tena anaweza akawa na mshahara mzuri kuliko hata Secretary na dereva wa Serikali cha msingi ni kushauri wadau mbalimbali watende haki mara wanapowaajili watu hawa.Mshahara wa secretary na dereva serikalini ni TShs 170,000.00. Sasa kama house girl / boy analipwa 60,000.00 huku malazi, mavazi, chakula na matibabu anapatiwa na mwajiri wake hapo nadhani ukikaa chini ukakokotoa vizuri huenda akamzidi mfanyakazi wa serikali kima cha chini.
 
Unapozungumzia msichana wa kazi, sijui mnazungumzia wa kiwango gani, mimi wapo ninao wafahamu wanalipwa mshahara laki na sabini pamoja na marupurupu kibao.
wote ni form 4 na F6.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom