Hoteli ya wanyama yafunguliwa Singapore

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,887
155,870
Mshirikishe mwenzako
141105085220_pet_hotel_640x360_bbc.jpg

Wanyama wakiwa ndani ya kidimbwi cha kuogea katika hoteli ya wanayama iliofunguliwa nchini Singapore


Hoteli moja ya kifahari ya wanyama wa kufugwa nyumbani imefunguliwa nchini Singapore.

Hoteli hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama hao,vyumba vyenye hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi kuimarisha viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa.

Hoteli hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa katika makaazi ya wanadiplomasia.

Vyumba vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.

Hoteli hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.

''iwapo tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli hiyo Estelle Taylor.

''Kama watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na eneo ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani'' aliongezea.

Wanaomiliki wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa, kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.

Hoteli hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo hadi makaazi yao.

Nchini Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka makubwa ya jumla.

Mfanyibiashara mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.

 
Tz wanahangaika kufisadi nchi badala ya kubuni mambo ya maendeleo yao kuwaingizia kipato, akili mgando sana.
 
Duuh kumbe Singapore ni mteremko hivi? Ngoja nianze kukusanya paka then niwaexport nikauze kule
 
Back
Top Bottom