Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Rais Samia leo ametoa hotuba ya kufungua Bunge la 13. Hii ni hutuba iliyosubiriwa na wengi kutoa mwelekeo mpya wa kipindi cha pili cha serikali ya awamu ya sita ambayo kwakweli imepitia kipindi kigumu cha uchaguzi.
Rais Samia ametambua uwepo wa maandamano na vurugu October 29, aidha ameliongoza bunge kuwaombea wale wote waliopoteza maisha. Rais ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, waliojeruhiwa na waliopoteza mali. Pia amevitaka vyombo husika kuwafutia mashtaka ya uhaini vijana wote walioandamana kwa kufuata mkumbo. Mwisho katika hili ametaka iundwe tume yakuchunguza kiini cha vurugu hizo.
Rais ametoa mkazo wa pekee kuhusu mambo ya vijana, ikiwepo kuundwa kwa wizara ya vijana, kuwepo ofisi maalum itakayomshauri kuhusu vijana pamoja na kutenga fungu la mitaji kwa vijana.
Rais ameahidi kuhuisha mchakato wa maridhiano pamoja na katiba mpya mambo ambayo kwakweli ndiyo yaliyopigiwa kelele sana katika madai ya No reforms, No election.
Ingawa hutuba yake imesheheni mambo mengi mazuri ambayo serikali yake itajikita kuyatekeleza, mambo hayo niliyoyataja hapo juu, kwa maoni yangu ndiyo yaliyokuwa yakisubiriwa sana kuiponya nchi yetu kufuatia yaliyotokea October 29.
Watanzania tunakutakia kila la kheri Rais wetu katika dhamira yako njema ya kulitumikia Taifa letu.