Hotuba ya Dr. Slaa Bungeni Juni 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Dr. Slaa Bungeni Juni 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 20, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Date: 6/20/2009
  Spika aweka kiporo kombora la Dk Slaa

  AITAKA SERIKALI ITOE MAELEZO IFIKAPO JUMATATU

  Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma
  Mwananchi

  ALIANZA na mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na jana Spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta aliahirisha majibu ya swali la Dk Willbrod Slaa aliyehoji sababu za kutokaguliwa kwa makampuni ya Buhemba Gold Mine (Meremeta) na Tangold.

  Selelii alihoji kama serikali imeshaanza kutumia fedha za bajeti ya mwaka 2009/10 kwa kutekeleza mradi wa upanuzi na ukarabati wa barabara ya Chalinze-Segera kabla ya kupitishwa wakati alipoomba mwongozo, na Sitta alijibu kwa kuitaka serikali impe maelezo, lakini hadi leo majibu hayo hayajatangazwa.


  Jana Sitta aliahirisha majibu ya swali la Dk Slaa, ambaye ni mbunge wa Karatu aliyerejesha Bungeni suala tata la kampuni hizo mbili wakati alipouliza sababu za kutokaguliwa kwa Meremeta na Tangold.

  Katika swali hilo namba 76, Dk Slaa alisema kuwa hotuba ya waziri mkuu kivuli kwa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), aliyoitoa bungeni Juni, 2007 ilieleza juu ya ubadhirifu mkubwa uliofanywa na makampuni ya Meremeta na Tangold.


  Dk Slaa pia alisema kwamba ubadhirifu huo ulibainika kwenye makampuni ya Mwananchi na Deep Green Finance Co., na kwamba kiasi kinachodaiwa kufanyiwa ufisadi ni zaidi ya Sh215 bilioni.

  Na baadaye alihoji: "Ni lini kampuni hizo zitafanyiwa ukaguzi wa kina kama ilivyofanyika kwenye akaunti ya EPA ili kubaini ubadhirifu huo uliohusisha uhamisho wa fedha kutoka Benki Kuu (BoT) na vyombo vya umma kupitia NBC Corporate Branch DSM na Ned Bank ya Afrika Kusini."

  Dk Slaa aliuliza ni sababu gani za msingi zilizofanya kuchukua muda mrefu kuanza ukaguzi wa kina hata pale tuhuma hizo zilizopigiwa kelele na jamii na hata kamati mbalimbali zilizoundwa kuchunguza tuhuma hizo.

  Baada ya kuuliza swali hilo la msingi, Spika Sitta alitoa maelezo badala ya kumruhusu Waziri wa Fedha na Uchumi kulijibu.

  "Hili swali lililoulizwa na Dk Slaa ni zito, inabidi serikali ipate muda wa kuandaa majibu ya kutosha, kwa hiyo naliahirisha hadi Jumatatu liweze kujibiwa," alisema.

  Hatua hiyo ya Spika Sitta ni mwendelezo wa danadana za kutoa maelezo kuhusu kampuni hizo mbili Tangold na Meremeta, ambayo inahusishwa na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ).

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliapa kutotoa maelezo kuhusu suala hilo la Meremeta hata kama akisulubiwa.

  Tayari pia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka huu imeshindwa kukagua Meremeta na Tangold.


  Utata mkubwa uliopo Meremeta ambayo inamiliki mgodi wa dhahabu Buhemba, pamoja na tuhuma za ufisadi ni utata wa wanahisa.

  Kamati ya rais ya kuishauri serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini ilitilia shaka malipo kwa kampuni hiyo na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya uanzishwaji wa Tangold na umiliki wake katika kampuni hizo.

  Pia serikali ilitakiwa ichunguze uhalali wa malipo ya dola 132 milioni za Marekani yaliyofanywa na Benki Kuu (BoT) kwa benki ya Nedbank ya Afrika Kusini.


  Kamati hiyo pia ilipendekeza serikali ichukue jukumu la kuhakikisha mgodi wa Buhemba unafungwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazohusu ufungaji wa shughuli za migodi na kuhakikisha kuwa taratibu za kurejesha mazingira katika mgodi huo zinafanyika.

  Kamati hiyo iliundwa na Rais Jakaya Kikwete, Novemba 12, mwaka jana na kuipa muda wa miezi mitatu kukamilisha kazi yake.

  Ilikuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani ambaye ni Mwanasheria Mkuu mstaafu na Wakili wa Kujitegemea na ilikuwa na wajumbe wengine 11, wakiwamo wabunge wanne.


  Hotuba yenyewe hii hapa:

  (download attachment)
   

  Attached Files:

 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Danadana zitaendelea tu maana hawataweza kamwe kuifanyia ukaguzi maana vigogo wote wamo hata wastaafu wengi tu wamo......ngoja j3 utasikia ma story mapya....watasema wamepeleka kwa JK.
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SLAA KAMATA CCM; USIWAPE NAFASI; WAMEIBA NA SASA NI MUDA WA KUUMBUKA ( Baada ya swali tunakusubiria Biharamulo mkuu)
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  tatizo ni sisi wananchi ndio tunawanyima support hawa majamaa, na kama raia tungekuwa tunaonyesha uchungu wetu kwa vitendo nadhani hii nchi ingekunyooka
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani maswali yanayoulizwa na wabunge si yanapelekwa serikali na kuka huko hata miezi mitatu yakitafutiwa majibu!!!!????!!! Sasa ilikuwa hili lisitafutiwe majibu ya kina mpaka uhitajike muda wa ziada? Au ndio mkakati wa kufunika kombe utakuwa unafanyika katika kipindi hicho cha muda wa ziada??
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Hivi wabunge wengine wanafanya nini huko bungeni? mbona mpiganaji dhidi ya Deep green na Tan gold ni Dr. Slaa peke yake miaka yote? Hongera kamanda, endelea tupo nyuma yako, 2010 gombea tukupe nchi.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wananchi tuamke, amkeni jamani sio mnafurahia tu Ze Utamu kutiwa nguvuni wkt kuna watu wanasababisha wananchi vijijini wana kosa dawa, wanakosa maji, wanakosa haki zao za msingi kwa ajili ya watu wachache wenye matumbo makubwa walio kula pesa za Tangold,Deep Green na Mwananchi mining Heko Dr.Slaa waache Mungu atawahukumu tu hawa wanao dhoofisha mapambano.
   
 8. t

  tddd24lab New Member

  #8
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 21, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabunge wa ccm wanafiki walikuwa wanaibana bajeti lakini sasa hivi wote wameitikia kuipitisha na wengine walikuwa absent ili wasikumbane na mziki mnene
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hongera Slaa kwa ushujaa wako endelea hivyohivyo tunakuunga mkono.
   
 10. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,585
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wabunge wengine wako Bungeni kwa ajili ya posho tu na sio kwa maslai ya majimbo yao na nchi kwa ujumla.
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mfano mzuri Dewji. sijawahi kumwona akichangia hoja wala kuuliza swali la msingi kwa kipindi chote alichokuwa bungeni. kama kuna mtu alimwona na aseme lini au katika hoja gani.
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jamani ndo nafungua tbc1 nakutana na slaa na hotuba yake ya tamisemi. KILA MARA ANAKATISJHWA. ANACHAMBUA KIFUNGU MPAKA KIFUNGU ANATETEA WALE HAWALALA HOI
   
 13. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kuna maneno mengi ya kiswahili kipya lakini namuelewa. anasema kasma kwa kasma pesa ni kidogio lakini ukimjulisha pesa ni nyingo]i kwa ujumla. mfano je friji, furniture ni kila mwaka?
   
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kuna maneno ambayo ameambiwa na spika asiyaseme. na kweli karuka ili kuondoa rabsha na spika.

  kuna m2 kaomba mwangozo, ni dialo
   
 15. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anasema kuhusu slaa kurudia kuhusu suala kuwa katika kamati. sitta kasema sawa. nahisi alifikiri atazuiliwa maana marmo alisema kuwa huu sasa ni uwanja wa siasa lakini sitta akasema anachambua na kutofautisha
   
 16. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anazungumzia rushwa.... anataka taratibu za ishus ambazo hazipo mahakamani. sijui ni zipi maana anaruka sana pages
   
 17. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anapongexza vyombo vya habari pamoja na JF nafikiri.
   
 18. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anaulizia mkakati kuondoa umaskini. anaulizia data ambazo ni za tofauti katika report za serikali. anauliza kwa siku 640/= unamtosha nini mtu hapa dar?
   
 19. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  anachambua maisha at ground based ,on fact za umaskini kupungua kwa umaskini kama riport za serikali
   
 20. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kimsingi mambo mengi hazungumzi maana pages nyingi anaruka eti spika kamwambia, ila anataka deep green tangdold nae waziri mkuu awe mkali kama deci.
   
Loading...