Hotuba ya JK yapondwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,782
*Wadai ni sawa na kuwatishia nyau
*Wengine wadai Rais ameteleza
*TUCTA wadai amewapaisha juu
*Wapinzani waiponda, wamtaka atangaze mishahara yao
*Wadai hakuna wasomi wengine wa kuziba mapengo



BAADHI ya wananchi wameibuka na kuiponda hotuba iliyotolewa jana na Rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ni sawa na kumtishia mtu mzima nyau na kwamba imejaa ubabe na udikteta.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nayakati tofauti, wakazi hao ambao wengi wametuma ujumbe kupitia barua pepe na wengine kupiga simu, wamedai kuwa wamesikitishwa na kauli ya Rais Kikwete kwa kuwa imeweka utu nyuma na kutanguliza ubabe mbele.

Wamesema Rais Kikwete anapaswa kuelewa kuwa wananchi aliokuwa akiwahutubia na waliofuatilia hotuba zake wana akili zao timamu na wametofautiana uwezo wa kufikiri.

“hatukutarajia kama Rais angeweza kuongea maneno makali kiasi kile. Sisi tunachoona labda rafiki zake ni mafisadi sisi wadai haki ndiyo adui zake wakubwa. Hataki kutusikia,” amesema.

Wameongeza kuwa yeye kama baba alitakiwa kutafakari na familia yake ni jinsi gani ya kupunguza ukali wa maisha kwa watoto wake lakini kinyume chake amezidi kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda, jambo ambalo linaonesha wazi kuwa si mtu mwenye kuwajali wananchi wake.

Wamesema watalishangaa Jeshi la Polisi kama litasonga mbele kuwanasa wanaogomea mishahara kwa kuwa nao ndio kilio chao kikubwa.

“Hivi unamwambia Polisi eti kawakamate wale wafanyakazi wa mashirika mbalimbali wamegomea mishahara midogo wakati yeye ndiye kwanza ana mshahara mdogo na kilio chake kikubwa ni ugumu wa maisha?” amehoji mkazi mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, amempongeza Rais Kikwete kwa kuonyesha makucha yake.

“Kwa wale waliokuwa wakimtafakari kama ni mpole sasa wameona ukali wake,” amesema Mrema.

Amesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) limeonekana si chama kizuri kwa wafanyakazi kwa kuwa kimekataa kurudi kwenye mazungumzo hali ambayo inaonesha ubabe na kwamba kimeonekana kuwa cha kisiasa zaidi.

“Ninawashauri TUCTA waingie katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu na wanachama wake wawapigie kura na wakishinda watangaze kima cha chini ni sh. milioni 2 kwa sababu watakuwa wameziba mianya yote ya rushwa kama kweli wataweza,” amesema Mrema.

Hata hivyo, mkazi mmoja wa jijini ambaye hakutaka kutaja jina lake, amesema wazee wanaodaiwa kuwa ni wa Mkoa wa Dar es Salaam si wafanyakazi na wengi wao wanategemea kuhudumiwa na watoto wao ambao ndio wenye kilio cha mishahara kiduchu.

“Sisi hatuelewi kama wale ni wazee wa mkoa huu au la. Mbona walivaa nguo za Chama cha Mapionduzi (CCM)?” amehoji mkazi huyo.

Wakati huo huo, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa, hakuna mwenye maumivu makali ya mshahara kama polisi, labda Rais hajui hayo.

Amesema JK hakufanya busara kuzungumza na wazee wale kwa kuwa sio walengwa wakuu wa mishahara iliyokuwa ikizungumziwa.

Ameongeza kuwa ni vyema amewaita watu wasiohusika kwa sababu hawajui kinachoendelea na kwamba angekuwa mkweli angewaambia mshahara wake ni shilingi ngapo, mishahara ya wabunge, mawaziri na wengineo.

“Tunachoomba Rais Kikwete atangaze hadharani mishahara ya viongozi wa juu. Pia aelewe kuwa wanaolalamikia uduchu wa mishahara hawana mashamba, biashara wala si wafugaji,” amesema Slaa.

Slaa amesema endapo kundi la wafanyakazi lisiposikilizwa linaweza likafa njaa na kushindwa kusomesha watoto kutokana na ufinyu wa mishahara.

Amesema kitendo cha Rais kutishia kuwa atawafuta kazi wanaogoma ni danganya toto kwa kuwa nchi hii hakuna wasomi wa kuziba mapengo kutokana na uwezo wa viwango vya elimu vinavyotolewa nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholous Mgaya, amesema hotuba ya JK imewajengea jina na kuonekana kuwa ni watu wanaoona mbali.

Amesema hata hivyo TUCTA imeazimia kutoa tamko zito kuhusu hotuba hiyo haraka iwezekanavyo.

Amesema aliyemshauri Rais Kikwete ili atoe hotuba hiyo amempotosha kwani ina mapungufu mengi na iliyojaa chuki.
 
Waalimu chonde chonde, tusirudie makosa ya kumpa HAYAWANI kura zetu.
Shime tuungane kuondoa utawala wa kidhalimu ili kuboresha hali zetu za kiuchumi na kuboresha mazingira yetu ya kufanyia.
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.
 
HOTUBA ZOTE ZA HUYU MUHESHIMIWA NI AIBU TUPU.
SIJAWAHI KUIONA HOTUBA YAKE YA MAANA.
KIDOGO ALIJITAHIDI KWENYE HOTUBA YAKE YA KWANZA ALIPOHUTUBIA BUNGE, LAKINI NYINGINE ZOTE NI :blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah:
 
Back
Top Bottom