Elections 2010 Hooray...Arusha Imeshakombolewa!

Wakuu kuna watu tulikuwa na kamjadala jana kwenye laga zetu aste aste!!

Nashangaa kuna watu bado wanaamini CCM itashinda tena kwa asilimia 65%!! Duh!

Jamani twendeni hiyo SUNDAY bila hiyana tupabadilishe uongozi!!!
 
baada ya mimi kumchagua DK SLAA,HALIMA MDEE,NA DIWANI WAO WA CHADEMA nitakuwa hapo JJ namshughulikia yule ''mdudu'' na grants kwa wingi sana:smile-big:

KARIBU SANA
Moyo wangu waumia sana kwakuwa niko mbali, amakwahakika ningekuunga mkono ndugu kwa 100%
 
Wakuu, jana 27/10/2010, Kamanda Mbowe alikuwa Arusha, ambapo walifanya mkutano wa kampeni wa Historia hapa mjini, katika viwanja vya NMC!...Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini Bwana G.Lema alihutubia huku masaa yote akishangiliwa na umati ambao ulivunja rekodi hata ile ya Mkutano uliohutubiwa na Dr Rais Slaa mwenyewe.

Katika hatua ya kushangaza na kukubalika kwa CHADEMA mjini Arusha, nilifurahi kugonganisha macho na Ndugu Felix Mrema, Mbunge aliyetupwa kushoto katika kinyang'anyiro cha safari hii, na ambaye amekuwa Mbunge wsa CCM kwa vipindi kadha, akiwa kwenye gari la taasisi fulani, huku akicheka muda wote katika hali ya kufurahia jinsi wanaArusha watakavyofanya mageuzi ifikapo 31/10/2010, na kummwaga Batilda.

Arusha imekombolewa tayari!, tuangalie kwingineko, Kamanda NGONGO, kazia maarifa hapa.
View attachment 15819
Hapa ni baada yaMwenyekiti wa Mkoa wa Chadema kumkaribisha Kamanda Mbowe ahutubie.
View attachment 15818
WanaArusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya G.Lema
View attachment 15817
Hapa wakishangilia
View attachment 15816
Eneo la NMC-Unga LTD ambako mkutano ulifanyika.

kaka huu mziki ni soo.
Jamaa hawalali ni vikao kwa kwenda mbele hadi milango ya nane nane ,tisa usiku wanapanga nini wafanze kujinasua na hili gharika!!
matokeo ndo kama hayo ya prof Majembe ooh Magembe kufkia kuropoka hovyo.
 
Siku ya ahadi imefika kwa watanzania..

Chagua dr. Slaa - raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania

chagua godbless lema - ubunge arusha mjini

chagua estomih malla - diwani kimandolu
 
Back
Top Bottom