Hotuba ya JK leo vipi?

Hotuba ya JK leo vipi?

......Mh!!!

....siku hizi kufura fura tuuuu....

...ntakuletea ukwaju na malimao!!!!

Mkuu nahisi huyu Simiyu yetu ni mja mzito....! Yeye kuwaka waka tu bila mpango.!
 
JK anategea tulale ndio ahutubie,Tumeshtuka....
 
siwezi kuwa mnafiki...mara nyingi nikiona hotuba za JK huwa nabadilisha channel.....kama kuna pointi kaongea nitaikuta humu Jf japokuwa mara nyingi hakuna masuala la maana sana anayoyazungumzia kwenye hotuba zake(copy-paste toka BWM) za mwisho wa mwezi
 
hivi unafikiri JK kuongea kwake ni tabu? subiri tu uone atakavyoporomoka na hoja za msingi

...aah acha kumtania bosi wako,umekua wewe,hotuba za kuandaa kwa vikao sizifagilii hata siku moja na ndo maana zinamakosa sana ya takwimu. Vichwa vichache vinavyoweza kushuka nondo na hotuba ikakamilika, mmoja wao ni dr. Slaa...
 
Wadau;

Tuliwekewa bandiko hapa kuhusu hotuba ya Mh.Rais Jakaya Kikwete itakuwa leo tarehe 03/10/2013,kutoka kwa Salva Rweyemamu baada ya kuahirishwa juzi,Tumesubiri muda mrefu mpaka tunaenda kulala hakuna cha JK wala R.Rweyemamu waliojitokeza hadharani,

Watanzania Tunaomba kama mlivyotutangazia kuwepo kwake,tutangazieni pia kutokuwepo kwake, Nahisi Mh.Rais atakuwa amepewa maelezo tofauti ya ratiba naye anajua ni mwezi ujao,

Nini kimetokea Hotuba ya Rais kuota Mbawa? Majibu tafadhali....!!
 
Lukuvi aliingia mitini siku chache zilizopita. Leo J.K nae. Nani kabaki wa kumwamini serikalini?
 
kuna uzi ulipita hapa jana
kueleza kuwa jk leo atalihutubia taifa kwa mwenye kujua kinachoendelea
atujuze
nini kimetokea hadi rais atoe hotuba mbona sielewi.
 
kunajamaa kanichekesha eti kamnunia jk kwa nini hajatoa hotuba.
 
JK alijua leo mdahalo nini?

Kuna tetesi kuwa aliugua ghafla ule ugonjwa wake wakati anajiandaa kuhutubia. Source: mfanyakazi wa ikulu kitengo cha mawasiliano. Nasikia kunaweza kuwa na taarifa mbaya! Tujiandae kisaiklojia.
 
...aah acha kumtania bosi wako,umekua wewe,hotuba za kuandaa kwa vikao sizifagilii hata siku moja na ndo maana zinamakosa sana ya takwimu. Vichwa vichache vinavyoweza kushuka nondo na hotuba ikakamilika, mmoja wao ni dr. Slaa...

naona umempigia chapuo dr..wee nawe mchama chama kumbe
 
Watanzania kudanganywa ni mkate wa kila siku...hawa jamaa hata aibu hawana tena!
 
Labda alipanga kutoa hotuba ya kujiuzulu kwani lawama zimezidi ila naona kashauriwa avumilie tu!
 
Back
Top Bottom