Hotuba ya Mwisho ya Muammar Gaddaffi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,550
Leo nimembuka hotuba iliyosononesha sana mwaka 2011. Hotuba ya aliyekua kiongozi wa Libya Kanali Mu'uammar Qaddafi. Aliiandika siku chache kabla ya kifo chake.

Hotuba hii nilipresent darasani enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa 2nd year na ikavuta hisia za wengi. Mwalimu wangu wa Media Ethics Denis Mpagaze alinitunuku zawadi ya vitabu 10 baada ya kuisikiliza.

QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
 
Mwaka 1979 huyo rafiki yako Muammar Qaddafi alipomsaidia Nduli Idd Amin askari pamoja na siraha za kivita kupiga Tanzania nina imani ulikuwa haujazaliwa.
 
Afrika ilipoteza Kiongozi. Kiongozi Shupavu. Viongozi wa namna hii hawatokei mara nyingi, ila wajapotokea, watapingwa ila watatimiza makusudio yao; watapingwa ila maneno na matendo / kazi zao zitabaki zikiwa hai na zikitoa sauti kuthibitisha Uongozi wao hata wajapokuwa hawaishi tena. Naitakia heri Afrika, iliyotarajiwa na Waasisi wake.
 
Denis mpagaze master of comm. Skills, alikufundsha saut mwanza au songea mkuu?
 
Mwaka 1979 huyo rafiki yako Muammar Qaddafi alipomsaidia Nduli Idd Amin askari pamoja na siraha za kivita kupiga Tanzania nina imani ulikuwa haujazaliwa.
wewe soma sababu za vita ya kagera ndio utajua na propaganda zenu.nahisi ulikuwa umezaliwa lkn akili
 
Ukweli lazima usemwe, pamoja na mapungufu take (kila binadamu anayo) Muammar Gaddaf alikuwa kiongozi wa aina yake si tu Africa bali duniani kwa ujumla. Kwa viongozi wetu wengi wa kiafrika Kama wangepata nafasi ya kuitawala Libya wangejilimbikizia mali nyingi mno na kujitajirisha, tofauti na Gaddaf aliwatajirisha wananchi wake na walineemeka mpaka wakajisahau na kuona neema waliyokuwa wakiipata ni ya kawaida, ona sasa wanavyoteseka na laana wanayoipata wanafia baharini kutaka kutafuta maisha nchi za ulaya.
Wengine hawampendi kwa sababu tu alimsaidia Nduli Amin kwenye vita Tanzania na Uganda, hicho sio kigezo cha kumfanya mtu kutokuwa kiongozi bora, kumbuka katika mgogoro wowote nchi inaingia kutokana na maslahi ya nchi husika Kama wafanyavyo wamarekani na nchi nyingine hasa za magharibi, walishindwa kuzuia mauaji ya kimbari Rwanda na kuamuru majeshi yao kuondoka na kuacha Wanyarwanda wakichinjana lakini waliingia Iraq, Libya na Syria kwa sasa kwa sababu ya maslahi yao. Hivyo all in all, Gadaff bado atabaki kuwa ni kiongozi wa kukumbukwa kwa mema makubwa aliyowafanyia wananchi wake kuliko kiongozi yeyote kwa sasa katika hii dunia.
Pasaka njema.
 
Jamaa ni mjinga sana, sheria ya vita ni ukizidiwa kimbia sio kufa kikondoo. Angeenda uhamishoni huenda Libya isingekuwa ilivyo sasa
Walibya walitaka wamekipata ili iwefundisho kwao na kwetu.
Watu mnasema marekani kunademocrasia nadhani uchaguzi uliopita mmeelewa kwamba marekani hakuna democrasia kama Tz
 
Acha hizo. Kwa hyo unamlaumu Gaddafi Kwa matatizo ya sasa ya Libya badala ya kuwalaumu hao mashetani walio vamia Libya?
 
Mwaka 1979 huyo rafiki yako Muammar Qaddafi alipomsaidia Nduli Idd Amin askari pamoja na siraha za kivita kupiga Tanzania nina imani ulikuwa haujazaliwa.
Zaidi ya hapo ni muhimu akajenga utamaduni wa kusoma historia na kupitia taarifa za vyanzo mbalimbali ili kupanua uelewa. Libya chini Muamar Gadafi ilitunza magaidi, wateka nyara.
 
Ukweli lazima usemwe, pamoja na mapungufu take (kila binadamu anayo) Muammar Gaddaf alikuwa kiongozi wa aina yake si tu Africa bali duniani kwa ujumla. Kwa viongozi wetu wengi wa kiafrika Kama wangepata nafasi ya kuitawala Libya wangejilimbikizia mali nyingi mno na kujitajirisha, tofauti na Gaddaf aliwatajirisha wananchi wake na walineemeka mpaka wakajisahau na kuona neema waliyokuwa wakiipata ni ya kawaida, ona sasa wanavyoteseka na laana wanayoipata wanafia baharini kutaka kutafuta maisha nchi za ulaya.
Wengine hawampendi kwa sababu tu alimsaidia Nduli Amin kwenye vita Tanzania na Uganda, hicho sio kigezo cha kumfanya mtu kutokuwa kiongozi bora, kumbuka katika mgogoro wowote nchi inaingia kutokana na maslahi ya nchi husika Kama wafanyavyo wamarekani na nchi nyingine hasa za magharibi, walishindwa kuzuia mauaji ya kimbari Rwanda na kuamuru majeshi yao kuondoka na kuacha Wanyarwanda wakichinjana lakini waliingia Iraq, Libya na Syria kwa sasa kwa sababu ya maslahi yao. Hivyo all in all, Gadaff bado atabaki kuwa ni kiongozi wa kukumbukwa kwa mema makubwa aliyowafanyia wananchi wake kuliko kiongozi yeyote kwa sasa katika hii dunia.
Pasaka njema.
Well said bro
 
Kiukweli kabisa duniani na hasa Afrika kupata viongozi wa kariba ya Gaddafi ni nadra sana. Wengi tulionao ni wenye tamaa ya kujilimbikizia mali na utajiri.
Libya enzi za Gaddafi imekuwa taifa la mfano kwa maisha bora kwa Afrika na dunia.

Licha ya kuwa mshirika wa Idd Amin Dada ktk vita ya Kagera lakini baadae alikuja kuwa mshirika wetu mzuri sana Tanzania kimaendeleo.

Leo hii wananchi wa Libya wanajuta kuingizwa mkenge na mataifa ya magharibi, maisha waliyodhani watayaishi imekuwa ndoto kwao na yenye shida kubwa ndani yake mpaka inafikiq hatua wanazamia nchi za magharibi kutafuta unafuu wa kimaisha.

Hili ni funzo kubwa sana katika nchi zetu.
 
Walibya walitaka wamekipata ili iwefundisho kwao na kwetu.
Watu mnasema marekani kunademocrasia nadhani uchaguzi uliopita mmeelewa kwamba marekani hakuna democrasia kama Tz
Ndugu unaonaje ukimaliza kwanza ya Muamar Gafafi wa Libya, halafu ndo uanze mada tofauti.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom