Hospitali ya Kairuki, hawa vijana ni madaktari au majaribio?

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,162
794
Nilikuwa katika kupata huduma za hospitali hii pendwa jijini. Yanayotendeka sijui kama wahusika wakuu wanaelewa hilo. Wakati huu ambao ajira ni shida ni maajabu kumkuta daktari anafanya hovyo ofsini kwake.

Kwa ufupi na sio mimi tu siridhishi na huduma za madaktari baadhi sio wote. Vijana mabishoo unaowaona kama consultant hawana credibility..na unaweza ukadhani hawana ujuzi wala uzoefu kutibu binadamu.

Haiwezekani unapewa majibu halafu yeye anatoa maelekezo ya kupewa dawa tofauti na tatizo la mgonjwa. Nashauri mtazame vema hawa madaktari. Nenda maabara kwa kutoa majibu ya uwongo hawa jamaa hatari...sijui mashine zao hazijui kusoma wadudu?

Mtu ama malaria anaambiwa hana...anakaa weweee na malaria hadi imuondoe duniani? Acheni mzaha na maisha na roho za binadamu


ova
 
Mi nawakataliaa..not to that extent.Au mleta mada una ndugu ana hospital imebumaaa unaona wivuuuuu!! Wenzio wanashamiri..kama tatizo ni baadhi ya daktari ungeenda chumba cha malalamiko kipooo Ndo ungesikilizwa kwa kuwa matatizo kama hayo hata hospitali kubwa yapoo Usiwashushie Credibility yao.Kailuki..is one of the Best Hospital in TZ by now.
 
Mi nawakataliaa..not to that extent.Au mleta mada una ndugu ana hospital imebumaaa unaona wivuuuuu!! Wenzio wanashamiri..kama tatizo ni baadhi ya daktari ungeenda chumba cha malalamiko kipooo Ndo ungesikilizwa kwa kuwa matatizo kama hayo hata hospitali kubwa yapoo Usiwashushie Credibility yao.Kailuki..is one of the Best Hospital in TZ by now.


Good
 
Cha kukusaidia tu madaktari wa vyuo vya private ufaulu wao ni kuanzia div 3 had I 4 ,tofauti na muhimbili uwezo some a udaktari kwa div 3
 
Madaktari vijana wana matatizo sana .....daktari anafanya ubishoo na mapozi kibao while unaumwa au una mgonjwa serious ....toka unaingia chumba cha daktari ni kama umeenda kumsumbua vile ....mmiliki wa hospital ya Rabininsia awe makini na vijana wake pia ....kuna ethics za kudeal na mgonjwa ....na wasifanye kazi kama vile wamelazimishwa ingawa tunajua changamoto za madaktari ....
 
Serikali yenyewe hadi imetoa matangazo hadi kwenye redio na runinga lakini kuna vichwa vigumu kama huyu hawaelewi. 'Si kila homa ni malaria'.

Waache watu wafanye kazi kama taaluma inavyowaelekeza na si mapendeleo ya wagonjwa.
 
Watanzania bhna, mimi sipingani na unachoweza kuzungumza juu ya hili lakini naomba nikusisitize kwamba yapo magonjwa mengi ambayo yana dalili sambamba kabisaa na ugonjwa ulio utaja...

kuna katabia ambako kapo kwasasa mgonjwa anapoulzwa juu ya afya yake baadhi yao wanafikia hatua ya kudanganya ndio maana inafikia hatua unapewa paracetamol unaambiwa uende hii ni kwasababu taarfa ulizozitoa hazi relate na diagnosis iliyopo....
suala la wafanyakazi ni kwa baadhi yao ndo huleta majibu tofauti, na zipo sababu nyingi ambazo hupelekea majibu tofauti na matarajio....
Embu fikiria umetoa taarifa si sahihi na utegemee majibu sahihi haimake sense hata kidogo
Tusifikie hatua ya kulaumu kikundi fulani direct kwanza tujiulize je taarfa ulio itoa umeitoa sahihi?

Shime Watz baadhi yetu tuache hii tabia, tutoe taarfa sahihi kwa mustakabali wa afya zetu na vizazi vyetu....
 
Nilikuwa katika kupata huduma za hospitali hii pendwa jijini. Yanayotendekasijui kama wahusika wakuu wanaelewa hilo.

Wakati huu ambao ajira ni shida ni maajabu kumkuta daktar anafanya hovyo ofsini kwake.

Kwa ufupi na sio mimi tu siridhishi na huduma za madakar-baadhi sio wote.Vijana mabishoo unaowaka kama consultant hawana credibility..na unaweza udhani hawana ujuzi wala uzoefu kutibu binadamu.

Haiwezekani unapewa anatoa maelekezo ya kupew dawa tofauti na tatizo la mgonjwa.

Nashauri mtazame vema hawa madaktar

Nenda maabara kwa kutoa majibu ya uwongo hawa jamaa hatar...sijui mashine zao hazijui kusoma wadudu?

Mtu ama malaria anaambiwa hana...anakaa weweee na malaria hadi imuondoe duniani?

Aheni mzaha na maisha na roho za binadamu


ova

Uhandishi wako mkuu
 
Tatizo lingine wagonjwa wanakuja na magonjwa yao kichwani drs nina Uti,Malaria au typhoid vipimo vikitoka kama hana hayo magonjwa anajua drs hujui kutibu,kuna ugonjwa na magonjwa mengine yanayofanana Sio lazima kila mgonjwa anayetapika ana malaria.
Kwa malaria kuna clinical malaria endapo vipimo havijafanyika au magonjwa mengine yote mgonjwa hana na anadalili za malaria na kama vile amekaa maeneo kama Tanga,Dar es salaam,Morogogoro,pwani etc unaweza peana dawa za mgonjwa.

Na pia kuna Sheria za mgonjwa na sheria za mtoa huduma la msingi ni mgonjwa ajue haki zake na apokee ushauri anaopewa na drs.
 
Back
Top Bottom