Lighton
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 1,904
- 3,099
Nawazungumzia wanawake ambao ni wazazi/wenye watoto ambao wamefikisha umri wa miaka 18+ na 25+ Ambao mpaka watoto wao wanafikia umri huo, wamekuwa na maadili ambayo ni mfano mzuri wa kuigwa Kwenye familia.
Watu wengine watasema, "ni Bora kuishi vile unavyopenda Haijalishi watu wanasema au wanafikiria nini, Au wengine ambao husema "Haijalishi unaishi vizuri namna gani watu wakiamua kukuchukia watakuchukia tu. Lakini ukweli ni kwamba ukitenda jambo la hekima na busara Kwenye jamii watu wengi watakupenda na kukuheshimu na wapo watakaobadilika.
Nimezungumzia wanawake kwasababu Hawa ndio walezi, Haijalishi wanajishughulisha na nini, Lakini wamewekeza Nguvu zao zaidi kwenye familia.
Niliwahi kumsikia Mama akimlaumu Baba Kwa kumkatisha kazi mama kwasababu ya kuwa karibu na familia, ilinichukua muda kuja kuiona point ya baba, kwamba kweli Kama isingekuwa vile basi sijui tungekuwaje mpaka hivi tulivyo 26+ and 30s.
Mama yetu alitusimamia kidete, alikuwa mkali ni hatari, cha ajabu pamoja na baba kuingilia kati mifumo ya uleaji wa mama, Lakini sijawahi kuhisi kwamba mama alituonea. Mama yangu alinichapa, lakini baadae alinipatia zawadi ya kunifariji, Alikuwa mkali ilipobidi. Miaka michache iliyopita, aliniambia "Nimewalea mpaka kufikia umri huo Sasa nimemaliza kazi yangu, mtajua wenyewe mbadilike au muendelee kuishi hivyo mlivyo.
Nilikuja kugundua kwamba mama alijiwekea mission kwamba itaanzia mda gani na itaishia mda gani. Hawezi kusahau siku aliyofanya maamuzi ya kumuuma kwasababu ya kumtii mume wake.
Sasa hivi yupo hukoo, viijijini na Mume wake wanasema wanamalizia maisha Yao huko.
Mwanamke ni kiumbe mwenye ushawishi zaidi. Ushawishi wa kubadilisha jambo jema kuwa baya na jambo baya kuwa jema. Mwanamke ni kiumbe anayeweza kuifanya dunia ikawa katika hali tofauti.
Wanawake wakiamua, Kutakuwa na maadili na heshima kwenye familia na jamii kwa ujumla. Kulea watoto,kumuheshimu mumewe na kufanya kazi Kwa bidii.
Hongereni wanawake mliofanikiwa katika hili🔥