ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,476
- 9,654
Saa chache kabla ya Marekani kufanya shambulio la makombora kwenye ngome za jeshi la Syria, Hillary Clinton alitoa ushauri kwa serikali ya Marekani kupiga mabomu ngome za jeshi la anga za Syria ili kuzuia kuruka kwa ndege za jeshi hilo(syria).
Kwenye mahojiano na Newyork Times hayo alisikika akisema " Ninaamini kabisa kwamba tulipaswaa na bado tunapaswa kuharibu kabisa viwanja vya jeshi la anga la Syria(airfields) kuzuia mashambulizi zaidi kwa raia wasio na hatia na kudondoshewa gesi za sumu".
Aliendelea kwa kusema kwamba angependelea hatua kali zaid zichukuliwe dhidi ya matendo mabaya ya Assad, na kuongeza kwamba "anajilaumu kwa kutokua na msimamo thabiti dhidi ya Assad wakati alipokua waziri".
Full interview
Je, unadhani kama Hillary Clinton angeshinda Urais Marekani hali ingekuaje huko Syria?