Hongera wanasheria jamiiforums

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
115
159
PONGEZI sana Kwenu ninyi Wanasheria ambao mnajitambua kuwa nanyi mmetoka katika MAISHA ya kawaida na wengine kutoka katika MAISHA nafuu na mkabahatika kusoma iwe Kwa shida au Kwa raha na kufanikiwa kuwa Wanasheria.

Wengi wenu mnatambua hali ya UELEWA wa Mtanzania kuhusu sheria, na nadhani mkabuni na kuweka ili Jukwaa la Sheria ili kuelimishana kuhusu Sheria.

Ninawapongeza Kutokana na kuonyesha Kwenu KUKERWA na mchangia Mada aitwae ' Witch Hunter' katika Uzi "Amedhalilishwa Kwa kutukanwa na kuambiwa kuwa ameua"

Katika Uzi huo huyo mchangiaji alionyesha Utoto sana. Sina muda wa kupoteza kueleza Utoto wake bali Wenye taaluma Yao 'Wanasheria' hamkuridhika na hamkukaa kimya na mkamueka Sawa, na kama atakuwa na Akili timamu sidhani kama ataleta huo ujinga wake wa kujiboost Tena.

Ukweli ni kwamba mmeliweka Sawa Jukwaa hili liwe wazi Kwa yeyote mwenye kutaka ufahamu wa sheria kama malengo yenu ya kuweka jukwaa hili.

Sidhani kama Jukwaa hili liliwekwa na maafisa Kilimo, Doctors au Drivers etc. halafu wakaliita Jukwaa la Sheria! Sikuwa member wakati wa kuanzishwa hili jukwaa lakini malengo Yao ni kuelimishana kuhusu Sheria.

Na ni ninyi Wanasheria ndio mlilolianzisha Kwa kuzingatia matatizo ya elimu ya Sheria Kwa waTanzania wengi. Leo anakuja mtu analeta Utoto kwenye suala la maana.

Namaliza Kwa kuwapongeza Wanasheria JF Kwa kutotaka Upuuzi na Utoto wa kijinga kwani Kwa wale tusio Wanasheria tulivunjwa MOYO kabisa na KUKOMA kujihusisha katika jukwaa hili kwani tuliona kuwa halituhusu, KUMBE ni mtoto tu aliona achafue Nanyi hamkukaa kimya kama ilivyo taaluma yenu na mkaliweka Sawa hili na mkamtolea Uvivu.

Tupo na tutaendelea kuwa Pamoja. Asanteni.
 
Back
Top Bottom