Hotuba ya Magufuli kwa Wafanyabiashara na Nchi ya matukio isiyokuwa na dira

puza46b

Member
Nov 3, 2010
91
261
Leo Magufuli katoa hotuba nzuri sana kupita nyingine zote zilizowahi kutolewa na raisi wa Tanzania kwa miaka 30 iliyopita. Ni kweli magufuli na serikali yake ya watu wawili wanahitaji maombi na msaada wetu katika kufanikisha hii sera ya hapa kazii tu. Ila inabidi tuwe makini haya matukio tunayoshangilia kila siku yasitufanye tupoteze dira ya nchi.

Kwa sasa gumzo la mitaani ni yaliyojiri bandari, stanbik, hoteli morogoro, kuchelewa kazini na kadhalika. Tusichozungumzia ni nini tunakipoteza tunapoendelea kujadiliana mambo ya matukio yanayopita. Kesho litakuja tukio jipya , na tutasahau yaliyotokea leo kama ambavyo IPTL na EPA zilivyogeuka kuwa hadithi.

Tutamsaidia magufuli kama tutalazimisha hoja na mijadala yetu iwe ikijaribu kutatua matatizo yajayo, kuweka misingi itakayowapa watoto wetu nguvu za kushindana kwenye soko la dunia na kutufungua kutoka kwenye minyororo ya madhulumu- ya kihistoria haswa ya kikoloni. Kwa sasa kama alivyosema Msigwa akili ndogo bado inatawala akili kubwa, yaani ushabiki wa kisiasa na story za vijiweni ndo zinaongoza dira ya nchi badala ya malengo ya mda mrefu. Sisi wanajamii tunachangia mapungufu hayo kwa kushangilia vitu vya ajabu visivyo na tija ya mda mrefu. Nakubali kwamba kila mtu ana mambo yaliyo muhimu kwake na huwezi mlazimisha afikirie tofauti.

Tujiulize, je Tanzania ina vijana wenye ujuzi wa kutosha kufanya kazi -pale uchumi wa gesi utakapoanza?

Je, tumejitayarisha kuhakikisha gesi inatengeneza uchumi mbadaala badala ya kuwa malighafi kuimarisha uchumi wa nchi nyingine? Au tutakuwa Nigeria inayohitaji kuagiza mafuta yaliyosafishwa?

Je tumejenga mihimili ya serikali imara inayofanya watu wawe na uchu mkubwa wa kuijenga taifa lao badala ya kuiuza kwa mataifa mengine? Mfano stanbink rushwa

Ni lini tutaacha kuwa watumwa wa nchi nyingine, hatujengi chochote hatuna utaalamu wowote na hatuna nguvu ya kusimama na kusema tunataka mkataba huu uwe hivi kulinda maslahi ya nchi.

Hakuna nchi iliyokuwa kiukweli kiuchumi kama uchumi wake wa ndani ya nchi haujaimarika. Jirani yetu Zambia wanalia kwa sababu uchumi wao umetikiswa na kupungua kwa bei ya coper kwenye soko la kimataifa. Je technolojia ikikua na kufanya gesi ishuke bei tutajilinda vipi? Au tutakubali yaliyotokea kwenye kilimo cha katani pale kamba na magunia ya niloni zilipoingia kwenye soko.

Ni kwa sababu ya mpungufu hayo machache, Stanbink benk inawaibia watanzania kisha inawalipa Uk $36 millioni na Tanzania inapata $7 millioni tu. Na tusisahau rada waliyolipwa $200 million na Tanzania $28m

Sitaki kuandika mengi, nachoomba tu.. tuendelee kuwapa pongezi Magufuli na Majaliwa kwa kazi nzuri wanayofanya ila tusijisahau na kuwa mashabiki wa matukio. Hoja ya msingi inayotakiwa kuwepo kwenye midomo yetu kila siku ni Tanzania gani tunataka kuwaachia watoto wetu. Tuchanganue kila kitu tulichonacho na ni jinsi gani kinaweza kuongeza tija kwa taifa. Na pale kwenye mapungufu tujiulize nini cha kufanya

Hotuba aliyotoa magufuli kwa wafanyabiashara ndo iwe gumzo la mitaani na siyo fulani anavunjiwa nyumba au kufukuzwa kazi kwa kuchelewa. Magufuli anajaribu kuweka dira ya nchi, tumsaidie kuhakikisha kila mtanzania anaimini na kuichangia.
Tusikubali hotuba ya Magufuli iwe tukio jingine, bali iwe dira ya taifa.

Mungu ibariki Tanzania,

Nawakilisha.
Nb..huu uzi ulihamishwa kwenye uzi wa matukio. Nimeiweka upya nione kama admini watachakachua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom