Hospitali ya Kairuki yakanusha tuhuma za mgonjwa kuachwa na vifaa mwilini wakati wa upasuaji

Faraji2017

Member
Feb 4, 2017
21
8
TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA TUHUMA ZA MGONJWA KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI

Uongozi wa Kairuki Hospital umepokea na kusoma kwa masikitiko taarifa zilizoandikwa na magazeti ya tarehe 28/8/2017 pamoja na kusambazwa kwenye rnitandao mbalimbali ya kijamii kuwa hospitali yetu imemsababishia mgonjwa madhara ya kizazi kwa kurnuacha na vifaa vya kuzalishia ukeni.

Magazeti yaliyotufikia yakiwa na tuhuma hizo ni pamoja na gazeti la Uhuru toleo na. 22847, Mtanzania toleo Na. 8651 pamoja na Daily News lenye toleo Na. 12021 yote yakiwa ya tarehe tajwa hapo juu.

UKWELI KUHUSU MGONJWA ANAYETAJWA
Hospitali inakiri kuwa iliwahi kumhudumia mama mjamzito aitwaye Khairat Shaib Omary mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam mnamo mwaka 2016. Mama huyo alihudumiwa kwa muda wa ujauzito wake kwa nyakati tofauti alizofika hospitalini kwetu. Pia alihudumiwa kwa kupewa huduma za kujifungua ambapo tarehe 15/12/2016 alijifungua kwa njia ya upasuaji baada ya njia za kawaida kushindikana kwa sababu zisizozuilika kitabibu. Mnamo tarehe 17/12/2016 mama huyo na mtoto wake waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari wetu kuridhika kuwa afya ya mama na mtoto zilikuwa salama na wakiendelea vizuri.

Mama huyo alirejea tena hospitalini kwetu tarehe 21/12/2016 kwa ukaguzi wa kawaida baada ya kujifungua ambapo daktari aliyemhudumia aliridhika kuwa afya ya mama huyo ilikuwa salama na hakuwa na tatizo lolote kwani hata kidonda cha mshono wake kilikuwa kikiendelea kupona vizuri. Mama huyo hakurejea tena hospitalini hapo kwa matibabu wala huduma zaidi ya hapo mpaka leo.

TUHUMA KUHUSU KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI
Kwa mara ya kwanza, tuhuma kuhusu mgonjwa aitwaye Khairat Shaib Omary, ziliwasilishwa kwetu mnamo tarehe 10/7/2017 kufuatia barua ya wakili wake aitwaye Jonas Estomih Nkya wa kampuni ya Jonas & Associates Law Chambers ambaye alitutaka tumlipe mteja wake Milioni mia Sita (Tshs.600,000,000/=) pamoja na riba ya asilimia ishirini na moja (21%). Hospitali yetu ilikanusha

kuhusika na tuhuma na madai ya Bi. Khairat Shaib Omary ambaye aliamua kufikisha madai yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu katika kesi Namba 184 ya mwaka 2017 akidai fidia mbalimbali.

Wakati kesi hiyo ikiwa tayari imepangiwa Hakimu wa kuisikiliza pamoja na tarehe ya kuitaja mahakamani, mgonjwa huyo ameendelea kutumia vyombo vya habari kutuchafua kwa nia ambayo sisi tunaamini ni kutaka kushinikiza hukumu yenye upendeleo kutoka mahakamani, kitendo ambacho hakikubaliki kamwe.

Hospitali yetu inapenda Umma ufahamu kuwa baada ya tarehe 21/12/2016, Bi Khairat Shaib Omary, anakiri katika hati zake za madai, kuwa alihudumiwa katika hospital nyingine tofauti kama vile Tanzania Occupational Health Services, Regency Hospital na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa nyakati tofauti. Hata hivyo, hakuwahi kutaarifu hospitali yetu kuhusu huduma alizopewa kwenye hospitali hizo.

Hospitali inakanusha tuhuma zilizoandikwa na magazeti tajwa hapo juu kwa kuwa hazina ukweli wowote. Endapo mgonjwa anayetajwa na magazeti anayo madai ya msingi dhidi ya Kairuki Hospital, alitakiwa kusubiri taratibu za Mahakama alizokwishazianzisha iii alete ushahidi na kuthibitisha tuhuma zake.

Kairuki Hospital tunasikitika kuona vyombo vya habari tajwa hapo juu vikiandika habari za kututuhumu bila kutuhoji wala kutupatia fursa ya kueleza nafasi yetu na nini kilifanyika kuhusu mgonjwa huyo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki zetu za msingi pamoja na maadili ya wanahabari.

Kairuki Hospital tunataka Umma, wateja wetu, wadau na wafanyakazi wote kuwa wazipuuze tuhuma zinazoendelea kuandikwa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kuhusu kuacha vifaa vya kuzalishia kwenye uke wa mgonjwa kwani hazina ukweli. Aidha, tunasikitika kwa usumbufu ambao umeshajitokeza kufuatia taarifa hizo.

Kwa sasa, Kairuki Hospital ipo katika mchakato wa kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha haki inatendeka kwa upande wetu na kukomesha vitendo vya wanahabari kutuhumu bila kupata maoni na taarifa sahihi za upande wa pili.

Imetolewa leo tarehe 28/8/2017.

Arafa Juba

Afisa Habari

KAIRUKI HOSPITAL

Kujua zaidi kuhusu mkasa huo >>> Hospitali Hubert Kairuki matatani kwa kusahau pamba kwenye kizazi wakati wa upasuaji

upload_2017-8-29_7-47-42.png

32c58897-d585-4d0b-8e03-49107395b9d2
 
Nilisikia ndani ya tumbo la uzazi jana kwenye magazet ukeni tena!!!
 
MSEMAJI WA KAIRUKI ANASEMA UKENI HUYU HUKU ANASEMA NDANI YA MFUKO WA UZAZI VITU VIMESAHAULIKA.

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Khairat Omary, ameishtaki Hospitali ya Kairuki na kudai fidia ya Sh milioni 155 kwa kumsababishia matatizo katika mfuko wa uzazi yaliyofanya aondolewe kizazi.
Khairat kupitia Kampuni ya Uwakili ya Jonas amefungua kesi ya madai namba 184 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Katika madai hayo, mdai anadai alikuwa akihudhuria kliniki wakati wa ujauzito katika hospitali hiyo na Desemba 15 mwaka jana alijifungua kwa upasuaji, akaruhusiwa Desemba 17 mwaka huo na kutakiwa kurudi tena Desemba 21.
Mdai akiwa nyumbani alianza kusikia maumivu ikiwamo kutapika, ilipofika Desemba 21 alirudi hospitali akaeleza maumivu anayopata kwa daktari ambaye alielekeza afanyiwe kipimo cha Ultra Sound.
Majibu yalipotoka daktari akampatia dawa za kutuliza maumivu na kumtaka apumzike hali itaendelea kuimarika.
“Akiwa nyumbani hali iliendelea kuwa mbaya, alisikia maumivu makali ya kichwa na alianza kubadilika rangi ambapo alikimbizwa hospitali ya jirani, walipompima wakaelekeza apelekwe Regency Hospital kwa matibabu zaidi.
“Regency walimfanyia vipimo na kubaini kuna tatizo katika mfuko wa uzazi na kumuhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia walimfanyia vipimo na kubaini wakati alipofanyiwa upasuaji kuna vitu vilibakia kama pamba ambavyo vimesababisha mfuko wa uzazi kuharibika,” ilisema sehemu ya hati hiyo ya madai.
Anadai ili kuokoa maisha yake alishauriwa kuondolewa kizazi, hata hivyo licha ya kuondolewa alibakia na tatizo la fístula lililosababishwa na pamba zilizoachwa wakati anajifungua.
 
Kazi ipo...ila hapo ni kiasi cha MNH kutoa taarifa yao, Regency kutoa taarifa yao!
 
Inawezekana kabisa, maana kama Medical Doctors (watabibu) wenyewe wa kairuki ni wale wanaotembea asubuhi na uniform wanavalia barabarani wakitokea kwenye majengo ya pale mkabara na hospital kama watoto wasio kuwa na makazi!!

Nilikuja nyumbani , Tanzania nikaona wanavyovaa nguo barabarani nikasikitika sana na nguo zenyewe chafuuuuuu hazina tena rangi ya weupe bali zimeanza kuwa na rangi ya cream!!!

Siwezi kupinga hilo, wao wenyewe hawajielewi sasa kutibu wanaweza!?

Pole sana , mgonjwa kwa masahibu yaliyokukuta.
 
Sasa kama vifaa viliachwa ukeni si rahisi tuu kuondoa na mkono? Kwa nn mpaka kizazi kiharibikeee? Wakae wayajadili wayamalize.
 
Inawezekana kabisa, maana kama Medical Doctors (watabibu) wenyewe wa kairuki ni wale wanaotembea asubuhi na uniform wanavalia barabarani wakitokea kwenye majengo ya pale mkabara na hospital kama watoto wasio kuwa na makazi!!

Nilikuja nyumbani , Tanzania nikaona wanavyovaa nguo barabarani nikasikitika sana na nguo zenyewe chafuuuuuu hazina tena rangi ya weupe bali zimeanza kuwa na rangi ya cream!!!

Siwezi kupinga hilo, wao wenyewe hawajielewi sasa kutibu wanaweza!?

Pole sana , mgonjwa kwa masahibu yaliyokukuta.
hao unaowazungumzia wewe ni wanafunzi na wanakuwa wanaenda darasani kusoma na wala hawatibii mtu. We ni mtu mzima kabla hujaandika kitu uwe unafikilia kwanza na uwe na uhakika. Acha kuzungumza vitu visivyo na uhakika.
 
hao unaowazungumzia wewe ni wanafunzi na wanakuwa wanaenda darasani kusoma na wala hawatibii mtu. We ni mtu mzima kabla hujaandika kitu uwe unafikilia kwanza na uwe na uhakika. Acha kuzungumza vitu visivyo na uhakika.


Mmmmmh, huuuh, huuuuh huuuuuh!!

Unadhani Mimi siijui Africa na Tanzania nimetembea karibu nchi zote za Africa hakuna jipya wote ni wale wale!?

Acha kujifariji, ao hao wanatibu na wanadunga hadi sindano, drip wanaweka na mara moja moja hupelekwa kwenye vyumba vya upasuaji

OK, let us say, ni wanafunzi sasa kwa watu wanaotakiwa kuwa MD na anavalia nguo barabarani tena anavalia uniforms za MD's zilizo chafuuuuuu atashindwa kusahau au kuacha vifaa kwa mtu anayefanyiwa upasuaji!?

Taaluma, zingine inabidi mtu awe makini sana kwa vitu vidogo ili aweze kufanya mambo mkubwa.

Any way, endelea vivyo hivyo.
 
Hamjasoma vizuri magazeti yanasema ukeni upo alafu naisi uyu msemaji anatoa kilicho sahihi waandishi wetu uwa wanakirupuka kuandika na mambo mengine ya kitabibu hawawez kuandika uke kwao ni mshangao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..hili linawezekana kabisa....kama Muhimbili walimkata ubongo mgonjwa wa mguu Na mguu Mgonjwa wa ubongo watashindwa mikocheni kufanya blunder kama hiyo????.....kwa tz yetu kila kitu kinawezekana...tena siku hizi wanatafuta hela kwa nguvu sana huko mahospitalini.... Unakuta mama k inaweza kupitisha mtoto lakini anapigwa operation....ili tu kupiga hela...ifike mahali kuwe Na quality assurance kwenye hizi hospital...Na kesi kama hizi ndio zitawaamsha waache kuwaibia wagonjwa....inaitwa karma...
 
Tusubiri ufafanuzi zaidi ndo tutaelewa tusihis kwanza ukiangalia kiafya MTU hawezi kukaa na vifaa vya uzazi tangia January hadi July na hakawa salama ni kama geresha vile

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nisha kwenda pale ila pale kuna wanafunzi wa udaktari na madaktari wenyewe Sawa Sawa na muhimbili kuna wanafunzi na madaktar ukiwa unaelewa ni rahisi kujua mwanafunzi ni yupi na Dr ni yupibivyo naisi hao wa barabaran ni wanafunzi na hawahusiki nakutoa uduma pia ukienda mwanayamara unakutwa unahudumiwa na wanafunzi kutoka vyuo mbal mbali wako kwenye mafunzo hivyo issue hii naona iangaliwe niwapi mistake ilitoke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmmmh, huuuh, huuuuh huuuuuh!!

Unadhani Mimi siijui Africa na Tanzania nimetembea karibu nchi zote za Africa hakuna jipya wote ni wale wale!?

Acha kujifariji, ao hao wanatibu na wanadunga hadi sindano, drip wanaweka na mara moja moja hupelekwa kwenye vyumba vya upasuaji

OK, let us say, ni wanafunzi sasa kwa watu wanaotakiwa kuwa MD na anavalia nguo barabarani tena anavalia uniforms za MD's zilizo chafuuuuuu atashindwa kusahau au kuacha vifaa kwa mtu anayefanyiwa upasuaji!?

Taaluma, zingine inabidi mtu awe makini sana kwa vitu vidogo ili aweze kufanya mambo mkubwa.

Any way, endelea vivyo hivyo.
We umetembewa wapi ulikuwa unaenda kufanya nini kama si kila hospital uliitembelea inaonekana wewe kiboko au unapitia mahospital kucheck if.......tupe ufafanuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom