HOTUBA YA RAIS OBAMA

innocent Kanyatta

New Member
Aug 12, 2015
3
0
Obama aliwaaga Wamarekani na dunia kwa ujumla kwa hotuba iliyojaa majonzi.Pengine mimi nabaki kujiuliza kwa nini Obama katumia mda wake mwingi ofisini kutekeleza yasiyo na manufaa kwa Wamarekani?
Kwa nini katumia pesa za walipa kodi kuendesha vita vilivyogharimu maisha ya watu wasio na hatia?
Je ilikuwa halali kwa Obama kuivamia Libya na kusababisha vifo vya watu wengi wasio na hatia na kumuua kiongozi wao Gaddafi aliesimamia raslimali za nchi yake kwa maslahi ya watu wake?
Msimamo wa Obama kuwakingia kifua waasi wa serikali halali ya Syria na kusababisha vita vilivyo ghalimu maisha ya watu wasio na hatia, tafrani na uhalifu wa kivita kuna tija gani kwa raia wa kawaida nchini kwake?
Maovu ya mshirika wake Saudi Arabia kwa vita vinavyoendelea nchini Yemeni vinavyogharimu maisha ya Wayemeni wengi wasio na hatia vina tija gani kwa wamarekani wa Kawaida?
Obama ameshindwa kuzuia mauaji ya watu weusi nchini.
Obama kashindwa kutatua tatizo la ajira na idadi ya Hillbillies inaongezeka kila leo.
Huduma za afya bado ni tatizo lakini pamoja na changamoto hiyo bado hajakoma kuipa pesa Israel.
Mpango Wa Obama wa bima ya afya hadi sasa haujaanza kutekelezwa hadi anaondoka.
Kuna tija gani hasa kutumia pesa za walipa kodi kwa ajili ya kulisha wanajeshi walioko kwenye base mbalimbali duniani huku maisha ya watu wako yakiendelea kuwa magumu?
Je Wamarekani ndio waliomtuma afanye hayo, kama si kwa manufaa ya Zionism na global Agenda?
Kama haitoshi kidonda ndugu cha Mashariki Ya Kati ndo hicho kinaendelea kutoa Usaha.
Dunia imeumizwa na sana na sera mbovu za mambo ya nje za marekani. Na matokeo yake ndio haya na yanaendelea.
Kwanza Hali ya Usalama ni mbaya duniani pote.Ughaidi na makundi ya watu wenye hasira wanaotekeleza mauaji kwa watu wasio na hatia, kwa kujitoa mhanga au kwa kutegesha milipuko, kugonga watu kwa magari mfano tukio la juzi Israel.
Tatito la wahamiaji linalotishia Uchumi na Usalama barani Ulaya ni matokeo ya vita na machafuko katika nchi za wakimbizi.
Umoja Wa Mataifa kutokuwa chombo chenye uwezo wa kutatua changamoto za wanachama wake na Baraza la Usalama kutokuwa na muafaka wa pamoja kutokana na Uhasama wa wajumbe.
Kuongezeka kwa Uhasama duniani mfano kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Marekani na China, Marekani na Urussi.Haya yoye ni matatizo ambayo Obama anayaacha mezani yakiwa hayana uvumbuzi.
Obama katumia mda wake vibaya, kaiumiza Dunia.
By
Innocent Yona Isaya
 
Obama ni mtu dhaifu anaewaza kinyume (anti clockwise) wewe mwandishi hujui lolote kuhusu uzayuni na ni bora ujifunze mengi kuhusu Israel usiyoyajua.Obama alitamani sana aifute hio misaada kwa namna alivyo kichwa mbovu lakini alishindwa hii ni kwa sababu Israel ni kubwa zaidi yake na pia wayahudi hawakurudi pale middle east by chance ila kuna sababu kubwa beyond our imagination..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom