Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.
Hapa hatukuja kulumbana, tumekuja kwenye semina, si mahala pake, lakini nyie wabunge ndio mlioamua kupitia Kamati Teule ya Bunge na mapendekezo yenu yapo, kwa hiyo iulizeni serikali, lakini hatuko hapa kushambuliana. Acheni kuhoji mambo hayo, kwani tukianza kuchambuana, hakuna atakayebaki salama !. Wapo wabunge wanaohudhuria semina zaidi ya tatu kwa siku moja na kusaini posho, lakini hata baada ya kuwezeshwa kwa posho hizo, hakuna uwajibikaji. Kwa kweli kuna mambo mengi yanayotokea, lakini tunayafumbia macho !
Najua unapenda historia na literature, utakuwa umemsoma Kaisari.
Isitoshe Kaisari ni favorite subject wa idol wako, Mwalimu Nyerere. Naamini umesikia mambo yake.
Kwa nini Kaisari alisema mke wake hatakiwi kushukiwa? Nini logic ya hiyo concept iliyo maarufu duniani?
Kwa hiyo hata wewe kamati yako inachunguzwa. Hiyo ni aibu!
Kwa nchi zilizoendelea ki utandawazi na uwajibikaji wa viongozi, hii ingekuwa ni kashfa kubwa kwa mtu kama Zitto, ambaye ndio kama mwokozi au mtume fulani wa kisiasa akatokea na yeye tume yake inachunguzwa.
Zitto shukuru Mungu uko kwenye uongozi nchi kama Tanzania ambapo kitu kama hicho watu hawajali.
Hapana Zitto, hapa sikubaliani na ushauri wako, kama TAKUKURU lazima wafanye huo uchunguzi basi Hosea akae pembeni la sivyo huku ni kutafutana uchawi !!
- Huyu ndiye Hosea aliyeisafisha Richmond akidai taasisi yake haikuona tatizo lolote na hiyo kampuni feki.
- Huyu ndiye Hosea aliyeonya kuwa watuhumiwa wa EPA ni wazito na wakikamatwa nchi itayumba.
- Huyu ndiye Hosea ambaye aliwajibu wazalendo waliomtuhumu kwa kushindwa kazi kuwa hajiuzulu ng'o na wakitaka washitaki kwa Raisi aliyemteua.
- Huyu ndiye Hosea anayetuhumiwa kwa mambo chungu nzima ya kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi.
- Huyu ndiye Hosea aliyeapa kulivalia njuga swala la Rada toka ripoti ya SFO itolewe halafu hivi leo kama kawaida anataka kula sahani moja na kamati za bunge zilizoanika janja yake na kumuumbua !
Zitto; kuna mgawanyo mzuri wa kazi na mgawanyo mbaya wa kazi. Kwa vile umetolea mifano taasisi za Marekani niseme hivi.
Taasisi mbalimbali za hapa zina uwezo wa kukusanya ushahidi ambao unaweeza kutumika mahakamani na zaidi ya yote zina uwezo pia wa kukamata (arresting power). Hivyo utaona kuwa idara hizi zina nguvu tofauti tofauti.
Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Marekani (iliyoko chini ya Wizara ya Biashara) ina wakaguzi wa aina mbalimbali lakini pia ina wale wanaoitwa "Special Agents" ambao ni maafisa wa kusimamia sheria wakiwa na nguvu za kuzuia, kukamata na kupekua kupata ushahidi. Wanapofanya uchunguzi na wanapoamini kuwa uhalifu umefanyika wana uwezo wa kumkamata mhusika na kukusanya ushahidi wa tukio la kihalifu na wakapelaka ushahidi huo kwa Waendesha mashtaka wa Marekani (Federal Prosecutors).
Wale FPs wao wanapitia ushahidi huo na mara nyingi wanafungua kesi kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na maafisa wa Mkaguzi Mkuu ambao huitwa kama mashahidi wa upande wa mashtaka.
Hilo pia linahusu FBI ambao kama unavyojua ni law enforcement agency. FBI wana uwezo wa kupekua kukamata na kukusanya ushahidi wa suala la kihalifu na ushahidi wao huuleta kwa FPs ambao hufungua mashtaka kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na FBI.
Kinachoepukwa ni kurudia uchunguzi mwingine tena. Yaani FPs hawaanzishi uchunguzi mwingine ila wasiporidhika wanawaambia watu wa hiyo idara kuwa ushahidi wao siyo mzuri n.k
Ni kweli tumeondoa uendeshaji mashtaka toka mikononi mwa Polisi lakini bado hatujajenga mfumo mzuri wa kushughulikia uhalifu. Kwenye suala hili tunalolizungumzia naamini CAG anapaswa kuwa na maafisa wa usimamizi wa sheria ambao wakati CAG anafanya uchunguzi na kukuta kuwa jambo fulani lina ushahidi wa kutosha wa uhalifu basi anaweza kumkamata mhusika na idara mojawapo ya CAG ikaandaa kesi na kuipeleka kwa Prosecutor ili waiendeshe.
Kwa kufanya hivyo, tutaondoa duplicity of roles isiyo ya lazima. Kama CAG kaingia Wizara ya Maji na katika uchunguzi wake kaona shilingi bilioni 2 hazina maelezo, kauliza nyaraka hakuna, kauliza vilivyonunuliwa hakuna; anaambiwa nileteeni ushahidi jamaa wanasua sua halafu yeye anaandika kwenye ripoti "nyaraka tuliagiza lakini hatukupewa" na ripoti inapokelewa ikionesha "ufisadi" wa bilioni 2. Hii ni kejeli.
Ingepaswa kuwa baada ya kuulizia taarifa muhimu toka Wizarani na hazipati maafisa wa CAG wawe na "trigger clause" katika sheria yao ambapo mhusika asipoleta taarifa za suala linalozidi shilingi milioni 1 basi wana nguvu ya kuitisha akaunti zake na za ndugu zake wa karibu, mali zake, na zaidi ya yote kumuweka kizuizini wakifanya uchunguzi. Na wakiona kuwa upo ushahidi wa suala la kihalifu basi ushahidi wote haupelekwi tena TAKUKURU bali kwa mwendesha mashtaka (wa wilaya, mkoa n.k, hata Tarafa kama tunaweza kuwa nao)
Jukumu la huyo mwendesha mashtaka utaona siyo tena kuanzisha uchunguzi wa jambo lile bali kuandaa kesi dhidi ya wahusika na maafisa wa CAG wanakuwa ni mashahidi wa upande wa mashtaka.
Nchi nyingine uchunguzi ukifanyika inakuwaje?
Posho zimewatajirisha saana Waheshimiwa wetu hawa. Wanalipwa kila wanakoenda hasa ile Kamati ya mashirika ya UMMA kiasi kwamba hawaoni kabisa jinsi mashirika haya yanavyotafunwa. Ile taarifa ya Mh Ndasa kuhusu TANESCO imeishia wapi?
Nchi nyingine wewe Zitto ungeweza kutakiwa ujiuzulu kuruhusu uchunguzi huru.
Na usingejiuzulu ungeweza kushindwa uchaguzi maana tayari una doa la kushukiwa ubadhilifu.
Zitto, wewe sio mbunge kama Chenge, wewe ni Zitto Kabwe, kamati yako inatakiwa iwe above suspicion kama mke wa Kaisari. Huwezi kuchunguzwa kwa rushwa bwana Zitto bwana. Ungekuwa nchi za watu waliopevuka ki uelewa, unaenda katikati ya nchi kutangaza chama na kukosoa ufisadi wa CCM watu wangekuuliza, wewe mwenyewe ulifanya nini hicho kilichofanya TAKUKURU wakushuku?
Nakwambia shukuru uko Bongo. Ila watu wa new school of leadership kama nyinyi ndio tulitegemea muanzishe hizo standard za hali ya juu kama nchi nyingine, kwamba kile kitendo cha kudhaniwa Zitto yuko katikati ya ubadhilifu ni kashfa, ni aibu. Utamkosoa vipi Mkapa na Yona na Chenge na Mramba wakati na wewe uko under a cloud of entanglement in corrupt activities?
Kama kweli hawa wabunge wetu wanalipwa posho mara mbili mbili kwa ujanja ujanja hiyo sio RUSHWA bali ni WIZI kwahiyo sio kazi ya TAKUKURU kupeleleza bali hayo ni makosa ya jinai na wenye kazi hiyo ni wakina Manumba huko polisi!! If it is true that PCCB is investigating the parliamentary committees then they cannot be doing so independent of directives from IKULU; this being another strategy of getting even with speaker Sitta and his colleagues!!
Nimekwambia ni Kamati zote zinachunguzwa ikiwemo ya Cheyo, Zitto, Slaa, Shellukindo, Anna Kilango, Missanga etc.
TAKUKURU ni zaidi ya Hosea. Hii ni Taasisi.
Haiwezi kuacha kufanya majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa sababu eti Bosi wao hatuna imani naye.
Lakini ni huyu huyu Hosea tuliyemfurahia kwa kuwafikisha kina Mramba mahakamani.
Tuchunguzwe tu na tukikutwa tumechezea fedha za Umma hatutakuwa na 'credibility' ya kuendelea kushika nyadhifa za Umma. (kesi ya Uingireza na Wabunge wao kutumia vibaya fedha ndio yaweza kutokea hapa nyumbani kufuatia uchunguzi wa TAKUKURU)
Nachoka kabisa!100% IKULU................ Spika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi. Inachunguzwa pia
Uchunguzi siku zote lengo lake ni kutafuta kama kuna mabaya. Hakuna uchunguzi wa kutoa zawadi za mazuri.
TAKUKURU wameshuku kwamba tume hizi, ikiwemo ya Zitto, kuna ubadhilifu, ndio maana wanachunguza. Hawaendi pale kutoa zawadi za birthday kwa kina Zitto, bali kuchunguza suspicion za ubadhilifu wa kina Zitto.
Hizo kamati nyingine sio jambo la ajabu, CCM ni wabadhilifu. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu, Mbunge wa upinzani, anaejiweka kama adui wa ufujaji na rushwa na ufisadi. Kamati yake inachunguzwa kwa kulipana kibadhilifu. Kashfa! Na unajua ni kashfa, Mwanakijiji; Unatetea kwa vile wewe huwa ni shabiki, unaendeleza "a mission." Ukishaniambia uko "on a mission" huwezi kuja kujaribu kunipotosha kwamba una chembe ya objectivity.
TAKUKURU wana wajibu wa kisheria kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kwamba Wabunge tumekuwa tukilipwa zaidi ya tunachotakiwa kulipwa kisheria. Wabunge hatuna kinga ya kufanya vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma na hatua hii ya TAKUKURU itaondoa 'impunity'. Kwamba wanafanya hivi kwa visasi sio kweli. Ni wajibu wao. Uchunguzi huu unafanyika kwa Kamati zote za Bunge na sio hizi tatu peke yake. Hivi kama Mbunge analpwa pesa ili asafiri kwa siku 5, na yeye anasafiri kwa siku moja. CAG anagundua hilo katika ripoti yake, kwa nini TAKUKURU wasichunguze na kufungua mashitaka?
Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.
Sawa, kwa hiyo uozo ndani ya taasisi hauhusiani na mapungufu ya kiongozi wake na ufanisi ndani ya taasisi hauhusiani na utendaji mzuri wa boss wake ! Mbona hiki ni kichekesho - kwa nini basi tunawalaumu viongozi wetu na kwa nini taasisi inapoboronga tunataka kiongozi wake awajibike. Mh. Zitto wengine hatutaki kabisa kusikia matamko kama yale ya Ikulu ya kudai Raisi asihusishwe na tuhuma za ufisadi ndani ya seriakli anayoiongoza.
Mbona hili linapingana na tabia ya ustaarabu kama ilivyo popote pale ulimwenguni. Kama hatuna imani na bosi wa taasisi yoyote dawa yake ni moja tu, hafai na tutadai kwa nguvu zote ajiuzulu au awajibishwe.
Ule usanii wa kuwafikisha mahakamani Mramba na wenzake wengine tuliukataa tokea mwanzo na siku zinavyosonga mbele, ukweli wenyewe unazidi kudhihirika.
Huyo kamanda anayeongoza jeshi hilo ndio tuna wasi wasi naye kutokana na rekodi yake ya nyuma baada ya kuisafisha Richmond na mambo mengine kemkem. Sisemi kamati hizi za bunge zisichunguzwe lakini Hosea kwanza awekwe kando. Madaraka aliyo nayo Hosea ndani ya TAKUKURU ni makubwa na mpaka sasa utendaji wake umekuwa hauridhishi.