Hoteli ya Kwanza Afrika Ndani ya Maji - Zanzibar

FM facts

Member
Mar 16, 2019
45
88
Hii ni Hoteli iliyo na Vyumba vya Kulala Ndani ya Maji Zaidi ya Futi 30 Chini katika Bahari ya Hindi - Zanzibar, Tanzania na Inaitwa "Manta Resort" na Imetajwa kama Moja ya Hoteli Bora Duniani Kati ya Hotel Zilizopo Ndani ya Maji.

Hii ndio Hoteli ya Kwanza Kabisa Barani Afrika Kujengwa ndani ya Maji, Ipo Pemba-Zanzibar-Tanzania Katika Bahari ya Hindi na Imejengwa Umbali wa Futi 820 Kutoka Ufukweni mwa Bahari (Kutoka Nchikavu).

Ilizinduliwa Rasmi Miaka 5 Iliyopita na Kuna Jumla ya Chumba 1 cha Kulala kilichopo ndani ya Bahari na Bei ya Kulala Usiku Mmoja hua Inabadilika Kutokana na Msimu, Kuna Msimu Hufika Hadi Tshs. Milioni 3.5, na Hii ni Bei ya Juu Zaidi Kulala Kwa Siku Mmoja, Ni Hotel ya Nyota 4 (4 Star Hotel).

Bei za Kawaida ni:
Masaa 3: Million 1.5
Masaa 5 (Nusu Siku): Million 1.7
Siku Moja (Masaa 8): Million 2.4

Kama Ukienda Kwa Lengo la Kutalii, au Ni Mteja Umelipia Chumba na Unataka Kutalii/ Kupunga Upepo Gharama Yake ni Wastani wa Tshs.170,000/= Kwa Mtu Mmoja na ni Kwa Masaa 2-3 na Unatembezwa na Boti.

Ikiwa Mteja Umelipia Chumba na pia Unahitaji Kujifunza Jinsi ya Kuvua Samaki Gharama yake ni Wastani wa Tshs. 70,000/= Kwa Mtu mmoja na Unakuwa Katika Boti, na ni Kwa Muda wa Masaa 2-3.

Ikiwa Ni Mteja Unayehitaji Kuelekezwa Vitu mbalimbali Binafsi Basi Gharama yake ni Wastani wa Tshs. 460,000/= kwa Mtu Mmoja kwa Siku Moja.. Lakini pia Kuna Huduna Nyingine Kama Kupiga Mbizi N.K

Instagram: @themantaresort
Website: themantaresort.com/

Hoteli hii inamilikiwa na Kampuni Moja Kutoka Nchini Sweden na Inamilikiwa na Mwekezaji Maarufu wa Mahotel Anayeitwa 'AB' Chini ya Mradi wake Uliopewa Jina la "Kwanini".

Mwaka 2007 Kampuni hii Ilikua ikitafuta Eneo la Kujenga Hoteli itakayokuwa Yakipekee ya Ndani ya Maji na Kuvutiwa na Eneo hilo lililopo Pemba na Kuanza Mchakato wa Ujenzi kwa Kushirikia na Serikali ya Zanzibar... Inamiliki Eneo la KM. 1 Katika Ufukwe wa Bahari.

Moja ya Hotel Nyingine ya Ndani ya Maji ni 'Poseidon Undersea Resorts' -FIJI.. Hii Itafunguliwa Rasmi Mwakani 2020 na Itakuwa na Uwezo wa Kuingiza Hadi Watu 150,000. Gharama yake Kulala kwa Usiku Mmoja itakuwa Wastani wa Tshs. 23M na Itakuwa ndio Hoteli ya Kifahari Duniani.

Zipo Nyingi Pia.



images.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom