Hotuba za Rais Wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba za Rais Wetu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sabi Sanda, Dec 24, 2009.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Salaam kwenu wote,

  Naomba msaada wenu. Kwa muda sasa sijapata fursa ya kumsikia na kumuona Rais wetu akihutubia taifa kupitia utaratibu wake wa kuongea na Watanzania kila mwezi kwa njia ya televisheni na redio. Je huu utaratibu umekufa? au ni mimi tu ambaye nimezikosa hizo hotuba za Rais za kila mwezi?.

  Nimeangalia tovuti ya taifa (www.tanzania.go.tz) bahati mbaya ukurasa wa hotuba za Rais haukufunguka japo kurasa zingine zimefunguka.

  Pia tuwaombe wahusika ofisi ya Rais wa-update LINKS/KURASA zinazomuhusu Rais bila kusahau masuala na taarifa nyingine muhimu kwa taifa letu.
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi mambo yanavyokwenda ndani ya nchi hii kwa sasa inahitaji ujasiri usikuwa wa kawaida kuweza kuhutubia taifa. Sababu iko wazi, kwani huwezi kutoa hotuba ya kawaida wakati serikali na chama chako ndio habari magazetini. Katika hali hiyo basi, ni lazima kila unapo hutubia ujibu kwanza yale mambo ambayo ni hot ki taifa na yanayohusu utawala wako na chama chako ndipo kama una chochote cha kimaendeleo uweze kuwaeleza wananchi.

  Kwa hivyo zoezi linakuwa gumu kwani kila wakati unatakiwa uwe unakidhi matarajio ya wananchi kwa kutoa majibu ya maswali yasiyoisha. Ndio maana aliporudi ziara yake ya nje ya nchi hivi karibuni, aliimba mipasho mbele ya waandishi wa habari na kwamba ni 30% tu ya watanzania ndio wanajua siasa za nchi hii waliobaki hufuata uelekeo wa upepo. Kwa tafsiri haya ni matusi kwa watanzania waliowengi na jibu wanalo tunapoelekea uchaguzi mkuu. Tutegemee nini kwenye chama ambacho wao wenyewe hawaelewani kila mtu anasema lake, watatufikisha kweli?
   
 3. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jayfour_King,

  Nimekuelewa. Je kuna haja ya kuufanya huo utaratibu wa Rais kuhutubia Watanzania kila mwezi kuwa wa kisheria kwa kila Rais atakayekuwa madarakani?
   
 4. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Natumaini mwisho wa mwezi huu tutapata fursa na wasaa wa kumsikia Rais akituhutubia.

  Nawatakia wote Krismas njema na kheri ya mwaka mpya pamoja na familia zenu.
   
Loading...