Hapa niko hospitali ya rufaa Mbeya,kuna wagonjwa ambao wamefika tangu saa 1,mpaka sasa ni saa 4 bado huduma hazijaanza eti madaktari wapo kwenye kikao...kiukweli napata tabu kupata jibu kwamba..>ni kwa nini vikao vinafanyika muda wa kazi?wakti huohuo ikifika saa 6 tu watasema muda wa lunch...hivi ni lini watanzania tutajali muda? aah Tanzania ingekuwa daladala tungeshuka wengi tukapanda daladala nyingine.!
Pole ndugu yangu, hiyo ndiyo Tanzania. Sisi hapa Moshi siasa zinatuumiza kabisa. Kwa sababu jimbo la Moshi linaongozwa na upinzani wizara ya afya imegoma kurekebisha kasoro za chumba cha upasuaji hapa mawenzi. Kwa sasa wagonjwa wanahitaji huduma ya upasuaji inawabidi waende St Joseph au KCMC.
Hii ndio hospitali ya rufaa kwa mkoa wa kilimanjaro iliyopandishwa hadhi kimaandishi ila huduma bado finyu kabisa. Huwezi kuamini ni zaidi ya miaka miwili wanatesa wananchi kwa sababu tu ya kutumia haki yao ya kidemokrasia.
Ukifika hapa utawaonea huruma wagonjwa wa majeruhi wanaoletwa hapa. manake kama unahitaji huduma ya upasuaji ndio hivyo tena utakubidi upelekwe sehemu nyingine.
Nimeulizia sababu za chumba cha upasuaji kufungwa nikaambiwa ni kutokana na uchakavu wa vifaa na mazingira mabovu yaliyosababisha kufungiwa tangu 2012.
Nichukue fursa hii kuomba kwa viongozi wa wizara ya afya kuacha siasa kwenye maisha yetu.
Jioni njema wote.