johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,269
- 1,756
Kwa muda wa takriban wiki moja nimekuwa nikifuatilia matibabu ya jamaa yangu ktk hospitali hii.
Maeneo mengi wanajitahidi Kwa kiasi chao lakini kuna kero kubwa ktk mfumo wa malipo.
Ktk kudhjbiti mapato, hospitali ya Bugando imeacha kupokea cash na badala yake mgonjwa anapaswa kulipia kupitia benki ya crdb yenye vituo, eneo la emergency, namba tatu na namba sita.
Kabla ya huduma utapaswa kufahamu kiwango cha malipo ya huduma husika kama ni dawa, mionzi nk kutoka idara husika. Hapa ndio kimbembe.
Nitoe mfano wa kilichonitokea jana.
Mgonjwa wangu amelazwa namba zake, zikatakiwa dawa, hiyo ni saa kumi jioni, nikaelekezwa pharmacy ghorofa ya nane huko ni kwenda kufahamu kiasi cha malipo ya dawa, nilitumia nusu saa, nikaelekezwa niende namba sita kulipia Kwa wakala wa crdb, hapo nikatumia robo saa. Kisha kulipa hela iko ktk kadi, itakulazimu urudi namba Saba kupata risiti ya hospitali ili uende kupewa dawa.
Hapa nakutana na foleni hadi saa 12, sista mkatoliki anayetoa huduma anagoma kuendelea na kututaka tunailipia dawa kwenda kupata risiti namba mbili.
Kumbuka, hospitali hii imewazuia wasio wagonjwa au wafanyakazi kutumia lifti hata kama inapanda/ kushuka bila mtu.
Kufika Namba mbili licha ya foleni iliyokuwepo lakini tunaambiwa mtandao imepatikana hivyo hakuna huduma!
Kwenda eneo la emergency hali ni hiyo hiyo, nusu saa baadaye anakuja mtu wa crdb( jina nahifadhj Kwa sasa) anajaribu kadi yake ya visa bila mafanikio na hatimaye anapiga simu mfululizo kukueleza ni makao makuu naye anachemka na kutuacha bila msaada!
Saa Moja na dk tano usiku, dada aliyekuwa zamu, ambaye alificha kitambulisho chake, nyuma mbele, akatutaka twende namba mbili kwani muda wake umekwisha.
Huko namba mbili wakati huu ndio watu wote wanaohitajj huduma wamejazana ilihali mtandao hakuna.
Ni usiku tayari, fedha iko ktk kadi ya benki yenye mikataba na hospitali, narudi pharmacy kule ghorofa ya nane labda watanisikiliza, ajabu imefungwa!
Namfuata muuguzi wa mgonjwa wangu ananitaka niende pharmacy ya emergency iliyopo ghorofa ya pili ili nikajaribu kuwaomba wahusika wanisaidie dawa!?
Sasa imefika saa mbili Na nusu usiku, pesa nimekuwa, urasimu na matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati vinatugharimu Watanzania.
Wahusika angalieni hili pamoja na kuwepo Kwa namba za simu za wasimamizi ili kutoa msaada.