Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,960
- 11,222
1.Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2.Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3.Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4.Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5.Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6.Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7.Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8.Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9.Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10.Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11.Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12.Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.
Aliyekusanya vingi hakuzidi wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa.Sie twamwomba Rab atujalie paji la imani thabiti, tusadiki kwamba Rab anaweza yote na kwake hakuna lisilowezeka.Aliyezoea umbeya na unafiki utamfahamu tu endelea na udini wako .
Rais Dhaifu
Wewe nawe!!! nyie ndo tunasema wabinafsi sana tena sana, yaani unataka waongezewe mshahara madaktari tu, watumishi wauma wengine wasiongezewe??? fikiri kwanza ndugu.
kila taaluma inaumuhimu wake ndugu hata manesi pale muhimbili wanaumuhimu wao pia, hata makondakta wa daladala wanaumuhimu wao pia ambao wakigoma leo tutaadhirika tu, kinachotofautisha ni kiwango cha adhari.
tatizo la wabongo ni ubinafsi umetujaa tuuu, hatuna uzalendo na upendo, mtu amekaa nyumbani anataka aongezewe mshahara ile hali mwenzie anakufa?? what is this? ndo miiko ya udaktari au ...??
ndo mana wengine waliposoma PCB na nakupata divi 1 form 6 walitafakari kuona mazingira magumu hivyo wakaenda ualimu, uasibu au uanasheria, wakawapa nafasi wengine waliopata div 2 au 3 ili kuondoa usumbufu kama huo. sasa leo iweje ulieenda ulete bughudha kwa wengine?. Serikali lazima iwe na msimamo asiyeweza fanya kazi selikarini atoke halazimishwi??
Kweli huyu ni mheshimiwa dhaifu, Hotuba ya mwezi mzima suala ni moja tu, wakati yako mengi katika nchi yanahitaji kauli ya kiongozi wa nchi, kalikoroga la madaktari hana jinsi, Waziri wa afya, Waziri Mkuu na mwisho Rais mwenyewe hakuna alie na busara kutatua tatizo la madaktari.
Wewe ufanye tathmin, Akili za Makalio bwana
[/SIZE]
Mungu wangu hili taifa linaelekea wapi, mbona tumejaza binadamu wenye tamaa sana. Watu wote tunaowapa elimu huishia kujifikiria wao tu. Hivi tutaletewa kweli maendeleo kama wasomi wetu wakisha hitimu ni posho tu ndicho walicho kariri.
I had my reservations towards the doctors demands but after reading them no sane individual will side on them. Eti posho ya risk allowance hivi ni doctor au polisi wa leo anaenda kupambana na maandamano yasio isha yupi anafanya kazi kwenye mazingira ya hatari. Hawa watu ni very selfish na ni tamaa tu.
Sote atukubali malipo ya wabunge na marupurupu yao, na tukiseme tuwaendekeze na madokta nao walipwe vile hii nchi aitakuwa na bajeti ya kufanya kingine chochote. Wabunge wapo 350 roughly. Embu madokta wapo wangapi kwa mishahara yao wanayodai tupate estimate ya demands ya mishahara tu let alone hayo marupurupu wanayotaka its absurd.
By the way so far hii sector pekee kumbe inachukua almost 8% ya keki ya taifa, tukiongeza na hiyo mishahara na marupurupu kitaifa god knows how much of the cake itaishia kwao. Ni uwenda wazimu kuwatimizia mahitaji na ni upumbavu wa hali ya juu kuwa-support tamaa hawa kama wabunge waliokosa uzalendo. Tofauti ya mmbunge na dokta kwa utamaa ni mmoja ana saini anapitisha malipo yake mwenyewe lakini motive ya tamaa ni same.
Kweli huyu ni mheshimiwa dhaifu, Hotuba ya mwezi mzima suala ni moja tu, wakati yako mengi katika nchi yanahitaji kauli ya kiongozi wa nchi, kalikoroga la madaktari hana jinsi, Waziri wa afya, Waziri Mkuu na mwisho Rais mwenyewe hakuna alie na busara kutatua tatizo la madaktari.
Kikwete ni mwanadiplomasia, wanaoelewa lugha iliyotumika ambayo ni diplomatic language anaelewa kwamba rais katoa tamko rasmi la kuwafukuza madaktari waliogoma na kufukuzwa kwenye nyumba za serikali wanazoishi ndani ya saa 24. Kazi hiyo imezanza kwenye hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya dini Bugando Mwanza na KCMC Moshi.
Kwa mtazamo wangu serikali haiwezi kuacha mambo yaendelee kama yalivyo, ni lazima uamuzi ufanyike ili kieleweke tuna madaktari au la. Tuwajue madaktari waliopo kazini wanajituma na nani hawako pale kikazi ila kimasilahi.
Uwezo wa serikali umeishia hapo, asiyeweza na afungue virago aende huko anaokoona atapata mafao anayetegemea. Kulipwa milioni 7 kwa mwezi kwa hali ya serikali sasa hapana.
Haya ndiyo madai ya madaktari na kusababisha mgomo, kuna tofauti gani na malalamiko ya wananchi dhidi ya madai ya wabunge kuongezewa posho kiwango ambacho kinatofautiana mno na watumishi wangine wa umma? Kuwa na kiwango cha juu zaidi kutokana na taaluma yao sishangai, lakini kwa madai haya ni juu mno ukilinganisha na uwezo wa serikali.
mi mwenyewe nimechoka...yaani mwezi mzima mambo ni mawili tu hili la wasafiri haramu na hili la ulimboka...
kwa nini hazungumzii barua aliyoandikwa na marekani juu ya meli za irani kutumi bendera zetu?
Ndugu yangu, inaonekanai umejikita zaidi katika "miiko ya udaktari" kuliko hali halisi, kwa sababu tu madaktari eti wana miiko, miiko ambayo ndiyo hutumwa kuwanyongea kila wanapodai haki zao stahili kufuatana na umuhimu wao katika jamii.
"Miiko" my foot! Serikali inayo 'miiko" chungu nzima lakini haiifuati na wananchi wanakufa bila sababu kwa kutoizingatia!
Nampongeza kikwete amefanya uamuzi mgumu tuliotazamia, tunataka watu wenye kujali uhai wa binadamu kuliko wanaotanguliza masilahi yao kwa kuwekea rahani uhai wetu.
Mkuu tuachane na mishahara kuna la uboreshaji wa huduma kwenye vifaa mbona hajajibu na hilo ndo linatuhusu sana watz!Kazi ya muda mfupi ni tofauti na kazi ya masiaha inayochukua maelefu ya watumishi, jaribu kutofautisha kdigo utaona.
mbona serikali inajificha nyuma ya posho na mishahara, madaktari wanachodai ni zaidi ya mishahara, wekeni na hayo madai pia msituletee usanii na kutafuta public sympathy, unafikiri kwa nini viongozi wanatibiwa na kufanyiwa check up nje ya nchi?
Unda jeshi ufadhiliwe na mmerakni (liite lord resistance army) ili uwaondoe JK na wafanyabishara kutoka iran, oman, saudi maana una allergy nao..ok
mbona serikali inajificha nyuma ya posho na mishahara, madaktari wanachodai ni zaidi ya mishahara, wekeni na hayo madai pia msituletee usanii na kutafuta public sympathy, unafikiri kwa nini viongozi wanatibiwa na kufanyiwa check up nje ya nchi?