Hoseah on ESCROW Scandal: No one would be spared

Ndio maana umeambiwa tulia wengi zaidi watafikishwa mahakamani,jamaa wa ardhi na tibaijuka wafikishwe mahakamani haraka sana
 
Dr MziziMkavu wanatuzuga tu hawa wahuni kama walivyofanya kwenye EPA na mabilioni ya Uswiss. EPA wakapindisha sheria kwamba wezi wamerudisha pesa zote kumbe ulikuwa ni uongo mkubwa. Walioambiwa waweke majina na wezi hadharani na kiasi kila mwizi alichorudisha wakashindwa kufanya hivyo. Rada yule mhindi Vethlani wakamuacha atoroke katika mazingira ya kutatanisha kwani alikuwa yuko chini ya ulinzi wa polisi na wahusika wengine akina fisadi Chenge mpaka kesho kutwa wanapeta na pesa zao za wizi. Werema mara ya mwisho alidai wahusika wa mabilioni ya Uswiss wamehojiwa alipoombwa kutoa majina akagoma sasa ndiye huyo hayumo tena Serikalini. Kikwete hajawahi hata siku moka kuzungumzia mabilioni ya Uswiss na huyo gaidi Mwigulu anaikimbia hii issue kama inavyokimbiwa Ebola.

Hivyo tusitegemee chochote cha maana kutoka katika hii Serikali iliyojaa wahuni, wezi na mafisadi. Watatuzugazuga tu na baada ya miezi michache hakutakuwa na lolote la maana dhidi ya wapokea rushwa na mtoa rushwa.


 
Last edited by a moderator:
Hawa Watakuwa ni Viongozi wasanii tu hakuna kitu hapo kitakachotendeka ni Usanii mtupu huo BAK
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Huyu bwana Dr.Hosea alitoroka JKT enzi hizo.Nashangaa leo ndiye mkuu wa idara muhimu hapa nchini.Usimwamini mtu aliyeshindwa JKT aweze kupambana na mijitu kama WEREMA.
 
Hili litapita tu kama la RICHMOND!
 

Fisadi MKUU ameishasema kwamba zile fedha zilizoliwa na majizi ya CCM sio za UMMA...sasa Hosea atawashtaki kwa kosa gani? CCM ni shedaaaaaaaaaaaa!
 

Utaambiwa baada ya Muhongo kujiuzulu kesi imeisha. Fedha hazitarudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…