Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Wosia wa Baba wa Taifa kwa Watanzania
"Mtu yeyote anayeonekana anapenda sana kwenda Ikulu, na hata yuko tayari kununua kura kufika Ikulu ni wa kukwepa kama ukoma. Hafai. Kwanza, hizo fedha kapata wapi? Mtanzania wa leo hawezi kununua watu bila kwanza yeye kununuliwa. Kazipata wapi? Watanzania hawa wote masikini hawa. Mtanzania anaomba Urais wetu kwa hela, amezipata wapi? Kama hajanunuliwa kazipata wapi huyu? Na kama kanunuliwa anataka kuzilipaje. Kama kakopa, atarudishaje?"
 
Hii Kanuni na Wosia wa Baba wa Taifa imeheshimiwaje kwenye kura za maoni za CCM zinazoendelea kutikisa ccm yenyewe? Hizi kauli za Mwl mnazitumia tu mnapotaka kupindisha mambo yawanufaishe wenyewe. Mlisema mnamuenzi Mwl. Ni kitu gani hasa kimefanyika kumuenzi zaidi ya kutumia kauli zake kujinufaisha kwa maslahi ya kibinafsi
 
Acha upoyoyo Tume yenyewe imetenga 5bils kwa ajili ya kampeni(sheria ya uchaguzi),hakuna uchaguzi bila pesa,vipeperushi,mabango,matangazo,kulipa watu wa kampeni,wahamasishaji wako vyote vinahitaji pesa,kuhonga wapiga kura ndio kosa eg kuwapa kanga,kofia,pilau na elfu10 Kama mnavyofanya.
 
Mimi binafsi sifanyi jambo lolote nikihusisha na wosia wa Nyerere kwani alikua ni mzee kama wazee wangu tu wengine sioni kinachomtofautisha mpaka watu tumfanye kama ndio kigezo kwetu. Siamini katika Wosia wa Nyerere.
 
nadhani ihi kauli ya nyerere kwanza ihanzie kwenye chama chenu,

sote tumeshuudia rushwa zikitawala kwenye kura za maoni, kwa macho yetu, kura zikiwa zimeshapigiwa tiki zikiingizwa kwenye masanduku ya kura,

sasa ni vyema unapoongea kwanza ukajikagua je! Wewe upo vizuri?

Kama chama cha mapinduzi kingekua bado ni kile cha nyerere, wananchi wasinge kikataa,

na hofu mlio nayo juu ya lowassa niya nini kama bado chama chenu kinafuata misingi ya mwalimu?

Mwalimu hasitumike kama kichaka cha kuficha uchafu ulio kithiri ndani ya ccm,

siku hizi watu wamesha helimika wanajua pumba na mchele,

kama lowassa angekuwa fisadi hasinge kubali kuama ccm, maana ccm ndio kinga yake juu ya maovu yake,

lakini kama lowassa ameama ccm basi huyu mtu hana hata chembe ya ufisadi,

lowassa ni msafi tena ni mwadilifu kabisa, ila chama chake cha zamani ndio kinachafua watu,
 
Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC
Dodoma 1995
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu
safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake
basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema
aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf
(Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni
tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa
Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza
uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na
ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado
akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi
hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu
hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine
safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua
huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari
kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee
kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi
na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa
mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC
Dodoma, Juni 1995
MYTAKE
JE TUNA MUASISI MWL NYERERE AU TUNAMPINGA? THINK CRICTICALLY.
 
-Aliwahi kufukuzwa na baba yake kwa wizi wa
ng'ombe wa familia ndipo akaamua kukimbilia
kwenye siasa
Alikula hela aliyopewa na Mwl Nyerere kwa ajili
ya kujengea ofisi ya ccm Arusha
Alifanya ufisadi mkubwa kipindi akiwa mkurugenzi
wa AICC Arusha
Kaliingizia taifa hasara kubwa baada ya kuingia
mkataba wa kifisadi na Richmond ambao mpaka
leo unawagharimu Watanzania kwa kupanda kwa
bei ya umeme.
Haitoshi kaona autafute urais kwa gharama
yoyote ile, alianza kuhonga viongozi wa nec wa
ccm, akaja kwa viongozi wa dini, akaendelea kwa
baadhi ya mbumbumbu wa vyuo vikuu wasio
jitambua, na sasa yupo kwenye vyombo vya
habari na baadhi ya taasisi binafsi kama
TW.....EZA.
Mbaya zaidi Kuna wapuuzi wanaojinasibu kama
wasomi wamekuwa wakijaribu kumsafisha kama
mtu safi kwa kisingizio eti ana maamuzi magumu
lakini hawatuambii hayo maamuzi magumu
yamelisaidia taifa kiasi gani zaidi ya kulitia
hasara tu,
wengine wanasema deal ya richmond alitumwa
na wakubwa kuifanya lakini swali la kujiuliza
kama anaweza kutumwa kutekeleza uhalifu dhidi
ya taifa lake na akakubali hivi tukimpa uraisi wa
nchi yetu atashindwa kuliweka rehani taifa letu
kwa mabepari kama anavyofanya jk?
Huyu fisadi kalima ya wizi ipo kwenye damu
tangu akiwa ndani ya familia yake hivi akipata
urais ni kweli utakuwà mwisho wa hiyo tabia
mbaya?
Na atawezaje kukomesha wizi wa mali ya umma
wakati yeye mwenyewe ni mwizi aliyekubuhu?
ikulu kuna deal gani mpaka akukimbilie kwa
kutumia fedha nyingi sana na hizo fedha
atazirudisha vipi?
Kuna wapuuzi wengine wanasema kwa sababu
ana fedha basi apewe urais kwa kuwa hawezi
kuiba tena, bila shaka huo ni uvivu wa kufikiri
maana siku zote mwenye fedha hutaka kuwa na
fedha zaidi ya zile alizonazo na ni wazi kwa hiyo
hoja yao inaonesha ni jinsi gani wasivyoelewa
hulka ya watu matajiri, na zaidi ya yote huyu mtu
wizi upo kwenye damu kutokana na historia yake
ilivyo.
Nihitimishe kwa kuwaomba Watanzania tusijaribu
kufanya makosa kumpa fisi atuchungie mbuzi
wetu maana ipo siku tutajuta pale tutakapoona
mbuzi wetu wameliwa wote.
 
hao manabii wanaofaa wametuletea nini zaidi ya kuiba rasilimali na kodi zetu ?
 
Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC
Dodoma 1995
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu
safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake
basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema
aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf
(Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni
tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa
Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza
uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na
ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado
akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi
hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu
hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine
safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua
huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari
kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee
kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi
na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa
mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC
Dodoma, Juni 1995
MYTAKE
JE TUNA MUASISI MWL NYERERE AU TUNAMPINGA? THINK CRICTICALLY.

Mwalimu alikuwa na mapungufu yake, hivyo siyo kila kitu tumfuate.....lowasa ndiye rais wetu wa hawamu ya tano.
 
Back
Top Bottom