Nafikiri ni vyema baadhi ya watu kama wewe wakapewa ufahamu wa mambo yafuatayo:
1. Kuna watu wanalipa kodi kwa lazima na wengine wa hiari lakini matumizi ya kodi zao ni kwenye kustarehesha baadhi ya watu huku wengine wakipata shida sana na kuona huduma mbovu.. Hii peke yake ni stress tosha..
2. Kuna maeneo mengi yanakosa huduma za msingi. Kwa mfano ukijaribu kutembea kwenye hospitali za vijijini na hata kwenye miji mikubwa, kama sio misaada ya nchi kama Marekani na wafadhili wengine nakuhakikishia hali ingekuwa balaa zaidi. Imagine, lab machines au equipments, drugs, computers, urekebishwaji wa vituo vya afya, allowances za madaktari na wauguzi kwenye vituo vya afya ili wafanye kazi muda wa ziada, ulipwaji wa mishahara kwa baadhi ya wauguzi au wafanyakazi wa vituo vya afya; vyote hivi unafanywa na donors and kuna watu wengine wanaenda kuvitumia vyote hivi kwenye kampeni na kutaka kusifiwa kama unavyoshauri wewe.. Umeona watu wanavyolala chini kwenye mahospitali huku wabunge wanalilia laki tano kama posho na huku hadi wafanyakazi wa chini serikalini wanatembelea V8..?
3. Barabara mbovu, unapita kwenye miji mikubwa kama Dar na bado kuna mapango kibao barabarani...
4. Huduma mbovu za maji.. Imagine Dar tu watu wanatembea na toroli zenye madumu hadi sehemu za mijini kisa hakuna maji safi na salama..
5. Elimu duni.. Watu mpaka wanaishia kusifia Division 5 na kuona kiwango cha kufeli ni jambo la kawaida, litapita tu...
Sasa vyote hivi halafu mtu akose stress..?? Unless wewe ni wale wanaofaidika na system...