Hospital gani wanapima masikio?

Hospital gani wanapima masikio?

Mtundu wa Tech

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Posts
642
Reaction score
612
Habari!
Kutokana na title inavyojieleza hapo juu, nahitaji kufahamu hospital ya masikio hapa jijini Dar ambayo inapima kwa usahihi na kugawa vifaa vya usikivu ili kuongeza uwezo wa kusikia.

Maana kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa sana enzi za nyuma na kupelekea kupoteza uwezo wake wa kusikia na mwanzoni madaktari walisema chanzo ni homa ya uti wa mgongo (Meningitis) na mitaani wanasema alirogwa kwa sababu alikua ana akili sana darasani.

Hivyo nawaomba wataalamu waniambie hospital nzuri hapa Dar au kama kuna taasisi wanapima na kugawa vifaa vya kuongeza usikivu bure nipeni contacts zao na kama kuna hospital nzuri wanapima na kutoa hivyo vifaa tafadhari msisite kuniambia ili aende kwa uchunguzi zaidi.

Maana tatizo limekuwa sugu kwa sababu hii hali ilianza muda mrefu kidogo. Kuna kipindi alipelekwa Mloganzila akapima na kuandikiwa vifaa na aliambiwa kuna form aende hospital ya Taifa Muhimbil akajaze kisha vifaa vikija ataitwa ila mpaka leo kimya hatujui tatizo liko wapi.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa watakao nisaidia hili kupatikana kwa wataalamu au madaktari bingwa wa masikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua mzee nilikua na appointment na dokta bingwa pale Mloganzila na tulipokwenda tukamueleza vizuri tu na mhusika akapimwa na dokta alitolea ufafanuzi kwa kina.

Sasa baada ya kutoka kwa dokta ikabaki kwenye vifaa na tuliambiwa kuwa tuende Hospitla ya Taifa ya Muhimbili kuna form tunajaza na contacts zetu kisha tunaambatanisha na ile form ya dokta.

Baada ya hapo tukae kusubiri vifaa vikifika tuliambiwa tutaitwa kwa sababu walidai vifaa mpaka waagize sijui wapi.

Ila mpaka leo hii kimyaa sioni chochote ndio maana nimekuja humu kuomba alternatives kama kuna Hospital nyingine au taasis ili tumpeleke huyu jamaa
Nenda hapo hapo Muhimbili wapo vizuri lakini haujaelezea vizuri ukubwa wa tatizo lake . Poleni sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa
tookl.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom