Hongera Waziri wa Elimu

Hongera Waziri wa Elimu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,531
Reaction score
6,270
HONGERA SANA WAZIRI WA ELIMU PROF. JOYCE NDALICHAKO KWA KUFAFANUA SUALA LA KATAZO LA MICHANGO MASHULENI.
Kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana wa maelekezo yanayotolewa na viongozi wa ngazi Zach juu wa serikali yetu,jambo linalonipa faraja ni utaratibu unaofanywa na Viongozi wa juu wa Serikali kuchukua hatua katika kurekebisha baada us kuona utekelezaji ukipingana na maekekezo wanayoyatoa,nakumbuka kuna wakati hata Rais Mh :John Joseph Pombe Magufuli aliamua kuwaita baadhi ya viongozi na kuwaeleza alichokuwa akimaanisha baada ya kuona "suala la uwajibikaji na uwajibishwaji (utumbuaji majipu)ukitekelezwa kwa namna ambayo sivyo alivyoelekeza nakumbuka alisema....."Mimi na Makamu wangu tumezunguka Nchi nzima kuomba kura.... "akionesha kutofurahishwa na utekelezaji wa maagizo anayoyatoa.
Hali ya namna hiyohiyo imejitokeza kwenye Wizara ya Elimu ambapo zuio la michango shuleni limetafsiriwa kwa namna tofauti kabisa na maelekezo ya Sera ya Elimu ambapo kinachofanyika mashuleni kuhusu suala la michango Waziri mwenye dhamana amestushwa.
Tuna sera nzuri lakini shida ipo kwenye utekelezaji wa sera zetu .
Sera kama kipimio cha Serikali inaweza ikaruhusu au ikazuia au ikaelekeza mienendo binafsi iwe namna ipi,lakini pamoja na hayo yote suala la msingi ni katika kutekeleza,sera ikieleweka vizuri na kutekelezeka inazaa matokeo yaliyotazamiwa,Sera huwa inaeleza nini cha kufanya na nini si cha kufanya.
Mathalani kama Serikali inataka kufanikisha jambo huwa inaandaa taratibu za kuwafanya Wananchi waishi katika namna ya kutekeleza jambo hilo,Sera ya Elimu ni utaratibu unaotutaka Wananchi kuishi katika namna ya kufikia malengo ambayo Serikali yetu imejiwekea kwenye Elimu.
Kuandaa Sera ni mchakato mrefu na unaogharimu sana kwa msingi huo kufanya mambo yetu tofauti na Sera ni jambo la hatari kwa sababu Serikali kupitia Wizara mbalimbali hujipima kupitia utekelezaji wa sera zake na hii ni kutokana na ukweli kuwa Serikali inapoandaa sera yoyote huwa inatekegemea matokeo kutokana na sera hiyo kutekelezeka(utekelezaji mzuri sera husababisha matokeo tazamiwa ya sera" good impementation of public policy assures predicted outcomes of that particular policy)
KUNA SHIDA HUKU CHINI
Inafahamika miongoni mwa mazingira mazuri us utekelezaji wa Sera ni:
(i)Sera husika kuongozwa na nadharia nzuri za kijamii,mbinu,na teknolojia.
(ii)Malengo yasiyokinzana(clear and non conflicting goals)
(iii)Kukubalika.
(iv)Usimamizi mauri.
Kwa nini utekelezaji wa Sera unatofautiana na Maekekezo:
(i)Baadhi ya Wasimamizi wa sera kushindwa lurkers nini ambacho Viongozi wa juu yao wanataka wakifanye.
(ii)Kuvuja kwa Mamlaka (leakage of authority),Maelekezo yanavyotoka juu kuja chin(top-down approach)ujumbe wa maelekezo unaweza kutafsiriwa tofauti.
Kwa mfano hata Kipindi cha Ujamaa kuna Waikati wasimamizi wa Sera walikuwa wakitekeleza tofauti kabisa na maelekezo hadi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kufikia hatua ya kusema "SIKUELEKEZA HIVYO"
(iii)Kuna wakati wasimamizi wa Sera wanapopatiwa majukumu hawaoneshi kukataa ila hawafanyi kile walichoelekezwa(coping mechanism)
Tanbihi:Kinachofanywa na Serikali kutoa ufafanuzi na kurekebisha pale inapoona kuna upotofu ni jambo zuri litakaloiwezesha Serikali kuvuna matunda iliyotazamaia kuyapata kutokana na Sera hizo.
Victor Mlakimtoto Wa Wilbard
 
Back
Top Bottom