Hotuba ya Lowassa yavuja

Hotuba ya Lowassa yavuja

Sasa hapo kuna mabadiliko gani wakati amewahakikishia hao vibaka wenzake ajira?? Huyu jamaa ni janga la taifa aisee
 
Wandugu, nimepata kipande kikubwa cha hotuba ya Lowassa ya kufungia Kampeni, kuna mambo mapya meengi saana atayaongea, ambayo nina uhakika yatamuongezeau kura nyiiingi saaana zilizokua zimebaki CCM.

Kwa ufupi kati ya hayo mambo ni yafuatayo;

1. Kulipa madeni yote ya ndani, kuanzia kwa watu binafsi, makampuni ya ndani na watumishi wa umma, wanoidai serikali, wakiwemo na wafanyakazi wa iliyokua jumuiya ya Africa Mashariki, (wale wazee), pia kuna watu wanaidai serikali kutokana na kuishinda serikali kwenye kesi mahakamani lakini hawajalipwa na serikali haina mpango wa kuwalipa.

Hatua hiyo, licha ya kwamba itamuongezea kura, itasaidia saana kunyanyua uchumi wa watanzania wengi.

2. Lowassa, anaahidi kuwalipa fidia (kuwarudishia fedha zao) wale wote walioathirika na upatu wa DECI, walipanda lakini hawakuvuna. Ikumbukwe kwamba fedha zao zilikamatwa na serikali ikazichukua, viongozi wao wakafungwa lakini serikali haijawarudishia fedha waathirika na wala haijasema imeweka wapi zile fedha ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya Billioni 29.

3. Pia anawapa moyo na kuwaahidi watumishi wa umma, kwamba ajira zao katika utumishi wa Umma zitaendelea kuwa vile vile, mathalani kwa mfano wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu, wakurugenzi wa halimashauri, wakurugenzi wa idara mbali mbali. Vyeo vyao vitaendelea kuwa kama kawaida, kama kubadirishwa itakua ni sababu yabutendaji na sio uhusiano wao na vyama.

Na mengine mengi subirini wenyewe kuisikiliza hotuba.

Nahisi hotuba ya hitimisho itamuongezea kura nyiingi saana Lowassa.

Lowassa anataka kutapeli wapiga kura..
Sera za ukawa na chadema hazitambui wakuu wa mikoa na wilaya.Chadema walishaapa kuwa siku ya kubahatika kuingia ikulu ndio mwisho wa vyeo hivyo
Leo lowassa anataka kutuhakikishia uwepo wa vyeo hivyo?.Ukawa ni walaghai kupita maelezo
 
Wandugu, nimepata kipande kikubwa cha hotuba ya Lowassa ya kufungia Kampeni, kuna mambo mapya meengi saana atayaongea, ambayo nina uhakika yatamuongezeau kura nyiiingi saaana zilizokua zimebaki CCM.

Kwa ufupi kati ya hayo mambo ni yafuatayo;

1. Kulipa madeni yote ya ndani, kuanzia kwa watu binafsi, makampuni ya ndani na watumishi wa umma, wanoidai serikali, wakiwemo na wafanyakazi wa iliyokua jumuiya ya Africa Mashariki, (wale wazee), pia kuna watu wanaidai serikali kutokana na kuishinda serikali kwenye kesi mahakamani lakini hawajalipwa na serikali haina mpango wa kuwalipa.

Hatua hiyo, licha ya kwamba itamuongezea kura, itasaidia saana kunyanyua uchumi wa watanzania wengi.

2. Lowassa, anaahidi kuwalipa fidia (kuwarudishia fedha zao) wale wote walioathirika na upatu wa DECI, walipanda lakini hawakuvuna. Ikumbukwe kwamba fedha zao zilikamatwa na serikali ikazichukua, viongozi wao wakafungwa lakini serikali haijawarudishia fedha waathirika na wala haijasema imeweka wapi zile fedha ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya Billioni 29.

3. Pia anawapa moyo na kuwaahidi watumishi wa umma, kwamba ajira zao katika utumishi wa Umma zitaendelea kuwa vile vile, mathalani kwa mfano wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu, wakurugenzi wa halimashauri, wakurugenzi wa idara mbali mbali. Vyeo vyao vitaendelea kuwa kama kawaida, kama kubadirishwa itakua ni sababu yabutendaji na sio uhusiano wao na vyama.

Na mengine mengi subirini wenyewe kuisikiliza hotuba.

Nahisi hotuba ya hitimisho itamuongezea kura nyiingi saana Lowassa.

Na wengi wao; mfano watu wa DECI, wazee na watu wa vijijini, hadi wasikie hilo watakuwa wameshapiga kura....! Bora angeyaongea haya siku nyingi, maana sioni sababu kwa nini hakuongea wakati wowote huko nyuma...! Vinginevyo napata shaka juu ya ukweli wa dhamira hiyo...!
 
Atatoa wapi hela kulipa deni lote hilo
Atupe scheme nzima ya mapato na kiasi sio porojo porojo kwa wananchi.
Siku izi watu wanajielewa na huo ni uong dhahiri
 
Ukiwa na akili lazima ujiulize ndani ya huo muda mfupi atazipata wapi hizo pesa, bila kusahau na za elimu ya bure toka msingi mpaka chuo, au amesemaje kuhusu atakavyozipata maana kulipa madeni LAZIMA uwe na pesa, elimu ya bure lazima serikali iwe na pesa, mambo yote hayo kwa pesa ipi ndani ya huo muda?
Ukiwa mjinga lazima akuingize kingi.

CCM na ukawa kila moja katoa ahadi nyingi.
 
Sidhani kama ataweza kuisoma kwa urefu huu labda atuwekee kwenye website ya chama tuipitie kabisa

Ni recoded speech, wakumuonea huruma no mtaalam wa Ku edit. imemchukua zaidi ya wiki moja kuiunga unga ndiyo maana imevuja
 
Kwa aina ya mfumo wa maisha tulionao watanzania hakuna mwanasiasa atakaekubalika kama hasemi uongo ni kudanganywa tuu na ndicho tunachotaka kusikia eeeh mungu tunusuru
 
Nimecheka sana leo kusikia Magufuli anawambia watu wa Mlandizi wasiuze ardhi yao maana anampango wa kujenga viwanda kama Elfu moja eneo hilo ndani ya miaka miwili au mitatu. Nimejiuliza au huyu jamaa hata mashine za kusaga mahindi nazo anajua ni viwanda?

Nilishangaa sana pia kusikia viwanda 1,000 eneo moja, hata ukichanganya na mashine za kusaga unga wa mahindi na wa mifugo bado havifiki 1,000. Kweli pombe mbaya.
 
sasa hapo kuna nn kipya cha kumwongezea kura?
huwezi ukapata kura za watu kwa kuhalalisha upuuzi wa kuvunja sheria
nani asiyejua kuwa deci ilikuwa ni taasisi ya kihuni kabisa ambayo ilikuwa inakwepa kodi za wananchi kwa kunufaisha wachache?
nani asiyejua kuwa kitendo cha deci kuwepo kungeleta fujo hasa katika taasisi za kifedha kwa sababu ilikuwa haifuati utaratibu?
 
Siku za 67 za Kampeni za uchaguzi mkuu nchini zinafikia kikomo kesho jumamosi, 24 oktoba 2015. Kwa kipindi chote hicho mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Ngoyayi LOWASSA ameshindwa kabisa kukata kiu ya Watanzania ya nini hasa atawafanyia Watanzania, nini kauli yake kuhusu tuhuma dhidi yake kuwa NI FISADI na MWENYE MATATIZO YA KIAFY n.k, tuhuma ambazo kimsingi siyo nzuri kuwa nazo mtu anayetaka kuwa katika nafasi ya juu kabisa katika nchi kama urais. Mambo yamekuwa tofauti kabisa ndani ya siku za kampeni, mambo mengi yamezidi kutia shaka na wasiwasi kama Lowassa anaweza kuwa mtumishi mtiifu kwa Watanzania. Miongoni mwa mambo ambayo yamezidi kumuweka Lowassa katika wakati mgumu na pengine kufikia hatua ya kutaka siku za kampeni zimalizike mapema ili aondokane na ghadhabu hiyo ni pamoja na:
1. Kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano yake ya kampeni kama ilivyopangwa kwa madai ya mara majukwaa hayajaandaliwa vizuri, vipaza sauti havifanyikazi wakati viongozi wengine wanavitumia vizuri vipaza sauti hivyo na majukwaa husika.
2. Kuonekana mara akiingia katika majengo ya MALIWATO karibu na maeneo aliyoandaliwa kuhutubia, matukio yaliyotafisiriwa kuwa ni kutokana na afya yake kuwa na matatizo
3. Kushindwa kabisa kujibu maswali ya wanahabari hususani yale yaliyomtaka kutolea ufafanuzi namna atakavyofanyia kazi ahadi zake anazozipa vipaumbele mfano elimu pamoja na tuhuma za ufisadi ambazo anarushiwa tangu akiwa CCM na viongozi wa upinzania na CCM kipindi hiki ambacho amehamia Chadema, chama ambacho ndicho kiliongoza harakati za kuanika UFISADI wake.

4. VIFO TATA NA AJALI ambazo kwa namna moja au nyingine amekuwa akihusishwa kuhusika kuyapanga KIMKAKATI na hata KISHIRIKINA kwa vile wahanga wa matukio hayo walikuwa na wengine wameendelea kuwa mahasimu wake wakubwa. Baadhi ya watu wamekwenda mbali na hata kusema LOWASSA NI FREEMASON na kwamba PETE yake inayoonekana kila anapoonekana kwenye picha ni ya KI- FREEMASON. Baadhi ya vifo hivyo na ajali hizo ni pamoja na:
1. Kifo cha Mch. Christopher Mtikila
2. Kifo cha aliyekiwa Mbunge wa Ulanga, Celina Kombani
3. Ajali ya Helikopta, ambayo ilipelekea aliyekuwa MBUNGE wa Ludewa , Marehemu Deo Filikunjombe kupoteza maisha.
4. Ajali ya gari aliyoipata juzi Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM na mgombea Ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye.

NINI HASA ANACHOKUJA KUTUAMBIA KWENYE HOTUBA YAKE YA LEO USIKU SAA TATU KAMA BADO KUNA SINTOFAHAMU IMELIGUBIKA TAIFA KUHUSU HARAKATI ZAKE ZA KWENDA IKULU?
 
Kwa sababu wewe ni kiziwi, hujui kusoma sasa unafikiri utaelewa nini? Mungu akusamehe hujui ulisemalo.
 
Back
Top Bottom