Ndio maana hii nchi haiendelei. Wachawi kila kona, Mtu unaweza ukadhani wachawi ni wale wanaoruka na ungo usiku, kumbe wengine wanatembelea Kilimo kwanza. Unaanzaje kubomoa jengo kama hilo. Kwani wao walikuwa wapi tangu msingi unaanza kuchimbwa?
Ahaaaaaa.
Mkuu kumbe ni maeneo yako hee!!!!!
Yule jamaa kapiga HELA ndefu sana mpaka sasa.
Bcoz even familia yake nasikia wanaishi kwa Obama.
By the way huku kwema kabisa mkuu.
Ila pale Ngemo bar pasivunjwe maana ugali wa pale na nyama choma saa mbili asubuhi ni balaaaaaa,yani unaenda town uko saaaaafi na lichupa la maji la lita moja na nusu.
Mjengaji na watoa vibali ni sawa na mtoaji na mpokea rushwa. Jengo livunjwe. Watendaji wawajibishwe.hao walijenga wamefanya makosa. lakini watendaji wa serikali walikuwa wapi kuzuia huu ujenz kuanzia ujenzi unaanza? kawaida ujenzi wa gorofa lazima halimashauri ijue na inginia wa halmashauri lazima ahusike. walikuwa wapi wote hawa? serikali isiishie tu kumbomolea huyo jamaa bali iende mbele zaidi kuwawajibisha waliohusika na uzembe huu. to sad.
Mjenzi na watoa vibali wachunguzwe. Ila jengo ni haki kubomolewa kama lipo kwenye kiwanja kisicho sahihi.Hivi kama kiwanja kapewa na manispaa na amekitafutia hati, kibali cha ujenzi anacho na kipo kihalali, taratibu zote kafuata..hawezi kuishitaki serikali na kudai fidia kama jengo likibomolewa?
Watamuua kwa presha mjaluo wa watu masikini dahh!
Mahakamani hata kama ulivunja sheria? Sheria haziangalii kiasi ulicho invest. Hata masikini wamevunjiwa, yeye nani asivunjiwe kama kiwanja si halali?Hapo mmiliki anatakiwa akimbilie mahakamani kuweka pingamizi. Hakuna mtu aliye juu ya mahakama bana. Kuna jengo kama hili lilitaka kuvunjwa Masaki miaka ya 2007. Serikali yenyewe ili back down na mpaka sasa yale majengo yapo.... Duh kamji ka Morogoro kalishaanza kupendeza,sasa wawekezajai wooote watakimbia...
Kweli kabisa...Wataisoma namba!huu uzembe wa watendaji,kutiana hasara tu,waliohusika na uzembe huo wafungwe jela miaka mia.iwe fundisho kwa matajir,kwa mara ya mwisho nimelala humo mwez october chumba 160000 tu.
Watanzania Tujifunze kuishi kwa kufuata sheria ndio tutaendelea, Huu ukanjanja ndio kama hivyo ikija serikali mpya mambo yanabadilika!
Kikwete alikuwa dhaifu, Magufuli ni muumini wa kufuata Sheria!
Huyo mmriki nae boya tu atafanyaje uwekezaji mkubwa namna hii bila kufanya upembuzi yakinifu? hotel kubwa namna ile unaijenga juu ya bomba la mafuta?? no wonder pesa ya uwekezaji huo itakuwa ni dirtyMONEY
Imejengwa juu ya bomba LA mafuta LA TAZAMA no lazima ibomorewe tu
Hotel inaitwaje. Ila hii sio nzuri mtu amejenga kamaliza huduma zimeanza afu inabomolewa. Siasa hizi
Sina tatizo na kubomoa kama imejengwa eneo lisilo haki kujengwa, ila waanze na kunyoosha maelezo kwanza kuwa huwa wanakuwa wapi majengo hayo yakijengwa? Adhabu za uzembe kazini zianzie kwao...
Huo ni upuuzi... Siwezi kumwaga pesa yangu kwenye sehemu yenye utata kama hiyo, muulize huyo mwenye hotel kama alipata hilo eneo kihalali kama sio kwa ufisadi!Sheria huwa zinafuatwa vizuri kwenye nchi zenye mipango, huwez kubomoa mali za watu kwenye nchi ambayo asilimia 80 haijapimwa, bongo hata leo hii ukinunua kiwanja mwaka kesho utaambiwa ni eneo la makaburi
Huo ni upuuzi... Siwezi kumwaga pesa yangu kwenye sehemu yenye utata kama hiyo, muulize huyo mwenye hotel kama alipata hilo eneo kihalali kama sio kwa ufisadi!
Halafu kesho ukisiki kwa Ujenzi wa hiyo hoteli amezui mkondo wa maji na kusababisha mafuriko yaliangamiza roho kadhaa kwa raia wasio na Hatia sijui utasema nini!
Ww ni mtu wa ajabu sana, inawezekana ni wale watu ambao wana mawazo ya kusadikika hujawahi kujenga hata kibanda hujakumbana na changamoto za kununua maeneo yenye matatizo ilihali umeenda hadi jiji kutafuta ukweli, mm sitetei watu wasiofuata sheria lkin ujue kuna watu wanaonewa sana kwene masuala ya ardhi ukiwa hujawahi kukumbana na hizo kadhia mshukuru Mungu wako lkin usituletee theory za darasanai hapa.