Hospitali ya Vichaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Vichaa

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Hmaster, Jun 6, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kutaka kujua maendeleo ya afya za wagonjwa wa akili (vichaa) katika hospitali fulani daktali huangalia mienendo ya wagonjwa wale tu: yule anayeenenda vizuri huamini kwamba ana nafuu kubwa au amepona hivyo humruhusu arudi nyumbani.
  Siku moja daktari huyo aliingia katika wodi ya wagojwa hao, wengi walionekana bado ni wagonjwa kwani walikuwa wanafanya fujo na kupiga kelele hovyo isipokuwa watatu tu. Akaamua kuwachunguza hao watatu tu kwa siku hiyo, na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo.
  Daktari: Vipi bwana mbona umekaa peke yako pembeni kabisa wakati wenzio wote wanacheza, wanapiga kelele na kuongea?
  Mgonjwa No.1: Samahani usije hapa kwa vile mimi ninataga, nikimaliza tu nakwenda kwa wenzangu. Daktari akamwacha akijua kumbe hata yeye bado ni mgonjwa akamwendea mwingine ambaye alikuwa hapendi kukaa ndani na wenzie badala yake alikuwa anakaa tu mlangoni.
  Daktari: We vipi mbona hukai ndani na wenzio kwa nini?
  Mgojwa No.2: Mi sifanani na hao waliopo humo ndani na kama unataka nikae ndani labda unijengee banda langu huku nje lakini usinichanganye na hao. Daktari aliposikia maneno yale aliona kwamba huenda yule bwana keshaanza kupata fahamu na kujitenga na vichaa hivyo alimuuliza swali moja tu la kizushi.
  Datktari: Una maana gani kusema kwamba hufanani na walio humo ndani?
  Mgonjwa No2: Mimi si ndiyo nawalinda hawa walio humu ndani, sasa tangu lini mbwa analalaga ndani. Daktari alichoka na akabaki kutikisa kichwa tu na tumaini lake kwa siku hiyo lilibaki kwa mmoja tu ambaye wakati wote huo alionekana kuamulia magomvi ya wenzie humo ndani na kuwazuia kelele. Daktari: Vipi bwana naona wanakusumbua sana wenzako kwa magomvi?
  Mgonjwa No3: We acha tu ndugu yangu, kama usiku wa kuamkia leo ndo sijalala kabisa kwa kelele zao.
  Daktari: Unaonaje kama nitakuruhusu urudi nyumbani kwako?
  Mgonjwa No3: Ntashukuru sana kama itakuwa hivyo! Daktari baada ya kupata majibu hayo alipata shauku ya kumtoa akiamini kwa majibu na busara ile lazima alikuwa amepona; akamwambia ajiandae na amsindikize standi ya basi. Baada ya maandalizi mafupi akawa tayari kwa ajili ya kuondoka. Kilichomshangaza daktari na kumuona mgonjwa wake bado ni swali hili lifuatalo:
  Mgonjwa No3: Mbona tunaipita sheli mafuta tutaweka wapi dereva, tutazimikiwa na gari?
  Daktari: Tuweke mafuta kwani sisi ni gari?
  Mgonjwa No3: Sasa, hebu sikiliza honi yake: pipiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Palepale Daktari akaomba msaada wa watu ili wamsaidie kumrudisha hospitali kwa matibabu zaidi.
   
 2. j

  jahboy New Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inaboa
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Haijatulia!
   
Loading...