FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 41,026
- 47,152
Mkuu mbona hujaeleweka. Hii picha ni ya eneo gani? Kama ni Jiji mbona inaonekana ni tope tena sio changarawe au lami
Nimefurahi sana kuona jinsi jiji lilivyopangiliwa vizuri kutokana na kazi kubwa mnayoifanya bila kuchoka.., yaani hapa kodi zetu mnazokula kila mwezi zinaenda kihalali kabisa (Big up sana!) hii picha ni ushahidi tosha kabisa!!
![]()
Hongera pia kwa halmashauri ya Jiji la DSM na VIONGOZI wake hasa ndg Meya wa Ilala Jerry Silaa kwa kulifanya jiji kuwa safi sana lisilo na taka na lenye harufu nzuri..Meya wa Jiji Msomi na Mbunge Mstaafu wa A.Mashariki Dr.Didas Massaburi kwa kazi zao wanazo fanya na kuonekana usiku na mchana!
Viongozi wa Jiji na Mipango miji wanapiga kazi sana..Juzi kati waliwafukuza wafanyabiashara soko la Ilala baada ya Kugoma wakawaruhusu kisha "Mipango Miji" wakaamua kulifunga Soko la Michikichini kwa Kiberiti! Kudos kwa wazee wa Dengue!
Hhahahahaha...! Aisee kula like jembe.., yaan nimeipenda hii mpaka basi.., u made my day......! hahahahah...!!!!
Heehehe..., si unabonyeza tu kitufe cha like...nielekeze namna ya kumpa like na mimi.. kanikosha jamaa
Na mimi pia nawapongeza akina jerry slaa na viongozi wote kwa kazi mahiri, iliyotukuka na yenye umakini wa kiwango cha hali ya juu ya kupanga vizuri mji wetu wa dar. Nawashauri wawape somo viongozi wengine barani africa kuiga mfano wa mipango miji, jiji la dar es salaam.