Hospitali ya Bugando inahitaji kujipanga

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,269
Reaction score
1,756
Kwa muda wa takriban wiki moja nimekuwa nikifuatilia matibabu ya jamaa yangu ktk hospitali hii.

Maeneo mengi wanajitahidi Kwa kiasi chao lakini kuna kero kubwa ktk mfumo wa malipo.

Ktk kudhjbiti mapato, hospitali ya Bugando imeacha kupokea cash na badala yake mgonjwa anapaswa kulipia kupitia benki ya crdb yenye vituo, eneo la emergency, namba tatu na namba sita.

Kabla ya huduma utapaswa kufahamu kiwango cha malipo ya huduma husika kama ni dawa, mionzi nk kutoka idara husika. Hapa ndio kimbembe.
Nitoe mfano wa kilichonitokea jana.

Mgonjwa wangu amelazwa namba zake, zikatakiwa dawa, hiyo ni saa kumi jioni, nikaelekezwa pharmacy ghorofa ya nane huko ni kwenda kufahamu kiasi cha malipo ya dawa, nilitumia nusu saa, nikaelekezwa niende namba sita kulipia Kwa wakala wa crdb, hapo nikatumia robo saa. Kisha kulipa hela iko ktk kadi, itakulazimu urudi namba Saba kupata risiti ya hospitali ili uende kupewa dawa.

Hapa nakutana na foleni hadi saa 12, sista mkatoliki anayetoa huduma anagoma kuendelea na kututaka tunailipia dawa kwenda kupata risiti namba mbili.

Kumbuka, hospitali hii imewazuia wasio wagonjwa au wafanyakazi kutumia lifti hata kama inapanda/ kushuka bila mtu.

Kufika Namba mbili licha ya foleni iliyokuwepo lakini tunaambiwa mtandao imepatikana hivyo hakuna huduma!

Kwenda eneo la emergency hali ni hiyo hiyo, nusu saa baadaye anakuja mtu wa crdb( jina nahifadhj Kwa sasa) anajaribu kadi yake ya visa bila mafanikio na hatimaye anapiga simu mfululizo kukueleza ni makao makuu naye anachemka na kutuacha bila msaada!

Saa Moja na dk tano usiku, dada aliyekuwa zamu, ambaye alificha kitambulisho chake, nyuma mbele, akatutaka twende namba mbili kwani muda wake umekwisha.

Huko namba mbili wakati huu ndio watu wote wanaohitajj huduma wamejazana ilihali mtandao hakuna.

Ni usiku tayari, fedha iko ktk kadi ya benki yenye mikataba na hospitali, narudi pharmacy kule ghorofa ya nane labda watanisikiliza, ajabu imefungwa!

Namfuata muuguzi wa mgonjwa wangu ananitaka niende pharmacy ya emergency iliyopo ghorofa ya pili ili nikajaribu kuwaomba wahusika wanisaidie dawa!?

Sasa imefika saa mbili Na nusu usiku, pesa nimekuwa, urasimu na matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati vinatugharimu Watanzania.

Wahusika angalieni hili pamoja na kuwepo Kwa namba za simu za wasimamizi ili kutoa msaada.
 
Inasikitisha sana huo urasimu na ubabaishaji aisee..mtu unaweza ukafa yaani daaah..kwa kweli wajipange sana
 
Kwa Hali ilivyo ya urasimu sina Shaka kuna watu wanaumia sana.
Ni kweli usemavyo watu wanaumia sana, sasa huu ucheleweshaji wa huduma unadhani ni watu wote wanaweza kuuvumilia ndio maana malalamiko mengi
 
Hii nchi hii mambo mengi tunayafanya kwa kukurupuka,, mifumo mingi iliyoanzishwa haikufanyiwa majaribio ya kutosha. Kilichobaki ni tabu tu.
Kama ni kudhibit mapato kwa nini mgonjwa asitibiwe then malipo hayo yafanywe baada ya matibabu?
 
Nimewasikia watu kadhaa wakitaka kurejeshwa mfumo wa zamani wa malipo ya cash au crdb na machine zao za aspire wapate mpinzanj.
 
Nimeshuhudia mengi ikiwa ni pamoja na wagonjwa walioanzisha hospitali ya butimba mapema asubuhi wakapewa rufaa kwenda sekou toure, huko wakatumwa Bugando lkn hadi saa mbili usiku hawajapata huduma.
 
Ni kwamba hospitali imezidiwa au...
 
Ni kwamba hospitali imezidiwa au...
Yaelekea hivyo, au kushindwa kukabiliana na changamoto za mabadilikko.
Ilifunguliwa mwaka 1972 kuhudumia mikoa ya kanda ziwa. Bila Shaka leo idadi ya watu ni kubwa maradufu, lkn hili haliwezi kuwa sababu kubwa Kwa wenye kufikiri sawa sawa.
 
Tatizo hili lipo kweli lakini nasikia uongozi wa sasa una badilisha mfumo wote wa malipo (eleckronic) na kuja na ambao utaondoa usumbufu huu. Mfumo uliopo kwa sasa umekuwa kero sana ,
 
Yaelekea hivyo, au kushindwa kukabiliana na changamoto za mabadilikko.
Ilifunguliwa mwaka 1972 kuhudumia mikoa ya kanda ziwa. Bila Shaka leo idadi ya watu ni kubwa maradufu, lkn hili haliwezi kuwa sababu kubwa Kwa wenye kufikiri sawa sawa.
Ni kweli mkuu..jitihada madhubuti inabidi zifanyike kuhakikisha hili suala linaisha na nadhani Menejimenti ya hospitali ikiamua inawezekana
 
Back
Top Bottom