Hongera Yanga Kurudisha Utani wa Jadi kwa Uteuzi Mpya.

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,799
71,220
Lazima ni declare interest kuwa mimi ni mwana Simba halisi. Lakini natoa pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa uteuzi wao wa Idara ya Habari kwa kuchagua vijana wasomi, wenye weledi na hekima.

Uteuzi huo umerudisha ule utani wa jadi kwa timu hizi Simba na Yanga utakao ongeza chachu ya maendeleo ya mpira badala ya hali iliyopo sasa ya ugomvi, uadui na fitina.

Kuna mtu ambaye alidhani yeye ni superior katika Soccer kiasi akawa na matusi kwa kila mtu, kebehi na majigambo huku akijinadi anachukiwa na watu kwa kuonewa wivu. Huyo ndio alijenga huu uadui, sasa baada ya kufungiwa na TFF na huku Yanga kapigwa chini basi sasa ni mambo mapya.

Simba na Yanga za sasa ni taasisi kubwa sana. Zinatoa ajira kubwa, biashara na kodi pia burudani kwa Watanzania kupunguza stress zao, sasa kwa nini kuziweka katika mikono ya matapeli? Watu wenye chuki na fitina? Hapana, hongera Yanga kwa maamuzi sahihi.

Hata hivyo pamoja na pongezi hizi, mechi ijayo ya Simba LAZIMA MLE KICHAPO

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani huyu Ali kamwe amechukua nafasi ya Bumbuli na sio manara wala sidhani kama Manari aliwahi kuwa afisa habari wa Yanga.
 
Back
Top Bottom