Hotuba ya karne ya Humphrey Polepole iliyowainua watu Mlimani City 2014

Hotuba ya karne ya Humphrey Polepole iliyowainua watu Mlimani City 2014

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
29,869
Reaction score
34,027
Toka maktaba:

November 26, 2014​

Mlimani City, Dar es Salaam

Hotuba ya karne ya Humphrey Herson Polepole iliyowainua watu Mlimani city 2014​

Alichosema Polepole katika Mdahalo wa Katiba Mlimani - City 2014 kinachoishi jana, leo na hadi kesho

Amb. Humphrey H. Polepole

View: https://m.youtube.com/watch?v=tMtyZvDJWGI

Mjumbe wa Kamati ya Katiba Pendekezwa ndugu Humphrey H. Polepole ahoji mambo mengi mazito ktk ukumbi wa Mlimani City .. kuwa hii Katiba pendekezwa ya 2014 ni katiba ya Kimapinduzi iliyokusanya maoni ya wananchi na siyo maoni ya viongozi kama wabunge n.k

Katiba hii pendekezwa inatoa nafasi kuwawajibisha viongozi waliochaguliwa na wananchi bila kusubiri muda wao wa kukaa madarakani baada ya uchaguzi uishe, ni kwamba kama kiongozi haeleweki basi atafungashiwa virago mapema kabla ya miaka mitano kuisha..

Yule mwamba wa movie Arnold Alois Schwarzenegger gavana wa ... aliingia madarakani baada ya wananchi wa jimbo kuonesha kutokuwa na imani na mtangulizi wake ndipo akapata nafasi ya kuchaguliwa mwigizaji mwamba Arnold Alois Schwarzenegger .. nchi nyingi katiba zao zinaruhusu kiongozi kuondolewa madarakani kabla ya muhula wake kuishi Kenya, Peru, Ecuador, Uswiss kwa kutaja kwa uchache ...kiongozi huweza kuondolewa kikatiba anapofanya vitu visivyoeleweka kwa wapiga kura wake..

..
Humphrey Polepole, aliitaka serikali kusambaza Katiba inayopendekezwa pamoja na rasimu ya Tume hiyo kwa wananchi ili waisome na kuielewa kabla ya kuipigia kura ya maoni.

Kuhusiana na suala la elimu ya wabunge, alisisitiza kuwa ni vema wabunge wawe na elimu ya kidato cha nne, tofauti na katiba inayopendekezwa inayowataka wawe wanajua tu kusoma na kuandika.

Alisema endapo Katiba itapitishwa kama ilivyo kwamba wabunge wajue kusoma na kuandika pekee, itamuwia vigumu rais kupata mawaziri wenye elimu ya kutosha ya kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi.

“Unawezaje kusema wabunge wawe wanajua kusoma na kuandika tu, isipokuwa mawaziri, je, wakichaguliwa wabunge wote ambao uwezo wao ni wa kusoma na kuandika tu, hao mawaziri watatoka wapi na shughuli za maendeleo wataendeshaje?” alihoji Polepole.

Kadhalika, alisema kuwa anashangaa mawaziri kuipigia chapuo Katiba inayopendekezwa na kuipinga serikali tatu, wakati hata wao walitoa maoni wakiitaka muundo wa serikali hizo.

“Mimi nilishiriki katika kikao cha kukusanya maoni ya mawaziri, walipendekeza serikali tatu, na hata baadhi ya mawaziri wakuu nao walipendekeza serikali hizo, na wasitake tufikie huko wanakotaka, wakibisha tunaweza kuwataja,” alisema huku walioshiriki mdahalo huo wakitaka awataje. Na akaongeza hii katiba mpya ni kwa ajili ya wananchi kuweza kuwadhibiti viongozi lakini, nashangaa viongozi wanapinga haki hiyo ya msingi ya wananchi kuweza kuwadhibiti viongozi waliowachagua pale vigogo hao wanapokengeuka

Pia ukumbini waliokuwa wajumbe Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kuikosoa vikali Katiba inayopendekezwa na kusema kwamba haitakuwa na manufaa kwa Watanzania.

Kadhalika, wamesema Muungano uliopo kwa sasa upo katika hatari ya kuvunjika na kwamba hali hiyo itasababishwa na Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba (pichani chini), akizungumza katika mdahalo wa kujadili katiba inayopendekezwa uliofanyika ukumbi wa City jijini Dar es Salaam jana, alisema Katiba hiyo imeondoa matarajio ya wananchi waliotegemea kupata katiba ya kuwakomboa katika miaka mingine 50 ijayo.

Alisema Muungano umefika hapa ulipo, umetokana na kudra za Mwenyezi Mungu na hekima za viongozi waliopita kwa kuuendesha kwa hekima licha ya katiba hiyo kubeba changamoto lukuki.

“Mimi nimeshangaa kuona waheshimiwa hawa wananitukana na kunikashfu eti nimemsaliti Mwalimu Nyerere, wanadiriki kutumia nguvu na maneno ya kashfa kupitisha katiba. Katiba haiwezi kupitishwa kwa namna hiyo, katiba ni maridhiano ambayo pia yanashirikisha maoni ya wananchi,” alisema Warioba na kuongeza:“Hata kama Nyerere angelikuwapo leo angeipinga Katiba hii inayopendekezwa.”

Warioba alisema hata kama wataipitisha kwa nguvu, lakini wanatakiwa kufahamu kuwa italeta matatizo baadaye na ni vizuri wafahamu kuwa hata kama itapita itakuwa na matatizo

Hoja za Humphrey Polepole ni moja ya hotuba zilizowanyanyua kutoka vitini wananchi waliojazana ukumbi huku pia majumbani familia na marafiki wakikodolea skrini za televisheni zao kufuatilia hotuba motomoto kutoka ukumbi wa Mlimani City.
 
November 26, 2014​

Mlimani City, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam

Jaji Warioba akoleza moto Katiba Mpya

Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.
Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika mdahalo wa jana, ukumbi huo ulijaa na kupelekea polisi kuwazuia baadhi ya watu kuingia ndani kutokana na kukosekana na nafasi.

Hali hiyo ilisababisha askari polisi kupata changamoto ya kuwaelewesha wananchi hao ambao hawakutaka kukubali kubaki nje.
 
25 May 2025
Habana, Cuba

AMB. HUMPHREY H. POLEPOLE, AOKOKA

View: https://m.youtube.com/watch?v=K3a-YI6csHY
Katika Album yangu ya Yesu ni Rafiki ambayo nimeandika mashairi na nimeitengeneza kwa kushirikisha Akili Mnemba au Artificial Intelligence (AI).

Huu ni mwimbo wa tatu katika Album hii na ujumbe wake unahusu neema ambayo tumepewa wanadamu kupitia kwa Yesu Kristo.

Wimbo unazungunzia uhusiano wetu na Mungu wetu wa Mbinguni na namna Yesu ameturudishia uhusiano wetu na Baba yetu na kwamba ukimkiri Yesu utaokoka!Ni nyimbo kali sana, nimeweka gitaa moja amazing sana, nyimbo nzuri kusikiliza kwenye gari, nyumbani, ukiwa na ndugu jamaa na marafiki. Barikiwa sana na wimbo huu!

N.B Taarifa Hakuna Hakimiliki (No Copyright Statement)Hakimiliki (Copyright): Huru kwa matumizi ya Injili. Wimbo huu umetungwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu wetu katika Kristo Yesu.

Unaruhusiwa kutumika, kuimbwa, kurekodiwa, au kusambazwa bila malipo au ruhusa maalum. Lengo ni kumtangaza Yesu na kuleta wokovu kwa roho. Usiuze kwa faida binafsi — tumia kwa huduma.
Mtunzi: [Humphrey Hesron Polepole]Mwaka: 2025
 
Mimi nilishiriki katika kikao cha kukusanya maoni ya mawaziri, walipendekeza serikali tatu, na hata baadhi ya mawaziri wakuu nao walipendekeza serikali hizo, na wasitake tufikie huko wanakotaka, wakibisha tunaweza kuwataja,”
Hahaha
 
Magufuli alisema Katiba mpya ni ujinga,anachoangalia ni maendeleo.

Polepole nae akamuunga mkono...ila kuna watu wamesahau haya wanamuona ni shujaa, mkombozi mpenda mabadiliko...
 
Toka maktaba:

November 26, 2014​

Mlimani City, Dar es Salaam

Hotuba ya karne ya Humphrey Herson Polepole iliyowainua watu Mlimani city 2014​

Alichosema Polepole katika Mdahalo wa Katiba Mlimani - City 2014 kinachoishi jana, leo na hadi kesho

Amb. Humphrey H. Polepole

View: https://m.youtube.com/watch?v=tMtyZvDJWGI

Mjumbe wa Kamati ya Katiba Pendekezwa ndugu Humphrey H. Polepole ahoji mambo mengi mazito ktk ukumbi wa Mlimani City .. kuwa hii Katiba pendekezwa ya 2014 ni katiba ya Kimapinduzi iliyokusanya maoni ya wananchi na siyo maoni ya viongozi kama wabunge n.k

Katiba hii pendekezwa inatoa nafasi kuwawajibisha viongozi waliochaguliwa na wananchi bila kusubiri muda wao wa kukaa madarakani baada ya uchaguzi uishe, ni kwamba kama kiongozi haeleweki basi atafungashiwa virago mapema kabla ya miaka mitano kuisha..

Yule mwamba wa movie Arnold Alois Schwarzenegger gavana wa ... aliingia madarakani baada ya wananchi wa jimbo kuonesha kutokuwa na imani na mtangulizi wake ndipo akapata nafasi ya kuchaguliwa mwigizaji mwamba Arnold Alois Schwarzenegger .. nchi nyingi katiba zao zinaruhusu kiongozi kuondolewa madarakani kabla ya muhula wake kuishi Kenya, Peru, Ecuador, Uswiss kwa kutaja kwa uchache ...kiongozi huweza kuondolewa kikatiba anapofanya vitu visivyoeleweka kwa wapiga kura wake..

..
Humphrey Polepole, aliitaka serikali kusambaza Katiba inayopendekezwa pamoja na rasimu ya Tume hiyo kwa wananchi ili waisome na kuielewa kabla ya kuipigia kura ya maoni.

Kuhusiana na suala la elimu ya wabunge, alisisitiza kuwa ni vema wabunge wawe na elimu ya kidato cha nne, tofauti na katiba inayopendekezwa inayowataka wawe wanajua tu kusoma na kuandika.

Alisema endapo Katiba itapitishwa kama ilivyo kwamba wabunge wajue kusoma na kuandika pekee, itamuwia vigumu rais kupata mawaziri wenye elimu ya kutosha ya kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi.

“Unawezaje kusema wabunge wawe wanajua kusoma na kuandika tu, isipokuwa mawaziri, je, wakichaguliwa wabunge wote ambao uwezo wao ni wa kusoma na kuandika tu, hao mawaziri watatoka wapi na shughuli za maendeleo wataendeshaje?” alihoji Polepole.

Kadhalika, alisema kuwa anashangaa mawaziri kuipigia chapuo Katiba inayopendekezwa na kuipinga serikali tatu, wakati hata wao walitoa maoni wakiitaka muundo wa serikali hizo.

“Mimi nilishiriki katika kikao cha kukusanya maoni ya mawaziri, walipendekeza serikali tatu, na hata baadhi ya mawaziri wakuu nao walipendekeza serikali hizo, na wasitake tufikie huko wanakotaka, wakibisha tunaweza kuwataja,” alisema huku walioshiriki mdahalo huo wakitaka awataje. Na akaongeza hii katiba mpya ni kwa ajili ya wananchi kuweza kuwadhibiti viongozi lakini, nashangaa viongozi wanapinga haki hiyo ya msingi ya wananchi kuweza kuwadhibiti viongozi waliowachagua pale vigogo hao wanapokengeuka

Pia ukumbini waliokuwa wajumbe Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kuikosoa vikali Katiba inayopendekezwa na kusema kwamba haitakuwa na manufaa kwa Watanzania.

Kadhalika, wamesema Muungano uliopo kwa sasa upo katika hatari ya kuvunjika na kwamba hali hiyo itasababishwa na Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba (pichani chini), akizungumza katika mdahalo wa kujadili katiba inayopendekezwa uliofanyika ukumbi wa City jijini Dar es Salaam jana, alisema Katiba hiyo imeondoa matarajio ya wananchi waliotegemea kupata katiba ya kuwakomboa katika miaka mingine 50 ijayo.

Alisema Muungano umefika hapa ulipo, umetokana na kudra za Mwenyezi Mungu na hekima za viongozi waliopita kwa kuuendesha kwa hekima licha ya katiba hiyo kubeba changamoto lukuki.

“Mimi nimeshangaa kuona waheshimiwa hawa wananitukana na kunikashfu eti nimemsaliti Mwalimu Nyerere, wanadiriki kutumia nguvu na maneno ya kashfa kupitisha katiba. Katiba haiwezi kupitishwa kwa namna hiyo, katiba ni maridhiano ambayo pia yanashirikisha maoni ya wananchi,” alisema Warioba na kuongeza:“Hata kama Nyerere angelikuwapo leo angeipinga Katiba hii inayopendekezwa.”

Warioba alisema hata kama wataipitisha kwa nguvu, lakini wanatakiwa kufahamu kuwa italeta matatizo baadaye na ni vizuri wafahamu kuwa hata kama itapita itakuwa na matatizo

Hoja za Humphrey Polepole ni moja ya hotuba zilizowanyanyua kutoka vitini wananchi waliojazana ukumbi huku pia majumbani familia na marafiki wakikodolea skrini za televisheni zao kufuatilia hotuba motomoto kutoka ukumbi wa Mlimani City.

Nimeitafuta sana hii hotuba, asante sana
 
Chama dola kongwe toka 2015 kimekosa wanasiasa wenye uelewa mpana.

Viongozi wa awamu ya tano na awamu ya sita hawana uwezo wa kutoa mhadhara tunduizi katika chuo kikuu chochote cha ndani ya nchi na nje ya nchi.

Ndiyo maana ndugu Humphrey Herson Polepole aliamua kuwa mpole wakati wa utawala wa awamu ya tano. Lakini anaona hali inazidi kudidimia awamu hii ya sita ya utawala na kuona atoke mbele kuonesha kutoridhishwa na uwezo wa kiuongozi ngazi ya juu toka 2015 hadi sasa ndani ya CCM.

Tukiangalia profile za Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Cleopa Msuya, John Malecela, Salim Ahmed Salim, Mizengo Peter Kayanda Pinda, Edward Sokoine ni ngumu sana kufananisha na za John Pombe Magufuli, Kassim Majaliwa Majaliwa, Samia Suluhu Hassan

Wale wa 2015 kurudi enzi za Julius Nyerere wanaonesha CV na exposure kubwa ya kisiasa ya ndani na nje kikanda

Sasa turejelee umuhimu wa kuwa na great thinkers wa awamu ya kwanza hadi awamu ya nne alipoishia Jakaya Kikwete.

Kauli mbiu za Hapa Kazi awamu ya 5 , Utu na Kazi Tunasonga Mbele awamu ya sita. Kauli mbiu hizo ni nyepesi zisizo na visheni yoyote kuonesha kundi hilo la viongozi ni wenye uwezo wa kufikiri kwa kina /critical thinkers kuhusu uongozi na taifa.

1752455177151.jpeg
 
1 June 2025
Habana, Cuba

Sehemu ya hotuba yangu katika kuahirisha Kongamano la Kimataifa la Masomo ya Utamaduni, Lugha, Sanaa na Fasihi katika Chuo Kikuu cha Havana, ujumbe wangu Mkuu kwa Nchi za Ukanda huu ni kutizama Mashariki, Kutizama Afrika. Ndg. Balozi Polepole - Balozi na Mkuu wa Kituo Havana

View: https://m.youtube.com/watch?v=vp6hgD8tiTw
En la Conferencia Internacional de Estudios Culturales, Lingüísticos, Artísticos y Literarios de la Universidad de La Habana, mi principal mensaje a los países de esta región es que miren hacia Oriente, que miren hacia África. Embajador Polepole.
 
Ipo haja ya chama kongwe kujiangalia upya kaliba ya viongozi wanaotakiwa kupewa dhamana ya kiuongozi kwa niaba ya umma mpana.

Ndugu Humphrey Polepole tangu mwaka 2014 akiwa mjumbe wa Katiba Pendekezwa alihoji kigezo cha KKK Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kama kweli kinafaa kwa wanasiasa watakao kuwa wabunge na baadaye hata mawaziri watarajiwa au waziri mkuu na rais wa Tanzania

Tunaona jinsi nchi ilivyoyumba sana toka 2015 hadi sasa 2025 na hatari kwenda mbele hadi 2050 na zaidi
 
NCHI YA SINGAPORE : UONGOZI BORA WA WASOMI NA MAENDELEO YA TAIFA

In 1970s Singapore, a focus on meritocracy and elite education was intertwined with the nation's rapid economic development. This period saw the rise of an elite group, particularly in politics and the civil service, who were seen as essential for guiding the nation's progress. However, this focus on elite leadership and education also sparked debates about social stratification and the potential for inequality.

Here's a more detailed look:
Elitism and Development:
  • Rapid Economic Growth:
    The 1970s were a period of significant economic growth for Singapore, with real GDP averaging 9.2% yearly between 1970 and 1980, according to SG101. This growth was fueled by a strong manufacturing base and an increasingly educated workforce.

  • Elite Recruitment:
    The ruling People's Action Party (PAP) actively recruited talented individuals into the government and civil service, creating a technocratic elite focused on economic development.

  • Meritocratic System:
    A meritocratic system, emphasizing academic achievement and performance, was promoted to identify and cultivate this elite.

  • Education Policy:
    The introduction of streaming in the late 1970s, along with bilingualism and an emphasis on elite education, aimed to channel students into different educational pathways based on their perceived abilities.

  • Focus on Efficiency and Pragmatism:
    The government prioritized efficiency, pragmatism, and a business-friendly environment to attract foreign investment and drive economic growth.
Emerging Tensions:
  • Social Stratification:
    The emphasis on elite education and meritocracy led to concerns about social stratification and the potential for a widening gap between the elite and the rest of the population.

  • Exclusion and Inequality:
    Some scholars argued that the system could lead to the exclusion of those who did not fit into the elite mold and exacerbate existing inequalities.

  • Impact on Social Cohesion:
    Critics also raised concerns about the potential impact of this elite-focused development model on social cohesion and the sense of national identity.

  • Contradictions in Ideology:
    There were also tensions between the ideology of meritocracy and the reality of social inequalities and the concentration of power within a small group.

  • Nation-Building Project:
    The government's nation-building project, while successful in many ways, was seen by some as relying heavily on the idea of an elite group leading the nation, potentially creating a fragile system.
In summary: The 1970s in Singapore saw a strong link between economic development and the emergence of a meritocratic, elite-focused system. While this approach contributed to rapid economic growth, it also sparked debates about social stratification, inequality, and the potential for social divisions.
 
Ipo haja ya chama kongwe kujiangalia upya kaliba ya viongozi wanaotakiwa kupewa dhamana ya kiuingozi kwa niaba ya umma mpana.

Ndugu Humphrey Polepole tangu mwaka 2014 akiwa mjumbe wa Katiba Pendekezwa alihoji kigezo cha KKK Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kama kweli kinafaa kwa wanasiasa watakao kuwa wabunge na baadaye hata mawaziri watarajiwa au waziri mkuu na rais wa Tanzania

Tunaona jinsi nchi ilivyoyumba sana toka 2015 hadi sasa 2025 na hatari kwenda mbele hadi 2050 na zaidi
Pumbavu huyo jamaa 2015-2020
Si alikuwa chawa wa jiwe mbona hakuona ubovu wa uongoz wake

Shenzi kabsaa hatuwez kuwapa nchi wahuni tenaaa
 
Back
Top Bottom