Hongereni wabunge kutoka vyama shindani mnatetea maslahi ya Watanzania, wenzenu ya chama chao

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, ofisini ninapofanya kazi akitokea mbunge kutoka kambi ya ushindani kuchangia hoja bungeni wafanyakazi wanasogea karibu na screen ya TV na anapotokea wa CCM wanarudi kwenye viti vyao maana wanategemea kusikia: "Mheshimiwa spika/naibu spika/mwenyekiti, kwanza, kabla sijasahau naunga mkono bajeti kwa 100%. Halafu mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, serikali imewasahau wakulima vijijini, mfano, ni jimboni kwangu. Hakuna barabara, umeme, maji, zahanati na pia wakulima hawana masoko ya mazao yao kwa sababu mkuu wa wilaya amekataza wakulima kuuza mazao nje ya wilaya. Na wanaokaidi wanakamatwa na polisi na kushtakiwa. Halafu mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, polisi wanawabambikia wananchi kesi na wanawatesa... Asante mhe spika/naibu spika/mwenyekiti, naunga mkono bajeti 100%." Je, ofisini kwetu au mahali penu pa kazi inakuwaje?
 
Mimi ni mmoja wapo. Akiongea upinzani ndio huwa nasikiliza, maana ndio huwa wana upeo wa kutosha ! Ila tukubali kuwa CCM wamegundua kuwa hawakubaliki na ndio maana kuna biasness ya wazi bungeni
 
Ofisi yetu huwa tunazijadili hoja madhubuti za washindani na kuzipondz na kuzicheka hoja dhaifu .....
 
Leo nilikuwa napita maeneo ya stend kuu ya mabasi arusha,nikaona watu wamejazana kwenye duka la tv,,ikabidi nisogee,nikagundua ni wakati ule kambi ya upinzani wanawakilisha hotuba yao,,mara baada ya kukau tishwa watu wote walsambaratika na kuendelea na shuhuli zao..nikasema yaani huyu speaker angepewa nafasi ya kuona kinachotokea huku kwa raia angetulia hukku akijua mwisho wa chama chake umefika
 
Back
Top Bottom