Hospital Za Bongo ni kwa ajili ya walala Hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospital Za Bongo ni kwa ajili ya walala Hoi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by AbrahamG, Oct 28, 2011.

 1. A

  AbrahamG New Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka mbunge wa kigoma Kwenye last session ya Bunge alichangia Hoja kwa kusema Hospital zetu zina hali ya chini kwa huduma kiasi kwamba Viongozi Hawakubali kutibiwa, akapingwa na baadhi ya wabunge, lakin hali hii inajionyesha sasa namba ya wabunge wanaokwenda na walioko india hadi leo hii.
   
 2. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja, Hizi hospital za bongo ni kwa ajili yetu sisi walalahoi tu.
   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=2]90 % ya viongozi wetu wenaugua magonjwa sugu , wanashindwa kufanya maamuzi[/h]
  Mapema mwaka huu viongozi wetu wa juu wakiwemo wabunge,mawaziri, majaji , wakuu wa mikoa, watendaji wakuu wa serikali walimiminika loliondo wakitaka kutibiwa magonjwa sugu ukiwemo ukimwi.mch ambilikile mwasapila (babu) aliwalaghai vigogo wa serikali na serikali yote kuamua kuelekea huko.
  Magonjwa sugu yaliyotajwa ni:
  1.ukimwi
  2.kisukali
  3.pressure
  4.
  5.
  Taarifa za daktari zinaonyesha kuwa watu wenye magonjwa sugu huwa wanhasira kali na kushinda kufanya maamuzi magumu na kukosa mipango endelevu. Wanauza mali hovyo na kutapanya rasilimali

  pamoja na kwamba dawa ya babu haitibu ukimwi lakini amefanikiwa kutupatia takwimu za ukweli kuhusu mtandao wa magonjwa sugu kwa viongozi wetu ambapo wametumia ndege kwenda loliondo na magari ya serikali.
  Ni dhahili kuwa viongozi wetu wanao tuongoza ni wagonjwa wa magonjwa sugu kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi mazito na mipango ya maendeleo y mda mrefu.

  Viongozi wetu wanahofu ya kufa kutokana na magonjwa yao na ndio maana wanauza madini, wanauza ardhi, wanauza wanyama hai mapema ili kukusanya pesa mapema.
  Wengi tunajua mtu akiwa na hofu ya kufa kutokana na ukimwi huwa anauza mali hovyo hovyo na maamuzi yake siyo mazuri.

  Mfano mzuri ni maamuzi ya kulipa dowans , jambo ambalo ni dhahili kwamba wanaofanya hivyo hawana mipango mirefu ya maisha katika taifa hili.
  Viongozi wa ccm wanakata kuachia madaraka kwa watu wengine wakihofia hatima yao baada ya kuuza nchi na wanyama nje ya nchi. Wametapanya mali hovyo kwasababu hawana mawazo mazuri, wanang'ang'ia madaraka na kutaka watoto wao walithishwe urais , ubunge, na uwaziri ili kulinda uhalifu waliofanya.wanahaha kuiba kura ili waonekane wanapendwa na wananchi.


  Mgogoro uliotokea libya ni sawa na mgogoro utao tokea tanzania 2015.
  Huko libya gadafi alitaka kuachia madaraka mikononi mwa watoto wake ambao nao wamejilimbikizia mali lakini raia wema wakamuonya lakini hakusikia.


  Hapa tanzania kuna juhudi kubwa za watawala wetu kutaka kurithisha madaraka kwa watoto wao ambao wamejirimbikizia mali katika vituo vya mafuta, migodi , maliasili, wameuza ardhi na sasa wanahaha kuiba kura.!!!!

  Kuna harakati kubwa kwa watu ambao wametuhujumu , wametuibia , wametunyonya na sasa haohao ndio wameunda mitandao ya urais 2015. Wanatumia fedha walizotuibia kutuhonga ili tuwape kura. Wanatumia pesa hizo kuwahonga wachungaji, wamewanunua wachungaji na kufanya kampeni makanisani.


  Watu hawa wakiugua tu utasikia walalahoi wanalalamika na kupiga kelele kuwa wamepewa sumu lakini safari ya loliondo walikwenda bila mtu kulalamika.wanasafiri kwenda india kutibiwa baada ya loliondi kupoteza umarufu lakini wanapo ondoka hawasemi wanaumwa nini !!!!!! Mauaji ya albino yanaongezeka ushirikina huku serikali ikiongeza kasi ya kutoa vibali kwa waganga .waliopo kwenda loliondo hawakusema wanaumwa nini!!! Lakini safari ya india ina maneno mengi


  ni bora mbunge ,waziri, vigogo wanapougua waangalie ukweli wa afya yake sio kusingizia sumu .

  Pia hapa kuna ubaguzi mpiga kura akiugua anafia nyumbani bila kufika hata dispensary, na hata akienda huko anakosa dawa.

  Wajawazito wametengewa bajaji ambazo bado zinasuasua.

  Waziri akiugua anakimbizwa haraka kwenda india na anagharimiwa fedha nyingi inayo weza kutibua zaidi ya walalahoi 100 hapa!!!

  Wakati wa kupiga kura wabunge wanapiga magoti kuomba kura, wakimunyima anachakachua!!! Je, ni haki????​
   
 4. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli,inasikitisha sana watu waliotuahidi kutuboreshea huduma za afya ndo kwanza hawapelekwe kwenye hospital zetu,watajuaje changamoto zilizopo kama sio data za kupikwa? ndo maana tunaimbiwa kuwa uchumi unakua kwa kasi ya panya ingawa maisha ya walio wengi yanazidi kudidimia kila kukicha,mi naona uchumi unakua kwa kasi hiyo mifukoni mwa mafisadi,so sad
  Mimi huwa nikihisi kuumwa nakuwa na mawazo mno coz nawaza kukutana na manesi waliokata tamaa hawawezi hata kumbembeleza mgonjwa,daktari anaetibu kwa maelezo tu bila vipimo, msururu mrefu kusubiri dawa,mazingira machafu sana ya wadi n.k. nimeamua kuwekeza zaidi katika imani.kweli inavunja moyo sana
   
Loading...