Hoseah on ESCROW Scandal: No one would be spared

Mkuu Mani Hawa wahuni wanatuzuga tu, kumbuka mabilioni ya Uswiss ambayo ($529 million) ambayo Werema alitwambia uchunguzi ulianza tangu June, 2012 hadi hii leo zaidi ya miaka miwili na nusu hatujui nini kinaendelea. Si Kikwete wala Mwigulu ambaye anaweza kutwambia nini kinachoendelea. Tusishangae kusikia kwamba Hoseah amestaafu na replacement wake atateuliwa na Rais mpya.

Halafu cha kushangaza wanakamatwa waliopokea alie toa anapeta.
 
Last edited by a moderator:
Kodi kwa biashara ya mihadarati???

Naona kama TRA wanakimbia vishindo bila kujua ni vya nini.

Ninaona kushitakiwa kwa rushwa pekee, kunaweza kuongeza ujasiri na kuzalisha wezi zaidi. Kesi kama mara nyingi kama si zote, serikali hupoteza..

Maoni yangu, hii mikiki mikiki ya hosea kuisafisha serikali iionekane imechukua hatua iendelee. Lakini watanzania tunahitaji zaidi ya hapa:-

Kwanza majina ya waliochota Stanbic yawekwe hadharani kwa sababu, yanajulikana na wala siyo kwamba yakisemwa yataharibu upelelezi wakati ni order ya sku moja na kesho benki ya Stanbci wanatoa details na vielelezo vya accounts zote zilizobeba sandarusi.

Tunahitaji kwamba fedha zote zilizotolewa escrwo zirudishwe mara moja na zile za Tanesco zirudi tanesco.

Hatua ya kuwachukulia watumishi wa umma pekee, unawaacha kina singa, ruge na wengine wasio watumishi wa umma ni udhaifu mbaya na ni kulea mafisadi na uhusiano hujumu wa viongozi na majizi.

Kukimbiilia kudai kodi ni kutakatifisha fedha haramu!.
 
Kipindi cha Nyerere; Aliyepokea Rushwa na Aliyetoa Rushwa, woote hawa maziganyanza! Awamu hii, Mtoa rushwa ndugu Rugemarulila yeye hana hatia, ila kosa la rushwa lipo kwa waliopokea!
 
Reactions: BAK
Huyu anauwezo wa kula vidagaa tu...hayo meno aliyonayo hayawezi kufua dafu mbele ya papa....akitokea papa hapo huyu atajipeleka mwenyewe kumezwa....
Mkuu hawa wanafurahisha baraza tu unafikiri kuna kitu hapo jiulize ni kashfa ngapi zimewahi tokea na ni hatua zipi ziliwahi chukuliwa ,sana sana vidagaa ndo vinaiona joto ya jiwe
 
I have no confidence in this government and all of its machineries.
 
Reactions: BAK
PIGA UA HUNA LOLOTE HOSEA UNALOWEZA KUAMUA KATIKA SWALA HILI.Kwanza bila juhudi za Mh Kafulila na bunge hawa mafisadi usigewaona.Baado waliokamatwa ni dagaa yuko wapi CHENGEEEEEEEEEEE,Ngeleja na Mama wa Escrow.Pia rushwa lazima imuhusu pia Mtoa rushwa na mpokea rushwa yuko wapi RUGE na SETH.UBWEKE USIBWEKE KUTAKUCHA.Huna meno unafanya kazi kwa maelekezo, bora urudi usukumani ukalime pamba.
 
Reactions: BAK
Mbona mtoa rushwa hajafikishwa mahakamani? Kwa mujibu wa sheria mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana makosa!!

ccm ni ukoo wa panya; baba mwizi, mama mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, babu mwizi. bibi mwizi, mjomba mwizi, shangazi mwizi, mkwe mwizi! By Mh. Nassari.
 
Kipindi cha Nyerere; Aliyepokea Rushwa na Aliyetoa Rushwa, woote hawa maziganyanza! Awamu hii, Mtoa rushwa ndugu Rugemarulila yeye hana hatia, ila kosa la rushwa lipo kwa waliopokea!

UKAWA waanze kuorodhesha mambo kama haya ya kuwaambia wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu. Wanawakamata panya road lakini mapanya buku(majizi ya kalamu) yanaachwa yakatumie pesa za wizi.
 
Kwanini Habibi Seth hawampandishi kizimbani
 
Naam, hayo ni mambo ya Kikwete, asiyekuwa na macho haambiwi tazama. Asiye na masikio haambiwi sikia.
 
Danganya toto hyo. Wanatumia vyombo vya habari kuiamanusha public kuwa wanafanya kaz. Wakati hakuna kitu
 
Nnahisi kuna wajumbe wa PAC wanahojiwa na PCCB,
 
Uchunguzi utamalizika lini wakati zimebakia Miezi Michache kutafanyika Uchaguzi Mkuu? Maneno yako Mheshimiwa ndugu Dr Edward Hoseah yananitia wasiwasi huenda ikawa hao walioiba Pesa za ESCROW wasifungwe ninahisi patafanyika uchakachuaji mkubwa hapo.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…