Hoteli nzuri Morogoro isiyozidi laki moja

Hoteli nzuri Morogoro isiyozidi laki moja

Vigezo vyako nenda nashela Hotel itakufaa sana Security iko bomba mandhari na swimming pool
....Hapo kwenye security iko bomba nashauri apate uzoefu kwa mhe Malima...

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Habari...

Niende moja kwa moja kwenye hoja husika..

Naomba kufamishwa hotel nzuri Morogoro, ni mara yangu ya pili, mara ya kwanza nililala Flomi hotel na nilipapenda sema mi napenda swimming na utulivu fulani, ila kwa pale flomi room nzuri sema hakuna ivyo vigezo vyangu, ila kila kitu kilikua poa sana kuanzia rooms na mazingira ya ndani kwa ujumla.

Naomba kujuzwa hotel zenye vigezo ivyo ninavyoitaji na bei isizidi laki 1 kwa siku.

Kama huna ushauri, bora upite kimya kimya kuliko kuweka utani au matusi.

Naomba kuwasilisha

Jaribu ' Kahumba ' Guest House Mkuu hutojutia kwani achilia mbali tu kuwa na Bei ndogo kuliko hiyo uliyoiweka katika ' Bajeti ' yako ila pia ' utafaidika ' na ' Vivutio ' vya ' Kutukuka ' kabisa vinavyopatikana hapo hapo katika ' Kahumba ' National Park katikati ya Jiji la Morogoro.
 
Vigezo vyako nenda nashela Hotel itakufaa sana Security iko bomba mandhari na swimming pool
Kuna mtu aliibiwaga binduki ya SMG hapo

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kufamishwa hotel nzuri Morogoro, ni mara yangu ya pili, mara ya kwanza nililala Flomi hotel na nilipapenda sema mi napenda swimming na utulivu fulani, ila kwa pale flomi room nzuri sema hakuna ivyo vigezo vyangu, ila kila kitu kilikua poa sana kuanzia rooms na mazingira ya ndani kwa ujumla.

Mie nikiwa safarini Iringa niliingia Morogoro na gari niko chicha sana, polisi walinipeleka hoteli fulani nililala bure. Iko njia ya kwenda Klilakala Girls', na ina ulinzi mzuri sana, ila sikumbuki jina lake. Naona usiku walipuliza dawa ya mbu inanuka vibaya! Asubuhi walini-check out nikaendelea na safari.
 
duh yaan uko chicha ht hujitambui?kisa ninn! aisee!
 
Matata ya muasi na mobali esila te na mokili Mkuu.

ahahahaa kuna watu hamjipendi na maisha yalivyo matamu namna hii!yaan nimejikuta nakushangaa! chicha??/mh pre rest in peace mzeiya!(jokes aside)
 
Biashara huria sheeda! Label muhimu zaidi ya content while price more fascinating than value!
 
Back
Top Bottom