Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,418
Waungwana,
Binafsi nitangulize shukran zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na afya tele. Pia nitume salamu zangu za pongezi kwa Mh Turkey na uongozi mzima wa kampuni ya Zan Fast ferries kwa kufanikiwa kuanza tena safari za usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya visiwa vya Zanzibar na Dar es salaam kupitia meli yao mpya iliyoingia hapa nchini hivi karibuni.
Hili si jambo jepesi hata kidogo hususan ikizingatiwa kwamba mshindani wake ndani ya sekta hii ni kampuni ya mfanyabiashara mkubwa Mzee S.S.Bakhressa kupitia kampuni yake ya Azam fast ferries. Hakuna haja ya kumzungumzia sana Mzee Bakhressa na utashi wake wa biashara maana Leo si siku yake, ila ipo haja kubwa sana ya kumpongeza Mh. Turkey na kampuni yake kwa kutuletea ushindani huu wa kibiashara.
Kama tujuavyo, popote pale unapokuwepo ushindani wa kibiashara, mtumiaji wa mwisho wa bidhaa au huduma husika ndio huwa mnufaikaji mkuu. Kwa ajili hiyo basi nichukue fursa hii kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuhakikisha ushindani huu unabakishwa kwa manufaa mapana ya wananchi wake. Serikali zisikubali kuja kuingizwa katika mtego zikajikuta kwa namna moja au nyengine zikitowa upendeleo wa namna yoyote ile kwa kampuni yoyote ile jambo ambalo linaweza kudhoofisha kampuni nyingine na kupelekea kushindwa kumudu ushindani na hatimaye kufa.
WASIFU WA ZANZIBAR 1:
Name: ZANZIBAR 1
Owner: ZAN FAST FERRIES
Designer: COCO YATCH BV (HOLLAND)
Builder: PLENTY SHIP BUILDING INDUSTRY CO. LTD (CHINA)
Capacity : 500 PASSENGERS
Maximum Knots: 40knots
Time from Zanzibar to Dar: 75 minutes.
Year Built: 2019
Kwa uongozi wa Zan Fast Ferries, tunawaomba muhakikishe huduma zinazopatikana ni Bora kabisa na ni za hali ya juu kuanzia kwenye ukataji wa ticket mpaka abiria anaposhuka kwenye chombo chenu huku akiwa amehitimisha safari yake. Hakikisheni kauli za wafanyakazi wenu ziwe nzuri na zenye kutambua mteja ndio mfalme.
Kwa jamii kiujumla: itakuwa ni busara kuiunga mkono kampuni hii kwa kusafiri nayo ili iweze kutoa ushindani kwa Azam Fast Ferries kwa sababu ukiwepo ushindani huo tutakaofaidika ni sisi wanyonge.
Naomba kuwasilisha!
FIRST CLASS
BUSINESS CLASS
ECONOMY CLASS:
TOILETS