MwanaKijiji ni suala la mgawo wa kazi tu kwani ikiwa CAG atafanya auditing na huyo huyo kuendesha mashtaka hapatakuwa na 'good governance' kwani principle inataka kila mmoja afanye kazi yake na kumwachia mwingine ili kuepuka mgongano wa maslahi ambao unaweza kutokea. Ndio maana hivi sasa tunaondoa waendesha mshataka kutoka Polisi ili kutofautisha kazi ya kuchunguza inayofanywa na jesh la Polisi na kazi ya kuendesha mashtaka iliyokuwa inafanywa na jehsi hilo hilo. Hivyo CAG akishaona kuna ubadhirifu yeye anaishia hapo maana yaya sio mtaalamu wa makosa ya jinai , mtaalmu wa makosa ya jinai ni DPP na kabla ya DPP kuchukua kesi ili kuendesha mashtaka Polisi wanafanya uchunguzi wao (na kama ni kosa la Rushwa, TAKUKURU wanaweza kufanya uchunguzi kuupeleka kwa DPP na kisha kuendesha mashtaka wao). Iwapo tukirundika auditing, uchunguzi na uendesha mashtaka kwa mmoja itakuwa na hatari (risk) ya Taasisi hiyo moja kuhodhi mamlaka na kuonea watu (absolute power corrupts absolutely).
Huu ni mfumo unaotumika katika nchi zote za kidemokrasia. CAG wa USA anaendesha mashataka? Au FBI wanaendesha mashtaka? Hii ni mifano ambayo itakuwa rashisi kwako kuchimba zaidi. Nadhani mfumo wa sasa ni mzuri na unaweka checks and balances. Huko mbele ya safari tutapa DPP anaefanya kazi kwa uadilifu, sujiali kaka
Zitto; kuna mgawanyo mzuri wa kazi na mgawanyo mbaya wa kazi. Kwa vile umetolea mifano taasisi za Marekani niseme hivi.
Taasisi mbalimbali za hapa zina uwezo wa kukusanya ushahidi ambao unaweeza kutumika mahakamani na zaidi ya yote zina uwezo pia wa kukamata (arresting power). Hivyo utaona kuwa idara hizi zina nguvu tofauti tofauti.
Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Marekani (iliyoko chini ya Wizara ya Biashara) ina wakaguzi wa aina mbalimbali lakini pia ina wale wanaoitwa "Special Agents" ambao ni maafisa wa kusimamia sheria wakiwa na nguvu za kuzuia, kukamata na kupekua kupata ushahidi. Wanapofanya uchunguzi na wanapoamini kuwa uhalifu umefanyika wana uwezo wa kumkamata mhusika na kukusanya ushahidi wa tukio la kihalifu na wakapelaka ushahidi huo kwa Waendesha mashtaka wa Marekani (Federal Prosecutors).
Wale FPs wao wanapitia ushahidi huo na mara nyingi wanafungua kesi kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na maafisa wa Mkaguzi Mkuu ambao huitwa kama mashahidi wa upande wa mashtaka.
Hilo pia linahusu FBI ambao kama unavyojua ni law enforcement agency. FBI wana uwezo wa kupekua kukamata na kukusanya ushahidi wa suala la kihalifu na ushahidi wao huuleta kwa FPs ambao hufungua mashtaka kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na FBI.
Kinachoepukwa ni kurudia uchunguzi mwingine tena. Yaani FPs hawaanzishi uchunguzi mwingine ila wasiporidhika wanawaambia watu wa hiyo idara kuwa ushahidi wao siyo mzuri n.k
Ni kweli tumeondoa uendeshaji mashtaka toka mikononi mwa Polisi lakini bado hatujajenga mfumo mzuri wa kushughulikia uhalifu. Kwenye suala hili tunalolizungumzia naamini CAG anapaswa kuwa na maafisa wa usimamizi wa sheria ambao wakati CAG anafanya uchunguzi na kukuta kuwa jambo fulani lina ushahidi wa kutosha wa uhalifu basi anaweza kumkamata mhusika na idara mojawapo ya CAG ikaandaa kesi na kuipeleka kwa Prosecutor ili waiendeshe.
Kwa kufanya hivyo, tutaondoa duplicity of roles isiyo ya lazima. Kama CAG kaingia Wizara ya Maji na katika uchunguzi wake kaona shilingi bilioni 2 hazina maelezo, kauliza nyaraka hakuna, kauliza vilivyonunuliwa hakuna; anaambiwa nileteeni ushahidi jamaa wanasua sua halafu yeye anaandika kwenye ripoti "nyaraka tuliagiza lakini hatukupewa" na ripoti inapokelewa ikionesha "ufisadi" wa bilioni 2. Hii ni kejeli.
Ingepaswa kuwa baada ya kuulizia taarifa muhimu toka Wizarani na hazipati maafisa wa CAG wawe na "trigger clause" katika sheria yao ambapo mhusika asipoleta taarifa za suala linalozidi shilingi milioni 1 basi wana nguvu ya kuitisha akaunti zake na za ndugu zake wa karibu, mali zake, na zaidi ya yote kumuweka kizuizini wakifanya uchunguzi. Na wakiona kuwa upo ushahidi wa suala la kihalifu basi ushahidi wote haupelekwi tena TAKUKURU bali kwa mwendesha mashtaka (wa wilaya, mkoa n.k, hata Tarafa kama tunaweza kuwa nao)
Jukumu la huyo mwendesha mashtaka utaona siyo tena kuanzisha uchunguzi wa jambo lile bali kuandaa kesi dhidi ya wahusika na maafisa wa CAG wanakuwa ni mashahidi wa upande wa mashtaka.