Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
```Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu```
 
Walio madarakani yaani ccm
-wanahofu ya kudondoka
-hawajiamini
-wanadhani upinzani ndio adui wao
-hawajuwi kuongoza, wao nikukandamiza
-hawana dira (short or long time plan)

Kwa maana hiyo wanajikuta kuzusha na kudanganya RAIA.... kisingizio upinzani ilhali wanachonga kinyago nakukiogopa mwenyewe. Tangu Uhuru 1961, Taifa hili linaongozwa na ccm yaani Tanu kisha 1977 ccm. Hawa wapinzani hawajawahi shika uongozi wa Taifa hili ...... Vipi wasingiziwe kukwama kwetu kiuchumi? Usiwe ccm
 
Matokeo ya kukwepa kuwajibika, ccm wanajikuta kutapatapa na wapinzani popote, kutwa kuacha. Tunajikuta badala ya kuimba Sera za kutukombowa kutoka umaskini.... Tunaimba...chadema, cuf....chadema, cuf..... Chadema, cufu.....

Ccm ni tatizo kubwa katika uzushi na unafiki

Chedema chama cha wachaga

Chadema chama cha wakristo

Cuf chama cha waislam

Cuf cha wapemba

Ccm haishi uzushi na propaganda chafu
 
```Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu```
Ni kweli kabisa hata Mahabusu katika hotuba za wanasiasa wanaitwa Wafungwa wa kisiasa!
 
Umebadili Heading tu, ila content yote ni ya Edo Kumwembe, halafu umejifanya kama we ndo mwandishi vile, hujatoa credit kwa Eddo, poor you brother!!
 
Mimi naandika kitu ambacho nina uhakika nacho,mada hii imeletwa jana hivi hivi kama hii na mwandishi wake ni Edo.
Kama haujaiona usiropoke ropoke.
mkiambiwa mna akili za kukariri mnaita watu malofa mwandishi anatuhusu nn wewe na mimi? issue pale ni contents ambazo zipo valid jana leo mpaka hata mwakani! jasho linakutoka kisa mwandishi?
 
Ni kweli kabisa hata Mahabusu katika hotuba za wanasiasa wanaitwa Wafungwa wa kisiasa!
mwaka wa tatu watumishi hawajaongezewa mishahara. bwana BASHITE aliyeiba vyeti bado yupo akihudumu kwenye ofisi ya uma na mahakama imebainisha pasi na shaka kwamba bwana lukuvi alimkwida mtu na kuchukua dola 40000. na kwamba bwana makonda alingiza makontena bila hata kulipa ushuru.
hapa kazi tu?
 
kukosa ajenda kubaya sana , anapozungumzia SGR, RELI, MAJI mnasema anarudia rudia yaleyale, anapozungumzia siasa mnasema anatajataja vyama. watanzania wanashindwa kuwaelewa hata kidogo
 
Ccm agenda yao kubwa ni kujadili utajiri wao kwanza na sio kusaidia watanzania. Wapinzani wakitoa ujembe reflective, lazima ccm uwachome. Kwahiyo kuishiwa Kwa hoja ccm Hakuna hoja yeyote ya wapinzani kupuuzwa by ccm.
 
yaani jana nimechangia mada hii halafu na leo nichangie tena mada ile ile?
Halafu kwanini unafanya plagiarism?
Mwandishi anayejitambua anatoa credit kwa mumiliki wa andishi.
Mmesoma shule gani nyie vijana?
Kinoamiguu
kusema tu ilitoka jana ni kuchangia... umejua lini maana plagiarism mkuu?ile ya jana ilikuwa ya edo kweli ama ilikuwa na jina lake tuu
 
Back
Top Bottom