Hormons nyingi zinasababishwa na nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hormons nyingi zinasababishwa na nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Joyceline, Oct 20, 2011.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  binadamu wa kawaida asiyekuwa na tatizo lolote anatakiwa awe na hormons kiasi gani?
  nini kinasababisha kupungua au kuongezeka kwa hormons?
  Na kwa watu wenye hormons nyingi kupita kiasi cha kawaida cha binadamu tatizo linakuwa ni nini?
  Na mtu mwenye hormons kiwango mia nane na zinaongezeka ni hali ya kawaida?
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mwili wa binadamu una hormones nyingi sana zikiwa na kazi mbali mbali...na hivyo sababu zake za kuwa nyingi au kidogo ni tofauti pia, na hii inategemea na hormone husika inatengenezwa sehemu gani ya mwili.

  Kila hormone ina range ya kiasi chake cha kawaida kwenye mwili ili kuweza kutimiza effect husika (ni vigumu kiwango cha 800 unachoongelea ni kwa hormone gani). Lakini kutokana na hali au matatizo fulani, hormone hiyo inaweza ikawa nyingi kupita range ya kiasi kinachoptakiwa, au chache chini ya kiasi kinachotakiwa! Ikiwa nyingi husababisha overactivity ya system husika, na ikiwa kidogo basi underactivity, na hayo yote ni matatizo.

  Sababu tofauti kutokana na sehemu inayozalishwa hormone hiyo zinaweza kusababisha kuzalishwa kwa wingi...mfano kansa ya kiungo kinachozalisha hiyo hormone (mfano adrenal tumor, pituitary tumor etc), lakini pia kuna magonjwa au uvimbe mwingine ukasababisha kuzalishwa kwa kiasi kidogo cha hormones (mfano ovarian tumor).

  Ni rahisi kama ungekuwa specific unaongelea hormone gani ili kuweza kufahamu sababu specific zinazosababisha hormone hiyo ipungue au iongezeke mwilini!
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante DR. ninaishi na mdogo wangu kila siku alikuwa ananielezea sijui anajisikiaje mwili wake unachemka yaani maelezo mengine sikumuelewa nikampeleka hospital akapimwa kila kitu ila kabla ya majibu dr. akaniita pembeni akaniambia huyu ni nai wako nikamweleza, akaniuliza ni muhuni nikamjibu hapana, akaniambia ana hormons nyingi sana ni mtu ambaye hawezi kupitisha siku moja bila kulala na mwanaume ana hormons kiwango cha 800 na zinachemka sana na zinazidi kuongezeka ndo zinafanya ajisikie mwili kuchemka na mambo mengine. Nadhani nimejitahidi kujibu, Kuna jinsi naweza kumsaidia kwa njia za kidaktari labda dawa na ni nini kinasababisha? maana Dr. ameniambia amezaliwa hivyo hivyo hamna kilichosababisha. Nataka kumsaidia kwa sababu bado ni mwanafunzi inaniumiza sana.
   
 4. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  masikini poleni, isikuumize! mpeleke kwenye mazoezi ya mwili, (michezo mbalimbali)

  Dr Riwa uko wapi?? maelezo yako yanahitajika hapa
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Humo ambako nimeweka red kwa kweli kumenifanya nitafakari sana na kujaribu kukumbuka kama somo hili labda lilinipita wakati niko shule...lakini sidhani, japo nilikuwa nasinzia sometimes darasani lakini si kiasi cha kumiss point kama hiyo katika career yangu. In short, SIJAWAHI KUSUKIA KITU KAMA HICHO wakati nasoma na hata kufanya kazi kama daktari! Ulimpeleka hospitali gani? na alionwa na daktari wa kiwango gani kitaaluma (Clinical Officer, Asst Medical Officer, Medical Doctor au Specialist)? Alifanyiwa kipimo cha kupima hormones gani?

  Yes, mwili wa binadamu unatawaliwa na hormones, na kwa masuala ya uzazi, hormones za mwanamke zinatofautiana kidogo na zile za mwanaume. Ila sijajua bado kama kuna hormone fulani ya kike ambayo mwanamke akiwa (kwa kuzaliwa) nayo kiwango cha 800 basi mwanamke huyo mwili unamchemka, anakuwa muhuni, na hawezi pitisha siku bila kulala na mwanaume.

  Matatizo mengi ya hormones huwa yanatibika kwa dawa (hormonal manipulation therapy) ambapo hizo dawa either zinaongeza au kupunguza uzalishwaji au uwezo wa kufanya kazi wa hormone husika. Ikishindikana kuna wakati inabidi kufanyiwa upasuaji ili kuondoza tezi au uvimbe unaozalisha hormone hiyo kwa wingi.

  Nashauri mpeleke dada kwa daktari (medical doctor) afanye kipimo kinaitwa hormonal profile (watamcheck hormones mbali mbali) lakini omba pia specifically achekiwe Thyroid function (TSH, T3 and T4) nadhani huko kuchemka mwili kunaweza kusababishwa na kuongezeka kwa Thyroid hormones (lakini hizi hazisababishi uhuni wala kulala na wanaume hovyo!).
   
Loading...