Ndugu wanaJF, ofisini ninapofanya kazi akitokea mbunge kutoka kambi ya ushindani kuchangia hoja bungeni wafanyakazi wanasogea karibu na screen ya TV na anapotokea wa CCM wanarudi kwenye viti vyao maana wanategemea kusikia: "Mheshimiwa spika/naibu spika/mwenyekiti, kwanza, kabla sijasahau naunga mkono bajeti kwa 100%. Halafu mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, serikali imewasahau wakulima vijijini, mfano, ni jimboni kwangu. Hakuna barabara, umeme, maji, zahanati na pia wakulima hawana masoko ya mazao yao kwa sababu mkuu wa wilaya amekataza wakulima kuuza mazao nje ya wilaya. Na wanaokaidi wanakamatwa na polisi na kushtakiwa. Halafu mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, polisi wanawabambikia wananchi kesi na wanawatesa... Asante mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, naunga mkono bajeti 100%." Je, ofisini kwetu au mahali penu pa kazi inakuwaje?