Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Hatimaye Hoteli ya Kitalii ya Snowcrest,iliyopo eneo la Ngulelo jijini Arusha, imefilisiwa rasimi mara baada ya kushindwa kujiendesha kutokana na madeni mbalimbali makubwa inayodaiwa na taasisi za kifedha ,watu binafsi yanayofikia kiasi cha sh, bilioni 14.
Hotel hiyo ambayo iliwahi kuzinduliwa kwa mbwembwe na Rais wa Awamu ya NNE Rais Jakaya Kikwete ,inamilikiwa na mfanyabiashara William Mollel ambaye aliinunua kutoka kwa mfanyabiashara aliyetambulika kw a jina la Tarimo.
Majira ya Alfajiri kampuni ya udalali iliyopewa mamlaka na Mahakama chini ya usimamizi wa askari Polisi wenye silaha , imekomba kila kitu katika hotel hiyo yakiwemo magodoro,Pazia, zamani mbalimbali, Viti,TV,Vyombo,vitanda, Kompyuta,Shuka ,Taulo nakadhalika na kuviacha vyumba zaidi ya 100 vyeupe.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya udalali vitu vyote vilivyotolewa vikiuzwa uwezekano wa kufidia madeni hayo bado ni mdogo na hivyo hatua ya kuiomba Mahakama kuuza jengo zima inaweza kufikiwa muda wowote.