DOKEZO Hospitali ya K’s Mbeya mna huduma mbovu

DOKEZO Hospitali ya K’s Mbeya mna huduma mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Jengo kubwa, huduma sifuri
Dah basi imebadilika Sana kama ndio hivyo ilkua hospitali smart Sana mwaka 2001 nimeugulia hapa almost mwaka mzima huduma ilkua nzuri Sana. Madaktari vijana wanachangamoto Sana aisee Mie kuna hospitali moja Kigoma MAC-REN niliwahi kaa saa nzima jamaa anapiga Stori tuu na demu na kuchekacheka tuu nlisepa na majibu ya maabara na sikuwahi kurudi tena
 
Sina muda wa kueleza sana, nimechoka.

Mmeajiri madaktari vijana wanakaa wanapiga story tu vyumbani badala ya kuhudumia wagonjwa. Watu tumekaa zaidi ya lisaa tunasikia wanachekacheka tu ndani na hakuna mgonjwa.

Unaingia kwa daktari wamekaa kama watatu mmoja anakuhoji wengine wanakuangalia na kujifanya wanachezea simu. Kama mtu ana jambo la siri anaelezaje?

Sijawahi kuona Hospitali ina utaratibu mbovu kama hii, unafika reception mmewaweka vijana wa field wana dharau kama nini: wanaongea kama hawataki. Mtatupeleka kwa amri tu “njooni huku”, “kaa hapa” yaani kama mnatupa huduma bure.

Sintakaa nije kupata huduma kwenu tena.

MAJIBU YA HOSPITALI YA K's
Akizungumzia tuhuma hizo, Suma Kabuje ambaye ni Afisa Mahusiano wa Hospitali ya K’s, amesema: "Taarifa hizo siyo za kweli, kwanza hatuna wanafunzi wa field kwa mwaka huu wote (2022), kuhusu madaktari wetu kila mtu ana chumba chake, unapomuona daktari chumba kingine basi ameenda kutoa msaada."

"Kwa leo wameingia madaktari wawili, daktari mmoja anamsaidia mwingine."

Kuhusu madai ya uwepo wa nzi wengi hospitalini hapo amesema: "Sehemu zetu ni safi na mazingira yetu hayana uchafu pia."
Kwanza hata namba zao mtandaoni wameweka ambayo haipatikani
 
Back
Top Bottom