naona leo anajifanya anajua sana mambo ya kilimo... kila kitu wahisani, wahisani watatupa watupaaaaa...bilioni bilioni kadhaaa.. nadhani anaonyesha umuhimu wa safari yake... anaelezea kuwa watu binafsi watapewa mashamba makubwa bila kupora maeneo ya wakulima wadogo... ahaaa daah huyu jamaa bora amalize tu aondoke, anaeleza sifa ya mkutano ulioisha jana arusha anadai ni maendeleo coz arusha watu walijaaa kila hoteli coz ya ule mkutano.... anaeleza hao wageni watatembelea hifadhi za wanyama. Jamaa ni kama anapiga stori kijiweni tu hana strategic yoyote.....anawasifu watu wa arusha kwa kuwapokea hao wageni katika mkutano wa arusha, kimtindo ni kama anaiponda chadema arusha, coz anasema kwa hari ilivyokuwa miaka miwili iliyopita arusha ilikuwa haijatulia.....so hata serikali isingekubali hao wageni wafikie arusha, anasema watu wa arusha waamue kutoka miyoni mwao kuasimamia utulivu ulipo now uendelee kuwepo, ni kama anasema labda lema asingevuliwa ubunge basi huo mkutano leo usingefanyika arusha, ni kama anafurahia kwa mambo ya kisiasa yalivyo now arusha... aneleza jinsi barabara zetu zinavyojengwa kwa wahisani wa kijapani na wamarekani kutoka tunduru mpaka mangaka... anaeleza kuwa kuna reli ya geji kubwa inataka kujengwa kutoka dar mpaka rwanda, anawasifu waitalia wanavyosaidia katika elimu, afya, na sayansi, jambo la tatu la tatu anazungumzia vurugu za zanzibar... anasema madhumuni ya uanzishwaji wa uamshu ulikuwa ni kwa madhumuni ya kidini,now wamecheng wanaelezea habari za muungano na chuki.. na matusi, anadai wanapandikiza chuki kwa wakristo, na wabara.. na makanisa kuchomwa, anadai vitendo hivyo ni uhalifu na ni vigumu kuvivumilia, anaungana na dr, shein kwa mambo yote atakayofanya, anasema ukristu haunguia kwa sababu ya muungano... dini ya kikristo ilienezwa bara kutokea zanzibar... makanisa ya agrikana na roman catholic yalikuwa ya kwanza kujengwa hata kabla ya mji wa zanzibar kukua